Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU
Viongozi wa chama cha akiba na mikopo cha watumishi wa manispaa ya songea mkoani
Ruvuma wametakiwa kuongeza kiwango cha
kutoa mikopo kwa wanachama wake ili waweze kujiimarisha
katika maisha yao
Baadhi ya wanachama wa sacco's wakiwa katika maandamano
Mkuu wa mkoa wa
Ruvuma said mwambungu ameyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa 20 wa
chama cha akiba na mikopo cha watumishi wa manispaa ya songea iliyofanyika katika
ukumbi wa songea club.
wanachama wa sacco's manispaa ya songea
Amesema mikopo
waliokopeshwa wanachama kwa ajili
ya ujenzi wa nyumba ni midogo
ukilinganisha na gharama za vifaa vya ujenzi.hivyo wanachama wanaweza kujenga
nyumba zilizo chini ya kiwango.
Mea wa mji bwana Chales Mhagama
Pia Viongozi wa chama
cha akiba na mikopo cha watumishi wa manispaa ya songea mkoani Ruvuma
wametakiwa kuendeleza utamaduni wa kuwa waaminifu katika kutunza mali na fedha
za wanachama wao.
Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti
Akisoma risala ya
mkutano mkuu wa 20 wa chama hicho mwenyekiti wa chama bwana Sky mpange amesema
chama kimejipanga kuongeza mikopo ya ujenzi wa nyumba kutoka shilingi milioni
nane hadi milioni kumi na mbili.
Mwenyekiti wa chama bwana Sky Mpange
Mpaka sasa chama kina jumla ya akiba za wanachama zaidi
ya shilingi milioni miatatu na laki
tisa, na kwa mwaka huu tayarikimekopesha wanachama wake zaidi ya shilingi
milioni miatatu na laki nane.
No comments:
Post a Comment