Friday, 21 December 2012

Wanafunzi 16,578 wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2013 Ruvuma.


SONGEA     
                  Katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma HASSAN BENDEYEKO akitangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2013
Jumla ya wanafunzi 16,578 wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2013 ambao ni sawa na asilimia 54.2 ya waliochaguliwa.Kati  ya wanafunzi hao wavulana waliochaguliwa ni 8088 na wasichana ni 8490 na ufaulu huo umeongezeka kwa asilimia 8.1 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2012 ambao ulikuwa asilimia 46.1 .


Katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma HASSAN BENDEYEKO amesema wanafunzi 16,463 wamepangwa katika shule 135 zilizojengwa kwa nguvu za wananchi , halmashauri na serikali.

Afisa elimu wa mkoa  Ruvuma bi Mayasa Hasimu amesema hali ya matokeo ya ufaulu kwa ujumla sio nzuri kwakuwa wanafunzi  9158 waliochaguliwa ufaulu wao upo chini  kutokana na sababu mabalimbali kama vile,utoro, shule kutokaguliwa mara kwa mara, walimu kukaa kituo kimoja cha kazi muda mrefu na kushuka kwa ari ya kufanya kazi kwa walimu kutokana na mgomo na kukosekana kwa motisha.
Afisa elimu  wa mkoa wa Ruvuma bi mayasa Hashimu amesema wanafunzi 103 wakiwemo wavulana 56 na wasichana 47 wamefutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu katika mtihani .
        Kaimu afisa elimu wa manispaa ya songea Concessa  Mbena amepongeza manispaa ya songea kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwa kufaulisha kwa asilimia 72.                                             

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO