Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na wananchi wa Kijiji
cha Monduli juu,Mkoani Arusha wakati alipokuwa akiwasili kijijini hapo
kwa ajili ya shughuli ya uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo katika
kijiji cha Mfereji Monduli juu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikaribishwa kwenye kijiji
cha Mfereji Monduli juu,wakati alipokuwa akiwasili kijijini hapo kwa
ajili ya shughuli ya uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akifunua kitambaa kwenye jiwe la
msingi kuashiria uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo,lililoko katika
Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wananchi wa Kijiji
cha Mfereji,Monduli Juu,mara baada ya kuzindua josho la kisasa la
Mifugo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa josho la kisasa la Mifugo,lililoko katika Kijiji cha Mfereji,Monduli
Juu.
Mifugo ikiingizwa kwenye Josho hilo,mara baada ya kuzinduliwa.
Wakazi wa kijiji cha Mfereji,Monduli juu wakimsikiliza Mh. Lowassa (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na wananchi wa Kijiji
cha Monduli juu,Mkoani Arusha wakati wa hafla ya uzinduzi wa josho la
kisasa katika kijiji cha Mfereji Monduli juu. ambapo ametoa wito kwa
wakulima na wafugaji nchini kuacha uhasama wa kugombea ardhi.
Amesema kuwa kila mtu ana haki yake
hivyo ni muhimu kwa jamii hizo kuheshimiana na kukaa pamoja kutatua
tatizo la ardhi kwa ajili ya malisho ya mifugo pamoja na kilimo.Kumekuwa
na matokeo mengi sehemu mbalimbali ya kupigana kuwania ardhi kati ya
wakulima na wafugaji, miongoni mwa maeneo hayo ikiwa ni mkoani arusha.
Amewaambia watu wa jamii ya kimasai
ambao ni wafugaji kuingia katika ufugaji wa kisasa utakaowazuia kuhama
hama kutafuta malisho ya mifugo yao.''Jamani watanzania wenzetu
hawatakubali mtakapovamia maeneo yao bila ya ruhusa ni lazima tuondokane
na tabia hii'' alisema.
No comments:
Post a Comment