Waziri wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika akiipongeza Hoteli ya DoubleTree by Hilton kwa kuona umuhimu wa elimu kwa kukabidhi taa mia mbili kwa Shule
za Msingi zilizopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma , Shule zilizopewa
msaada huo ni Shule ya msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang'ula , Taa hizi zinazotumia Nishati ya jua pia ni rafiki wa mazingira.
" Taa hizi zitawasaidia
kuepeuka kutumia vibatari na mishumaa muda wa kujisomea kwa sababu ni hatari kwani vimekuwa
vikisababisha majanga ya kuungua kwa watoto wengi nchini ".
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joesph Joseph Mkirikiti alie kaa katikati na kutoka kulia kwake ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by Hilton Tanzania Bw. Judd Helman na alie kaa kushoto ni mkurugenzi
wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata wakati wa hafula ya kukabidhi msaada wa taa zinazotumia nishati ya jua.
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph
Joseph mkirikiti akiteta jambo na mkurugenzi
wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata (kushoto)
juu ya matumizi ya taa zinazotumia nishati ya Jua ambazo pia ni
rafiki wa mazingira kwa Wanafunzi wa darasa la Saba. Kulia ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by Hilton Tanzania Bw. Judd Helman .
Toka kushoto ni Mkurugenzi
wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata akiwa
ameshikilia taa na wakatikati ni mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph
Joseph mkirikiti akiwa ameshikilia taa na wa mwisho ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Judd helman
Mkurugenzi
wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw.
Judd helman akimkabidhi moja ya taa inayotumia nishati ya Jua mwanafunzi
wa Shule ya Msingi Liumbu iliyopo ndani ya manispaa ya Songea mkoani
Ruvuma .
Waziri wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika
hapa ni umati wa wanafunzi (Viongozi wa leo) kila mmoja akitaka ampe
mkono wa pongezi baada ya kumalizikla hafla ya kukabidhi taa za nishati
ya jua kwa shule nne za manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
Wanafunzi toka katika shule nne za msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang'ula na wakifatilia kwa makini hutuba iliyokuwa ikitolewa kabla ya
kukabidhiwa taa zinazotumia Nishati ya jua ambazo zimetolewa na Hoteli
ya DoubleTree by Hilton.
Wanafunzi hao wameishukuru Hoteli hiyo na
kusema taa hizo zitawasaidia kujisomea hata kipindi ambacho Umeme
umekatika majumbani hivyo kuongeza uwezo wao kielimu na kupunguza matumizi ya kununua mafuta ya taa kwa ajili ya kusomea
Naye Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata amesema
"tumeamua kufanya kampeni
hii ambayo ni endelevu tutakuwa tukigawa taa 200 za mezani
zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule
tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu
ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira vile vile tunaomba wahisani wengine nao wajitokeze".
Chanzo: www.demashonews.blogspot.com
No comments:
Post a Comment