Mkuu wa wilaya ya Songea Bwn:Joseph Mkirikiti
Mkuu wa wilaya ya Songea
JOSEPH MKIRIKITI amelitaka shirika la mizinga kutumia wafanykazi wake wasomi
kutengeneza ajira za vijana ambao wengi hawana mwelekeo wa maisha.
Mkuu wa wilayay ya songea
amesema hayo wakati akidungua kikao cha tano cha baraza la wafanyakazi la
shirika la mizinga kilichofanyika katika manispaa ya songea mkoani Ruvuma.
Joseph Mkirikiti amesema
kikosi cha mizinga kina wasomi ambao wakitumika vizuri wanaweza kutumia taaluma
zao kutengeneza ajira za vijana .
Awali akitoa taarifa ya
ufunguzi wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa shirika hilo, Meja jenerali
CHARLES MUZANILA amesema kikao hicho ni utekelezaji wa siasa ya ushirikishwaji
wa wafanyakazi mahali pa kazi kama ilivyoagizwa na tamko la hayati baba wa
Taifa tamko namba 1 mwaka 1970 na sheria zingine za kazi kwa madhumuni ya
kuondoa migogoro sehemu za kazi na kuongeza tija.
Meja jeneral Chalres Munazila akisoma taarifa ya baraza la wafanyakazi wa shirika la mzinga
Meja jenerali Muzanila
amesema shirika la mizinga kwa muda wa mwaka mmoja limefanikiwa kusimika
mitambo mipyaya uzalishaji wa mazao ambayo ilizinduliwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mwaka
jana.
kuanzisha miradi mbalimbali
katika kupunguza utegemezi wa ruzuku kutoka serikalini kwa kutengeneza
samani,za kisasa za maofisini na majumbani, uuzaji wa milipuko na viwashiovya
kiraia kwa ajili ya wachimba madini na wapasua kokoto.
Wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa shirika la mzinga wakiimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya kuanza kikao.
Wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa shirika la mzinga wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Songea JOSEPH MKIRIKITI.
No comments:
Post a Comment