Mkuu wa mkoa Ruvuma azipongeza halmashauri kwa kupata hati safi
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amezipongeza halmashauri za wilaya na Manispaa mkoani Ruvuma kwa kupata hati safi kufuatia ukaguzi uliofanywa na mkaguzi wa hesabu za serikali kwa halmashauri zote za mkoa na kuwataka madiwani na watendaji kutobweteka na hati hizo safi bali wanapaswa kuendelea kufanya kazi kwa umakini mkubwa.
Pongezi hizo alizitoa wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kilichowajumuisha pia wabunge Kapten John Komba(Mbinga magharibi) na Gaudens Kayombo(Mbinga mashariki) pamoja na wakuu wa wilaya ya Mbinga na Nyasa ambapo aliwataka kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi kwa uadiliffu na kwa kuzingatia maadili ya utendaji kazi hiyo.
Alisema kuwa hati hizo safi zimetokana na kuwepo kwa uadilifu na ushirikiano baina ya madiwani na watendaji wa halmashauri hizo ambao unapaswa kudumishwa kwa maslahi ya wananchi zaidi na kwa kuzingatia upendo na uelewano miongoni mwao na kujenga utamaduni wa kumaliza tofauti zinazojitokeza kwa kuzungumza kwenye vikao na siyo kutengeneza makundi ya kusengenyana.
Aidha aliwataka madiwani kwa kushirikiana na watendaji kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri katika sekta zote muhimu ambazo ni elimu kwa kujenga nyumba za walimu na kuwa utamaduni wa kuwavutia walimu wanaopangwa kufanya kazi katika maeneo ya halmashauri hizo huku katika sekta ya afya akiwataka zahanati na vituo vya afya vijengwe na kukamilishwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo muhimu.
Pia Mkuu wa mkoa aliwataka madiwani kusimamia kwa ukaribu miradi mbali mbali inayoletwa na kutekelezwa katika maeneo yao ili kudhibiti vitendo vya ubadhirifu katika miradi hiyo kwa sababu baadhi ya miradi inayotekelezwa katika baadhi ya maeneo haiendani na thamani halisi ya fedha inayotolewa kwa sababu kunakuwepo na vitendo vya ubadhirifu kwa kukosekana kwa usimamizi thabiti.
Aliwataka viongozi hao kuonesha uwajibikikaji kwa vitendo katika majukumu yao kwa sababu wanaowaongoza na kuwasimamia wataiga mfano wa wao kama viongozi lakini wasipowajibika hata wananchi na watumishi wengine walio chini yao hawatawajibika ipasavyo.
Akitoa shukrani baada kwa mkuu wa mkoa mbunge GaudensKayombo alimpongeza mkuu wa mkoa wa mkoa pamoja na wakuu wa wilaya hizo mbilikwa utendaji wao wa kazi ambaon ni wa ushirikiano mkubwa hali inayowafanya hatawananchi kuiga kutoka kwao pamoja na kuwepo kwa changamoto katika sekta zotemuhimu zinazowagusa wananchi ambazo serikali inaendelea kufanya jitihada zakuzitatua huku akisema kuwa upatikanaji wa maji na salama kwa wananchi wa wilayaya Mbinga na Nyasa bado ni tatizo kubwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment