Friday, 28 December 2012

MKUTANO WA EWURA NA JUKWAA LA WAHARIRI WAFANA DAR

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu (kushoto), Haruna Masebu akielezea utendaji wa mamlaka hiyo wakati wa mkutano wa pamoja na wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wa kubadilishana mawazo, Dar es Salaam . Kulia ni Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari.
Mhariri wa habari wa gazeti la Daily News, Leonald Mwakalebela akiuliza swali wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari wa kubadilishana mawazo na uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu (kulia) akijadiliana jambo na maofisa wake muda mfupi kabla ya mkutano na Jukwaa la Wahariri kuanza katika Hoteli ya JB Belmonte Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), ABsalom Kibanda akizungumza na  Haruna Masebu Bosi wa Ewura.
Mkurugenzi Mkuu wa EWQURA, Haruna Masebu akiwakaribishwa wahariri kwenye mkutano huo
Mhariri Mkuu wa gazeti la Habari Leo, Joseph Kulangwa akiuliza swali kuhusu tatizo la maji wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Jukwaa la Wahariri Tanzania,  jijini Dar es Salaam. Kulia ni Tumiani Abdalah wa Daily News.
Mkurugenzi wa Maji na Maji Taka wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Mhandisi Mutaekulwa Mutegeki (kushoto) akielezea kuhusu mfumo wa maji safi na taka wakati wa mkutano na wajumbe wa Jukwaa la Wahariri (TEF), wa kubadilisha na mawazo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Umeme wa mamlaka hiyo, Mhandisi Anastas Mbawala na Mkurugenzi wa Uchumi wa Ewura, Felix Ngamlagosi.
Meneja Ufundi wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA, Gerald Maganga akifafanua jambo kuhusu masuala ya mafuta wakati wa mkutano na wajumbe wa Jukwaa la Wahariri (TEF), wa kubadilisha na mawazo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Gesi Asilia wa mamlka hiyo, Mhandisi Charles Omujuni.
Mkurugenzi wa Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA, Felix Ngamlagosi akifafanua jambo kuhusu utendaji wa mamlaka hiyo wakati wa mkutano na wajumbe wa Jukwaa la Wahariri (TEF), wa kubadilisha na mawazo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maji na Maji Taka wa EWURA, Mhandisi Mutaekulwa Mutegeki.
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA, Miriam Mahanyu (kushoto) akifafanua jambo kuhusu utendaji wa mamlaka hiyo wakati wa mkutano na wajumbe wa Jukwaa la Wahariri (TEF), wa kubadilisha na mawazo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Haruna Masebu.
Mhariri wa Habari wa gazeti la Habari Leo, Mgaya Kingoba akichangia hoja wakati wa mkutano huo. Kutoka kulia ni Joyce Shebe wa ITV na Mhariri wa Redio Uhuru, Godfrey Chongolo.
Mtangazaji wa Star Tv, Tom Chilala akiuliza swali kwa uongozi wa Ewura. Kushoto ni Mhariri wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Abraham Ojuku.
Mhariri wa Redio Uhuru, Godfrey Chongolo akiomba muongozo katika mkutano huo. Kulia ni Joyce Shebe wa ITV.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo akifafanua jambo wakati wa mkutano huo
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri, Nevile Meena akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda (kulia) akiongoza mkutano wa wahariri wa kubadilishana mawazo na uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Haruna Masebu.(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO