MKAZI wa Kijiji cha Tingunya Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma
aliyefahamika kwa jina la Matatizo Mohamedi (27 anashikiliwa na Jeshi
la polisi kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia katika tukio lililo tokea
kijijini hapo desemba 12 mwaka huu.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusidedit Nsimeki alisema
kuwa Mtuhumiwa huyo anashikiliwa kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga
Mwenzie kichwani kwa kutumia Mguu (Tendegu) la kitanda baada ya kutokea ugomvi
kati yao.
Akifafanua taarifa hiyo Kamnda Nsimeki alimtaja aliyefariki katika
tukio hilo kuwa ni mtu aliyefahamika kwa jina la Maulio Tikiri (14)
aliyedaiwa kupigwa na Tendegu hilo Kichwani na kupoteza maisha muda
mufupi baada ya kufikishwa katika kituo cha afya cha Nakapanya kwa
matibabu.
Kamanda Nsimeki aliendelea kufafanua kuwa taarifa za uchunguzi wa
awali zinaonesha kuwa chanzo cha ugomvi huo kilitokana na maerehemu
kutuhumiwa kuiba matita ya Nyasi ambazo walizikata katika eneo moja
kwa ajili ya kuezekea nyumba zao.
Alisema kufutia hali ya upotevu huo mtuhumiwa Mohamedi alimtafuta
marehemu Tikiri na baada ya kumuona alianzisha ugomvi huo ambao
ulisababisha mauti kwa mtu huyo aliyetuhumiwa kuiba nyasi hizo .
Alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za
upelelezi kukamirika ili sheria iweze kufuta mkondo wake.
Akizungumzia tukio hilo mganga aliye ufanyia uchunguzi mwili wa
marehemu Tikiri Dkt.Jeshi Daraja alisema kuwa chanzo cha kifo hicho ni
kutokwa na damu nyingi na kupasuka kwa fuvu la
kicha.
No comments:
Post a Comment