Wachuuzi wa vitunguu ambao hawakutaka kutaja majina yao katika eneo la soko kuu la Songea wakisubiri wateja wao.
.....................................................................
Na Amon Mtega ,Songea
WAFANYABIASHARA wa soko la mazese ,A, na ,B, lililopo kata ya Misufini manispaa ya Songea
mkoani Ruvuma wameulalamikia uongozi wa kata hiyo katika kitengo cha afya kwa
kushindwa kuwasiliana na uongozi wa manispaa wa kitengo hicho ilikufanikisha
kuondoa taka zilizofurika kwenye madampo yaliopo sokoni hapo na kusababisha
usumbufu kwa wafanyabiashara hao kwa kuwepo na harufu kali.
Wakiongea na mwandishi wetu wa demashonews kwa nyakati tofauti katika eneo la tukio hilo mmoja wa wafanyabiashara Jastin Robo
alisema kuwa taka hizo zimerundikwa hapo kwa muda mrefu licha bila kuzolewa
licha ya wao kuwajibika katika utoaji wa ushuru.
Robo alisema kuwa
madampo hayo tangu yawekwe taka hayazolewi na sasa kwa kipindi cha masika hii
kumekuwa na hali mbaya kwa takataka hizo kutoa harufu kali pamoja na kuchuja
maji machafu ambayo ni hatari kwa mripuko wa magonjwa hasa ya kipindu pindu.
“Sisi tunaulalamikia
uongozi wa kata hii hasa katika kitengo cha afya kwa kushindwa kulifuatilia
suala hili katika ngazi ya manispaa ili waweze kutatua kero hii maana sisi
wafanya biashara tunaumia kwa harufu chafu kama
hiyo”alisema Robo.
Naye mwanamama
Happnes Hyera anayefanyabiashara katika soko hilo alisema kuwa atha wanayoipata
katika biashara hiyo kutokana na dampo hilo
kufurika kwa taka ni kubwa sana maana hata ulaji wa chakula cha mchana
wawapo kazini hapo unakuwa ni washida sana .
“Mwandishi chakula cha
mchana tunakula hapahapa maana hatuwezi
kuondoka kwenda mbali kuyapisha madampo haya kwa kuwa biashara zetu zipo hapa na
wateja wakija wakiona hatupo hawawezi kufanya biashara “alisema Happnes.
Kwa upande wake
diwani wa kata hiyo Salum Mfamaji kwa tiketi ya CHADEMA alisema kuwa tatizo la
ujaaji taka huo unatokana na manispaa hiyo kutokuwa na vitendea kazi vya
kutosha maana kwa sasa magari ya kuzolea taka yapo mawili tuu na ambayo
yanafanya zamu ya kuzunguka katika kata mbalimbali.za manispaa hiyo.
Aidha aliwaomba
wafanyabisha hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kwa kuwa manispaa tayari
inashughulikia kuongeza vitendea kazi ili kufanikisha kukabiliana na changamoto
hizo kwa kuwa uzalishaji taka umeongezeka .
No comments:
Post a Comment