MBUNGE LEMA WA ARUSHA ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI
Na Mahmoud Ahmad, Arusha
Jeshi
la polisi mkoani hapa limemtia mbaroni mbunge wa jimbo la Arusha mjini
Mhe Godless Lema kwa tuhuma za uchochezi kwa wanafunzi kwenye chuo cha
uhasibu mwanzoni mwa wiki katika vurugu zilizotokea chuoni hapo baada ya
mwenzao kuuwawa juzi usiku huko maeneo ya njiro jijini hapa.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas
alisema kuwa Mhe Lema alikamatwa huko nyumbani kwake Njiro majira ya
saa 9 usiku.
Afande
Sabas alisema jeshi hilo linaendelea na mahojiano na mtuhumiwa na kuwa
katika tukio hilo zaidi ya watuhumiwa 14 walifikishwa mahakamani jana
na kuwa hao hawezi kuwaongelea kwani kesi yao ipo kwenye chombo hicho
cha sheria.
Pia
kamanda Sabas alisema kuwa Mh Lema anashikiliwa kutokana na vurugu
zilizotokea juzi kwenye chuo cha uhasibu na kuwa atafikishwa mahakamani
siku ya jumatatu.
Kwa
upande mwengine Kamanda Sabas alisema kuwa zaidi ya hao watu 14 na Mhe.
Lema hakuna mtuhumiwa mwingine aliyakamatwa. Awali ilisemakana wakili
wake Albert Msando nae amekamatwa.
Mnamo
siku ya Jumatatu mwanafunzi mmoja aliuwawa kwenye mitaa ya Njiro jijini
Arusha na watu wasiojulikana hali iliyoleta tafrani hadi wanafunzi hao
walipoleta vurugu chuoni hapo na polisi kutumia mabomo ya machozi
kuwatawanya.
Sekeseke
hilo lilimalizwa na jeshi la polisi baada ya wanafunzi kutotii amri ya
mkuu wa mkoa huo Magessa Mulongo na kuanza kuingia barabarani
kuandamana.
No comments:
Post a Comment