Wanachama wa Shirika la Restless development wakiwa katika kongamano
Hawa ni wanachuo waliojitokeza katika kongamano la
Restless development
..........................................................................
Kauli
hiyo imetolewa na mkuu wa Wilaya ya Songea Bw, Joseph Joseph Mkirikiti
katika kongamano la vijana lililofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu
cha St. Augustine tawi la songea,
Kongamano
hilo liliandaliwa na Restless development shirika lisilo la kiserikali ambalo
linalofanya kazi na vijana katika nchi 11 ulimwenguni, ufundisha vijana na
jamii kwa ujumla kuhusu afya ya uzazi na makuzi, jinsia, stadi za maisha, elimu
ya uraia, ujasiliamali na kuwajengea uwezo vijana waliopo ndani na nje ya
shule. Lengo kubwa ni kuwaweka vijana katika mstari wa mbele katika kujiletea
maendeleo.
Joseph
Mkirikiti amesema kuwa vijana ni kundi muhimu na ndio chachu ya maendeleo katika
nchi yoyote ile na hakuna nchi iliyoendelea bila ya kuwatumia vijana kwani ni
kundi lenye nguvu na tajiri wa maarifa.
Hivyo kuachana na tabia ya kujivunia ujana
kanakwamba ujana ni wamilele badala yake waone kule wanakokwenda na wajielekeze katika fikra pana sio fikra finyu,
"
Lazima utambue ujana ni ndoto kwa sababu kila dakika unayoyafikiria ni machache
sana utayaota, ndoto zenu zisiwe
kutafuta ukubwa bali ziwe za kuwatumikia wanyonge,Nchi yetu inatumia rasilimali
nyingi kuwasomesha vijana ambao mwisho wa siku wanaishia mitaani bila kuwa na
ajira zinazoeleweka wala kujiajiri wao wenyewe walio wengi wanaosoma kwa
malengo yakuwa viongozi na wengine hubagua kazi na hata sehemu za kufanyia kazi
,tutumie vyanzo tulivyo navyo kuleta maendeleo”
Kongamano
hili limewakuwakutanisha vijana kutoka katika vyuo mbalimbali na shule za
sekondari zilizopo manispaa ya Songea ili kuongeza jitihada katika kutengeneza
sekta ya vijana iliyoimara.
Kwa upande wake Bw. Lucian Sengesela ambaye ni
mkufunzi wa chuo cha ualimu songea amesema ujana unakabiliwa na majukumu ya kuwa
mzazi wa sasa na wa baadaye ikiwemo changamoto mbalimbali za maisha,maambukizi
ya magonjwa hasa hatarishi kama vile ukimwi, changamoto za kimaadili, ukosefu
wa ajira na kumiliki rasilimali.
“
ukosefu wa ajira kwa vijana unachangiwa na maadili ya tabia kwani vijana wengi
kwa sasa hawana maadili hata maofosini wengi wao wako kisasa zaidi kwa kujiona wao ni wasomi, kubagua kazi kwa kujiona wao ni wasomi hawezi kufanya kazi
ambazo haziendani na hadhi yao, pia
wengi wao pale wanapopangiwa kazi vijijini hukataa kuripoti sehemu ya kazi ”
Nae
Bw. Nicas Ngumba ambaye ni mratibu wa
Restless development amesma wameona
haja ya kuandaa kongamano la vijana ili kuweza kujadili utambuzi wa fursa za
uzalishaji mali, ajira na kujiajiri kama msingi wa kutengeneza sekta ya vijana
iliyo imara, pia tuweze kutizama mfumo wa elimu na hasa ule wa vyuo ili kuweza
kuona uwaandae vipi vijana ili waweze kunufaika na fursa za uzalishaji mali ili
waweze kujiajiri wao wenyewe.
No comments:
Post a Comment