Wakati idadi ya wanawake wenye
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiongezeka, asilimia 26.5 ya wanawake
Tanzania wamebainika kuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile.
Mfumo wa uzazi unaharibika
Watafiti wanabainisha kuwa kitendo
hicho licha ya ukweli hakifai kwa vile kinaharibu mfumo wa uzazi, kina
athari kubwa mno kwa mwanadamu, mojawapo ni ikiwemo uwezekano mkubwa wa
wahusika kuambukizana virusi vya Ukimwi kwa vile hakuna vilainishi,
hivyo kusababisha michubuko ambayo ndio njia kuu ya kuambukiza vijidudu
hivyo.
Mtafiti Mwanasayansi, Irene Mremi
kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini
Tanzania (NIMR) alitoa ripoti hiyo hivi karibuni hapa jijini Dar Es
Salaam.
Mremi akiwa na jopo la watafiti kutoka
NIMR anasema kuwa wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho
wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi na
Kuogopa kupata Mimba.
Vilevile alizitaja sababu nyingine za
wanawake kufanya mapenzi kwa njia hiyo ni kulinda usichana wao na
baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.
Sampuli za utafiti
Utafiti huo ulikusanya sampuli kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Tanga, Makete na Siha.
Mremi anasema “Utafiti wetu
uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea
na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa
bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani
Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo.
Imani potofu kwa wanaume
Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya
kwa ajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maaambukizi ya
VVU, kitu ambacho ni uongo, kwani huko ndiko kwenye kuchangia ukimwi
kwa haraka zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote. CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment