Friday, 8 March 2013

MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU ATOA ONYO KWA WALE WANAOUZA MAZAO YAO BILA KUSHIRIKISHA WAKE ZAO.



Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwangu akizungumza katika siku ya wanawake duniani

Mkuu wa Wialaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti akitambusha viongozi aliofatana nao

Mwenyekiti wa kamati ya wafanyakazi wanawake wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) Taifa dokta ANGELINA SANIKE akijitambulisha .
 Kikundi cha cha akina mama kikitoa burudani katika maadhimisho hayo
 Wanafunzi wa shule ya msingi wakicheza kiduku ya asili kwa kupigiwa ngoma za asili
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akitoa zawadi ya sale ya shule, madaftali na sabuni kwa mtoto yatima ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akitoa zawadi ya sale ya shule, madaftali na sabuni kwa mtoto yatima ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari

 Viongozi mbalimbali toka serikali wakifatilia kwa umakini kilichokuwa kinaenelea uwanjani
 Kikundi cha ngoma ya asili kikitoa burudani ya (Ngoma ya Lizombe)
............................................................


Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu katika maadhimisho ya siku ya wanawake dunia  iliyiadhimishwa kimkoa  katika kijiji cha Lusonga Wilaya ya Songea.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAIDI MWAMBUNGU amekemea vikali vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya wanawake katika mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha lusonga wilaya ya Songea hapo jana MWAMBUNGU amesema ni marufuku wanaume kuuza mazao yao bila kushirikisha wake zao. Na kwawale  wanaotenda hivo watachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa ni moja wapo ya ukatili dhidi ya wanawakePia  amesema serikali inafanya juhudi ya kutokomeza vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya wanawake.

Akisoma risala katika maadhimsho ya siku ya wanawake iliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Lusonga wilaya ya Songea mkoani Ruvuma afisa maendeleo ya jamii wa wilaya WENISARIA SWAI amesema kuwa katika mkoa wa Ruvuma wananawake ndio wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula na biashara lakini hawashirikishwi katika kutoa maamuzi.

Amesema wanawake wengi katika familia wananyimwahaki ya kushirikikatika kutoa maamuziya mgawanyo wa mapato yanayopatikana ingawa wao ndio wazalishaji na watendaji kazi wakubwa.Aidha shughuli nyingi zinazofanywa na wanaake hazina ujira hali inayosababisha ndoa kukosa malezi mema hatimaye watoto na vijana kuondoka nyumbani na kujiingiza katika makundi ya ombaomba mitani.

Naye mwenyekiti wa kamati ya wafanyakazi wanawake wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (talgwu) taifa dokta ANGELINA SANIKE ametoa wito kwa jamii kuelimsha watoto kike ili kuondokana na mfumo dume .

MKURUGENZI WA MAFUNZO YA UFUNDI JESHI LA KUJENGA TAIFA KANALI CHACHA WANYANCHA AFUNGA MAFUNZO YA UZALISHAJI UMEME KWA KUTUMIA NISHATI ITOKANAYO NA BAYOGESI (JKT MLALE)


Mkurugenzi wa mafunzo ya ufundi Jeshi la kujenga Taifa Kanali Chacha Muninka Wanyancha

Injinia wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemoakitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa mafunzo ya ufundi Jeshi la kujenga Taifa Kanali Chacha Muninka Wanyancha kuhusu mtambo utakao wekwa katika shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka mtambo.
 Mkurugenzi wa mafunzo ya ufundi Jeshi la kujenga Taifa Kanali Chacha Muninka Wanyancha akisikiliza melezo toka kwa mkuu wa Kambi ya JKT Mlale

..................................................................


Katika hafla ya kufunga mafunzo hayo Kanali Chacha Wanyancha  amewataka wahitimu watambue kuwa wanalo jukumu kubwa mbele yao baada ya kupata mafunzo ya uzalishaji umeme kwa kutumia nishati jadidifu itokanayo na Bayogesi kwa kuwa wao ndio watakaokuwa chachu ya uhamasishaji wa matumizi bora na sahihi ya nishati jadidifu katika  maeneo yao baada ya kuhitimu mafunzo haya. 

“Kufanya kwa mafunzo haya kutawezesha kufikia malengo ya Milenia, MKUKUTA na sera ya Taifa ya Nishati ambayo yanalenga katika upatikanaji wa nishati bora kwa lengo la kukuza uzalishaji mali na kuendeleza huduma za  jamii, pia  kutokana na mafunzo waliopata yatasaidia kupatikana kwa huduma bora za nishati mbadala na endelevu kutachochea kuchangia katika kupunguza  umaskini na uharibifu wa mazingira ambayo kwa sasa ni tatizo kubwa.

Katka  hutuba yake  Kanali Chacha Muninka amezitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau kwenye uendeshaji wa vyanzo vya nishati vijijini, kamavile ukosefu wa mitaji, uwezo mdogo wa kiutaalamu  na wa kiufundi, mabadiliko ya hali ya hewa  na athari za mazingira pia kutojua fursa zilizopo katika uwezeshwaji wa kuanzisha miradi ya aina hii. Changamoto hizi zinaweza  kumalizika iwapo kutakuwa na  ushirikiano wa karibu na wadau , wakala wa Nishati Vijijini na Taasisi za ndani na nje zinazojishirikisha  na nishati vijijini na masuala ya mazingira.

Naye Inocent Msua  amesema kuwa wakala wa Nishati vijijini wanatoa ruzuku kwa waendelezaji wa miradi ya nishati vijiji kama sehemu yake ya kuchangia  kukabiliana  na tatizo la mitaji. Wakala  hawa wa Nishati Vijijini wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha mabenki na taasisi nyingine za fedha za ndani na nje ya nchi kutoa mikopo yenye riba na masharti nafuu kwa waendelezaji wa miradi ya nishati vijijini hapa Tanzania.
Pia ameongezea kuwa tayari mpango huu kwa sasa unatekelezwa na benki za TIB,CRDB,NBC,NMB,TWIGA BANCORP na AZANIA. 
 

Thursday, 7 March 2013

SAI-BABA EXPLESS LA GONGA NA KUUA HAPO HAPO- SONGEA


 TUNAOMBA RADHI KUNAPICHA SINZURI KWA KUANGALIA ILA IMETUBIDI TUWEKE KWA AJILI YA KUONYESHA UKWELI WA JALI JINSI ILIVYOTOKEA

 Hili ndio Bus lililogonga  lenye namba za usajili T 690 BUW

Hawa ni abilia wakieleza namna ya ajali ilivotokea leo maeneo ya kwa Mburushi
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusdedit Nsimeki alie vua kofia akiwa katika eneo la tukio maeneo ya kwa Mburushi
Dereva wa Bus la Sai - Baba Expless  Bw. Robison Sanke (57
 Hii ndio pikipiki ya marehemu  Steven Adam (62) yenye namba za usajili  T 618 ATX
 Umati wa wasafiri wakiwemo wapita njia wakiangalia ajali hiyo mbayailiyotokea leo majira ya saa moja asubuhi, TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZINAZOFUATA HAPO CHINI KWANI ZINATISHA,
 Hivi ndivyo ilivyotokea ajali hiyo leo majira ya saa moja maeneo ya kwa Mburushi 
Mwili wa Steven Adam ukiwa umelala chini baada ya ajali

Bus la Kampuni ya SAI – BABA EXPLESS lenye namba ya usajili  T 690 BUW likiwa safarini kuelekea Dar Es Salaam likitokea Songea limepata ajali leo majira ya saa moja na nusu asubuhi maeneo ya kwa Mburushi mjini songea.
Bus hilo limemgonga Dereva wa pikipiki (yeboyebo) ambaya ni mkazi wa Liumbu Mletele aliejulikana kwa jina la Bw. Steven Adam (62) mfanya biashara ya maziwa .
 Marehem Steven alikuwa akielekea mjini kupeleka mazima yake kwa wateja ndipo alipotwa na mahuti hayo. Kwa maelezo ya wasafiri wamesema mwenye makosa ni dereva Pikipiki ambaye hakuwa makini barabari kwa kuendesha vibaya na kwamwendo kasi pasipo kuzingatia sheria za barabarani.

Wednesday, 6 March 2013

Wakazi wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamelalamikia uharibifu wa mazao mahindi na mpunga unaofanywa na mifugo.

Wakazi wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamelalamikia uharibifu mkubwa wa mazao yao ya mahindi na mpunga unaofanywa na mifugo aina ya ng'ombe walioingizwa wilayni humo kinyume na sheria.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa wilaya ya Tunduru mkuu wa wilaya hiyo ABDALLAH LUTAVI amesema ng'ombe hao wameenea katika maeneo mabalimbali ya vijiji na kushambulia mazao ya wakulima.


Amesema serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya wale wanaolisha mifugo yao katika mashamba ya watu na kuomba kikao hicho kiweke mkakati wa haraka kuzuia uingizwaji wa mifugo hiyo ili kujiepusha na njaa inayoweza kutokea kutokana na mazao kushambuliwa na mifugo hiyo.


Mkuu wa wilaya ya Namtumbo ABDALLAH LUTAVI alikuwa akizungumza katika kikao cha ushauri cha mkoa wa Ruvuma kilichofanyika katika manispaa ya Songea.


Naye mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mheshimiwa vita kawawa amesema ng!ombe hao wakiachwa kwa kipindi cha mwaka mmoja tu basi wilaya hiyo itakosa kabisa mazao.



 Kikao cha kamati cha ushauri cha mkoa wa Ruvuma kimewaagiza viongozi wa kila wilaya kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenda kuripoti shuleni kabla ya mwisho wa mwezi huu.


Agizo hilo limetolewa na wajumbe wa kikao hicho baada ya kupata taarifa kutoka kwa afisa elimu wa mkoa wa Ruvuma Mayasa Hashimu kuwa jumla ya wanafunzi 6300 waliofaulu hawajaripoti shuleni mpaka leo.

Hivyo kikao kikalazika kuwaomba viongozi kila mmoja kutumia nafasi yake kuwabana wazazi ambao hawajawapeleka watoto wao kuripoti shuleni.

Wajumbe wa kikao hicho wametoa muda kuwa mwisho wa kuripoti wanafunzi wote wasioripoti shule ni tarehe 20.3.2013,
Itakapofika tarehe hiyo kila mkuu wa wilaya anatakiwa kutoa taarifa ya wanafuznzi ambao bado hawajaripoti shuleni na  wazazi wao wamechukuliwa hatua gani za kisheria.

Akizungumzia sakata la wanafuzi wa kidato cha nne kufanya vibaya katika matokeo ya mtihani wao afisa elimu mayasa hashimu amesema baada ya kufanya utafiti amegundua kuna changamoto nyingi sana katika pande zote za wazazi walimu wanafunzi na serikali.

Kwa upande wa wazazi afisa elimu amesema wazazi wengi wanasahau wajibu wa kuona umuhimu wa watoto kwenda shule na kuhakikisha watoto wanhudhuria shule kila siku, kuwaandalia vifaa vya shule kama vitabu na kuhakikisha watoto wao wanapata chakula cha mchana.

Aidha wazazi pia wanatakiwa kutoa michango inayopitishwa na kamati  za shule au bodi ya shule.

Pia wazazi wametakiwa kujenga tabia ya kufuatilia maendeleo ya shule ya watoto wao na kukagua mahitaji yao na kubwa zaidi kuwajenga watoto katika maadili mema kwa kuhakikisha wavaa mavazi mazuri na kuwapatia mahitaji muhimu ya shule.

Afisa elimu huyo aliomba  marufuku  kuwa ngoma ya saka mimba ambayo ipo katika wilaya ya Tunduru ambayo inahamasiha watoto kupata mimba.

Kwa upande wa wanafunzi amewataka wajitambue na wawe na malengo na kujua nafasi yao katika jamii na kujijengea tabia ya kujisomea na kutembelea maktaba.

Akiwageukia walimu amewataka wafanye kazi zao kwa uaminifu, watoe notes zinazoendana na mihutasari,walimu watoro wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Akizungumzia serikali kuwajibika kwa upande wake kuhusu elimu amesema serikali inapaswa kuwasikiliza walimu matatizo yao na kuwasaidia pale wanapokuwa na shida.


Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU amepiga marufuku vitendo vya kuchochea vurugu katika mkoa wa Ruvuma katika kikao cha ushauri wa mkoa



 Mbunge wa jimbo la Namtumbo VITA KAWAWA wa kwanza kulia , katikakti ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya namtumbo  bwana kinana
 kulia ni mkurugenzi wa wilaya ya mbinga na mbunge wa jimbo la mbinga mashariki Gaudence Kayombo wakisikiliza jambo katika kikao cha ushauri cha mkoa.




Serikali mkaoni Ruvuma imepiga marufuku kuuza kanda zinazoenezanchuki na kuchochea masuala ya vurugu katika mkoa wa Ruvuma.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU amepiga marufuku vitendo hivyo katika kikao cha ushauri cha mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Songea club katika manispaa ya Songea.

Amesema serikali haitamvumilia mtu , kundi au kiongozi yeyote wa dini ama siasa atakayeonekana kuchochea machafuko na chuki miongoni mwa wananchi katika mkoa wa Ruvuma.

Ameongeza kuwa serikali kupitia jeshi la polisi itamkamata mtu yeyote mchochezi na kumfikisha mbele ya sheria bila kujali nafasi yake.

Mkuu huyo wa mkoa wa Ruvuma ametumia nafasi ya kikao hicho kuwaomba wakazi wa mkoa wa Ruvuma kushirikianan na serikali ili kuwafichua na kuwabaini wanaouza kanda za uchochezi za aina yeyote zinazoeneza chuki za kidini.

Aidha amewataka viongozi wa dini ya kiislamu na wakristo kupitia misikiti na makanisa kuhubiri upendo ,amani, na utulivu miongoni mwa wananchi.
Said Mwambungu amewasihi wakazi wa Ruvuma kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano wa kitaifa.

Tuesday, 5 March 2013

WAKALA wa Nishati vijijini kupitia wadhamini wa Rural Energy Agency (REA) kukijengea kikosi cha JKT Mlale mtambo wa kuzalisha umeme wa BIYOGESI ambao utakagharimu kiasi cha shilingi milioni 123


Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph Mkirikiti akisisitiza jambo katika ufunguzi wa mafunzo katika kikosi cha JKT Mlale

Meneja wa mafunzo na ujengaji uwezo Grace Mathew akitoa maelezo mbele ya mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti.
  Injinia wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemoakitoa maelekezo kuhusu mtambo utakao wekwa katika shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka mtambo.
  Injinia wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemoakitoa maelekezo kuhusu mtambo utakao wekwa katika shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka mtambo.
Shimo hili ni lamtambo utakao wekwa
 ......................................................................................
 WAKALA wa Nishati vijijini kwa kupitia wadhamini wa Rural Energy Agency (REA)wametoa mafunzo ya utengenezaji wa mitambo ya umeme ya Biyogesi kwa kikosi cha JKT MLALE ,842KJ kilichopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma pamoja na kuwajengea mtambo wa umeme huo kikosini hapo  utakao garimu milioni 123 ,ili kufanikisha kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo na uharibifu wa mazingira.

  Akiongea jana meneja wa mafunzo na ujengaji uwezo Grace Mathew mbele ya mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia sana katika hali ya kukambiliana na changamoto za ukosefu wa wa Nishati ya umeme pamoja na uharibifu wa mazingira kwa kukata miti kwa ajili ya mkaa na kuni.
 
  Methew alisema kuwa wameamua kutoa mafunzo kikosini hapo kwa kuwa watu wa sekta hizo za JKT ndio wenye uzalendo mkubwa wa kutoa elimu hiyo kwa vijana mbalimbali hasa waliyopo mafunzoni kwenye vikosi hivyo na kuwa vijana hao pia wataenda kutoa elimu hiyo kwa wananchi wengine ikiwemo na kuwatengezea mitambo hiyo ambayo garama yake ni nafuu.

 “Nasema ni garama nafuu kwa kuwa kunamitambo midogo kulingana na uhitaji wa mwanachi mwenyewe anavyohitaji matumizi yake ya umeme huo na kuwa sasa ni zamu ya watu wa vijini kunifaika na hiyo mitambo ya biyogesi na kuachana na tabia ya kuona umeme wanapata watu wa mijini tuu”alisema meneja huyo.
  
  “Vijijini siku zote walikuwa wakitoa michango yao  kwa serikali kupitia  ulipaji  kodi ya vitu mbalimbali ndani mwake kukiwemo na suala la umeme sasa ni wakati wa kuwatambua na wao kuwa wapate umeme ambao hawata kuwa na garama ya kuwajibika TANESCO kama ilivyo kwa umeme unaotumika mijini”alisema.
     
  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti akisoma hotuba yake wakati akifungua mafunzo hayo alisema kuwa ni vyema sasa suala hilo la umeme wa biyogesi lizingatiwe kwa umakini ili kuondokana na uharibifu unaofanywa katika misitu mbalimbali hapa nchini.
    
   Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa zoezi hilo likifanikiwa litasaidia sana hata kwa vijana ambao kwa sasa wamekosa ajira hivyo kwa kufanya kazi hiyo ya ujenzi wa mitambo hiyo kwao itakuwa ni ajira tosha  na hatimaye watainua uchumi ndani ya Taifa pamoja na uchumi wao .
       
   “Naomba niseme kwa moyo wa dhati umeme wa mtindo huo nimeshauona na nimeona manufaa yake hivyo ningeliomba hata kwa wabunge wetu wawapo mbungeni kuliongelea suala la umeme wa biyogesi kwa wananchi kwa kuwa ni sehemu ya ilani ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi CCM”alisema kuwa kila mwanachi anahaki ya kutumia Nishati hiyo.
          
  “Leo kikosi hiki cha JKT MLALE mnajengewa mtambo wa uzalishaji wa umeme wa biyogesi wenye thamani ya milioni 123 utakao kamilika ndani ya miezi miwili na kupata umeme ambao hauna ugovi na shirika la TANESCO je mngesubiri umeme wa gridi ya Taifa mgepata leo “alisema mkuu huyo wa wilaya.
       
 Alisema kuwa sina maana kuwa umeme wa gridi ya Taifa usifike Songea bali nasema wakati umeme huo unasubiriwa sisi tuwe na umeme mbadala ambao hauna garama ya kutumia na kwamba umeme huo hauna kuweka manguzo bali ni wewe na Nyumba yako.
      
  Naye Meja mkuu wa kikosi hicho Thomas Mpuku alipongeza jidihada zilizofanywa na watu wa Wakala wa Nishati vijijini kwa ubunifu wao mkubwa na kuendesha mafunzo hayo katika kikosi chake na kuwa yeye atahakikisha elimu hiyo inaendelezwa na wengine .

   Aidha Injinia wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemo ambaye anasimamia ujenzi wa mtambo huo katika kikosi cha JKT MLALE alisema kuwa ukifanikiwa kuwa na mtambo wa biyogesi kazi yako kubwa ni kutumbukiza taka unazo zizalisha kwenye mtambo huo ili kuendelea kupata umeme.

 Hata hivyo alisema kuwa wamesha pita katika maeneo  mbalimbali kutoa elimu hiyo na kujenga mitambo hiyo na sasa tayari wananufaika nayo na pia wataendelea kwenda katika maeneo mengine kutoa elimu hiyo.
    
Picha na habari kwa hisani ya  www.demashonews.blogspot.com

TUPE MAONI YAKO