Mchungaji Shadrack Langu (katikati), wa kanisa la KKKT Amani akiwa na baadhi
ya watoto na kikundi cha VICOBA baada ya kukabidhi
Katibu VICOBA kanisa KKKT, Usharika Amani, Singida mjini Mwl Anna Abdalah
akikabidhi mafuta ya kula, ikiwa ni sehemu ya msaada
Na: Elisante John-Singida
KANISA la KKKT-Dayosisi ya kati Usharika Amani Singida
mjini, umetoa wito kwa madhehebu ya dini kusaidia makundi maalumu yasiyojiweza
ikiwemo watoto wanaoishi mazingira hatarishi.
Wito huo umetolewa na
Mchungaji wa usharika huo, Shadrack Langu, wakati wa makabidhiano ya msaada wa
chakula na vitu mbalimbali kwa kituo cha Malezi, Kititimo mjini
Singida.
A u, ili kujemesema
utoaji wa misaada hiyo kwa makundi yasiyojiweza, itasaidia kuijenga moyo wa
upendo baina yao.
Msaada huo wa kibinadamu uneotolewa na kikundi cha
VICOBA, chini ya kanisa hilo, kwa ajili ya kituo hicho, chenye jumla ya watoto
40.
Mchungaji Langu amesema moja ya majukumu ya kanisa ni
kuia jamii, hususani makundi yasiyojiweza ili kuwajenga kimwili na kiroho
baadaye wamudu maisha yao.
“Kazi ya kanisa ni kuhakikisha mwanadamu anakombolewa
katika maisha yake…ndiyo maana hata wamisionari walipokuja kwetu, walipojenga
shule, walijenga pia zahanati na hospitali ili kusaidia jamii kimwili,”alisema
mchungaji Langu.
Mapema akimkaribisha mgeni rasmi, katibu wa VICOBA –KKKT
Amani, Mwalimu Anna Abdalah aliwaasa watoto hao kuondokana na huzuni badala yake
wajione wapo sawa na watoto wanaokula, kulala na kuishi na sehemu nzuri wakiwa
na wazazi wao.
Kwa upande wake mwangalizi wa kituo hicho anayetumia
maisha yake kuishi na kuwahudumia watoto hao, Ali Makala alishukuru msaada huo
na kuiomba jamii kuiga mfano wa akina mama wa VICOBA kutoka usharika wa Amani
katika kusaidia kituo hicho.
Msaada huo unaojumuisha unga wa sembe kilo 150, mchele
kilo 100, mafuta ya kula, sabuni, maharage, mafuta ya kupaka, dawa ya meno,
kalamu, daftari, juisi, biskuti, miswaki na dawa ya kuulia kunguni, una thamani
ya zaidi ya Sh. Milioni 1.1.Chanzo Mjengwahabari
No comments:
Post a Comment