Wazazi wanatakiwa kuwaangalia kwa karibu watoto wao katika kipindi hiki cha masika .
Ni Baadhi ya Watoto wakichezea maji machafu ambayo yanatililika kutoka maeneo mbalimbali
Kutokana na mvua ambazo
zinaendelea kunyesha katika Manispaa ya Songea Baadhi ya mashimo ya vyoo ya
zibuka na kutoa maji machafu yakiwa yameambatana na maji ya mvua ambapo watoto
wadogo wamefanya maji hayo ndio mchezo wao mkubwa katika michezo yao ya
kuchezea maji bila kujali machafu au laa.
Baadhi ya wafanya biashara
ndogondogo ususani wauza mboga wamekuwa wakitumia maji ya mito kuoshea biashara
zao ambazo ni za mboga na kuhatarisha maisha ya wakazi wa manispaa kiafya.
Muuza mboga za majani akitoka mtoni kuosha mboga zake kisha kuzikpeleka katika soko la kuuzia
Aidha baadhi ya maeneo ya
barabara yameharibika na mvua hizo na madaraja mbalimbali yamebomoka kutokana na
maji kuwa mengi sana hivyo kusababisha foleni ya magari ambayo yanapita katika
eneo hilo.
barabara ya bombambili,matarawe ilivyoharibiwa na mvua
No comments:
Post a Comment