Thursday, 17 January 2013

JIMBO KUU KATOLIKI LA SONGEA LAFUNGA MCHAKATO WA KUMTANGAZA SISTA BERNADETA MBAWALA KUWA MWENYEHERI

 Hili ni sanduku lililowekwa masalia ya Mtumishi wa Mungu  Sista Bernadeta Mbawala katika kanisa la jimbo kuu katoliki la Songea Mkoani Ruvuma ambaye 14.1.2013 jimbo lilifunga mchakato wa kumtangaza mwenyeheri kwa kuadhimisha misa takatifu na kusafirsha taarifa zake zilizokusanywa na mahakama ya mchakato.
 Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki Mhashamu Norbert Mtega akitoa wito kwa watanzania kuchangia mchakto wa kumtangaza sista Bernadeta kuwa Mwenyeheri. na baadaye mtakatifu.


 Maandamano yakielekea ndani ya kanisa kwa ajili ya kuadhimisha misa ya mchakato huo.

Masista wakiwa wameshika picha ya sista Bernadeta Mbawala 
 Masista wakiimba katika misa takatifu ya mchakato huo.
 Hao ni mapadre wa kanisa katoliki la Songea wakiwa ndani ya kanisa 

 Hili ni sanduku lililowekwa masalia ya Mtumishi wa Mungu sista Bernadeta Mbawala.

Jimbo kuu katoliki  la Songea leo limeadhimisha misa takatifu ya kufunga mchakato wa kumtangaza  sista BERNADETA MBAWALA OSB  kuwa mwenye heri na baadaye mtakatifu katika ngazi ya jimbo.
****************************
Akizungumza na waumini wa jimbo katoliki la Songea  Askofu mkuu wa jimbo la Songea  Mhashamu NORBERT MTEGA alisema jimbo kwa upande wake tayari limeshafanya utafiti na kukusanya   taarifa mabalimbali alizoziandika sista Bernadelta Mbawala, ambapo wamepata barua alizoandika enzi za uhai wake zaidi ya mia moja, na machapisho mbalimbali ya magazeti.

Pia walipata sala alizotunga mwenyewe na kuzitumia kusali lakini kazi kubwa ilikuwa ni kuhoji watu kadiri ya sheria za kanisa ambapo tayari wamehoji watu 83, wakiwemo mapadre na watawa kutoka Songea na njombe.

Askofu Mtega aliongeza kuwa kanisa sasa limechukua hatua ya  kuanza  kutafiti na kuzungumza hadharani  ili sista Bernadeta OSB aweze kupata heshima ya kutangazwa mtakatifu.

Askofu huyo wajimbo kuu katoliki la Songea Mhashamu Norbert Mtega katika Mahubiri yake hayo alisema kama sista BERNADETA OSB atafanikiwa kutangazwa kuwa mtakatifu atakuwa ni mtanzania wa kwanza kufikia hatua hiyo, na kuwaomba waumini waendelee kuomba ili mchakato huo ufanikiwe.

Alisema baada ya kumaliza mchakato huo wa ngazi ya jimbo kinachosubiliwa sasa ni kutokea kwa miujiza miwili  na miujiza hiyo itokee popote duniani, ukitokea muujiza kwanza basi sista Bernaderta  atatangazwa kuwa mwenye heri na ukitokea muujiza wa pili atatangazwa kuwa mtakatifu.

Askofu alitumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania kuchangia kwa hali na mali zoezi hili la mchakato kwa kuwa kunahitajika zaidi ya dola 20,000/= ili uweze kukamilika.

Aidha Askofu Mtega alimuelezea Sista Bernadeta OSB  Kuwa alizaliwa mnamo mwaka 27/10/1911  katika kijiji cha likuyufisi wakati huo kwa sasa ni manispaa ya Songea, wazazi wake ni Stefan Msikazonge na Agata Mayanda, alibatizwa 5/11/1911 peramiho, kipaimara alipata tarehe 8.12.1921 peramiho, na alijiunga na utawa 7.08.1929 peramiho, Nadhiri za kwanza alipata 11.11.1934  wakati huo hakukuwa na nadhiri za daima na alikufa ta29.11.1950.

Sista Bernadeta Mbawala OSB  kutoka nyumba ya mtakatifu Agnes ya chipole  maisha yake na wazazi wake yalikuwa ni ya sala na kuabudu sana na alikuwa anatokewa na moyo mtakatifu wa yesu n aalikuwa anazungumza sana na bikira maria na mtakatifu Agnes,

Aliugua sana lakini aliunganisha mateso yake nay a yesu kristu na hakuwahi kutamka kutafuta dawa za mitishamba, alitolea mateso yake kwa kuwaombea wakosefu na hivyo amewafundisha wakristu kuyapokea mateso kwa imani kwa kuwa mateso ni moja ya sala na sadaka.

Baada ya kufa kwake miaka 61 baadaye  kanisa limeshuhudia watu wakienda kusali katika kaburi lake na kufanikiwa mambo yao huku hakuna kiongozii wa dini aliyeagiza watu wafanye hivyo huo ni ushuhuda kuwa sista BERNADETA anafaa kuwa mtakatifu.

Kazi kubwa imefanywa na mahakama ya mchakato huo ya kuandaa taarifa za sista Bernadeta ambazo taarifa hizo zimekamilika na Askofu mtega ametia saini na kugonga muhuri tayari kwa kusafirishwa kwenda ROMA  kwa mchakato zaidi.

Naye padre CAMILIUS HAULE  naibu wa askofu aliyemwakilisha  askofu katika kufanya kazi kwenye Mahakama ya mchakato  huo  akiwa ni mtetezi wa haki  ametoa tamko .nanukuu  hakuna kitu chochote cha kutiliwa shaka kati ya yale yote yaliyokusanywa na mahakama ya mchakato na ndio yatamkwe hivyo.

Kwa upande wake waziri wan chi ofisi ya makamu wa Rais mazingira  dokta terezya huvisa ametoa ushuhuda mbele ya waumini kuwa amekuwa akiomba katika kaburi la sista Bernadeta na kupata mafanikio ikiwa pamoja na uongozi na ametoa mchango wa shilingi milioni mbili kwa ajili ya mchakto na ujenzi wa kanisa la lizaboni katika manispaa ya songea.

Taarifa za sista bernadeta ndio zinazosafirishwa kwenda ROMA kwa ajili ya kuendelea na mchakato zaidi lakini Masalia ya mwili wake yamebaki katika sanduku la mbao katika kanisa la jimbo kuu katoliki  la songea kwa wale wote wanaohitaji kusali katika masalia hayo wanaalikwa.

Wednesday, 16 January 2013

AJALI MBAYA YATOKEA ASUBUHI YA LEO WILAYANI TUNDURU KATIKA ENEO MTAA WA MUUNGANO

Mkazi mmoja ambaye ni mkazi wa Tunduru na jina lake halikuweza kufahamika kwa haraka kutokana na sababu zisizo zuilika amepata ajali mbaya leo asubuhi wakati anatoka nyumbani kwake na kuelekea kazini kwake ambapo ni katika duka lake ambalon anauza madawa baridi lililopoa makabala na benki ya NMB Tawi la Tunduru.
 
Dereva huyo amejikuta akiingiza Gari katika korongo lililopo katika mtaa wa muungano karibu na ofisi za tanesco wilayani Tundru ambapo alikuwa anavuka daraja lililopo katika eneo hilo na hatimaye kushindwa na kujikuta anaingia katika bonde ivyo kujisababishia michubuko katika mwili wake na kwa sasa anaendelea vizuri.
 
Wakazi wa eneo hilo a muungano wamewahasa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa makini pindi wanapoku wanaendesha ili kuepukana na ajali hizo

PAMOJA NA UJENZI WA BARABARA ITOKAYO MJINI SONGEA KUELEKEA WILAYANI TUNDURU KUFANYIWA UKARABATI LAKINI BADO BAADHI YA MAENEO NI BADOKERO KWA WASAFIRI.

Hii ndio hali halisi kwa barabar itokayo Songea kuelekea Tunduru katika maeneo ya kijiji cha Namingwea
Barabara ambayo inatokea Songea kuelekea Tunduru ambayo inafanyiwa ukarabati na makampuni mawlili tofauti ambayo ni Sogea Satom ambayo inadhamana ya utengenezaji wa barabara kuanzia Mjini Songea mpaka katika Wilaya ya Namtumbo ambayo inaonekana kuendelea vizuri na ukarabati huo na wapo katiaka hatuwa za mwisho za ukarabati huo.
Na kuanzia katika Wilaya ya Namtumbo mpaka wilayani Tunduru Kampuni ambayo inadhamana ya utengenezaji wa barabara hiyo ni Progressive ambayo inamilikiwa na wahindi,licha ya kampuni hiyo kusitishiwa mkataba wake wa ujenzi wa barabara hiyo lakini bado watumiaji wa barabara hiyo wapo katika wakati mgumu hasa katika kipindi hiki cha mvau.
haya ni baadhi ya magari ambayo yamenasa katika eneo hili
Magari mengi yakiwemo ya abiria na vilevile ya mizigo yameshindwa kuendelea na safari katika maeneo ya kijiji cha  Namingwea kilichopo wilayani Tunduru kutokana na halimbaya ya barabara na kusababisha magari hayo kukwema(kunasa)katika eneo hilo ivyo kusababisha abiria kushidwa kuendelea na safari zao na hata kukosa huduma muhimu kwani eneo hilo lipo polini sana na hivyo kuhatarisha maisha yao.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Tunduru bwana Chande Nalicho alipo kuwa anatoka Mjini Songea kurudi na kurudi katika wilaya yake ya Tunduru naye pia alikumbana na tatizo hilo ambapo alinasa katika eneo hilo la kijiji cha Nmigwea zaidi ya mala tatu(3) na kulazimika kushika chepe na Jembe kwa ajiriya kufanya jitihada za kulitoa gari ambalo lilinasa katika tope zito ilikuendelea na safari na zoezi hilo lilichukuwa takribani saa nzima mpaka kufanikisha kupita katiak eneo hilo la Namingwea. 
Mkuu wa wilaya ya Tunduru wa kwanza kushoto na Mkurugenzi wa wilaya hiyo wa pili kutoka kulia wakiwa mzigoni
Wananchi wengi wamekuwa waathirika wakubwa kwani hakuna njia nyingine ya usafiri wanayoitegemea kutoka songea kuelekea Tunduru na kutoka tunduru kuekekea songea na wakaiomba serikali ilingalie kwa umakini zaid lakini pia Mkuu wa wilaya hiyo nae pia akiwa ni mmoja wa waathirika wa ubovu wa barabara hiyo pia aliiomba mamlaka husika  na ujenzi wa barabara hiyo iliangalie suala hilo kwa umakini mkubwa sana..

Sunday, 13 January 2013

MDAU WA ELIMU WILAYA YA SONGEA JABIRI KILIHAMA AMETOA MSAADA WA MIFUKO 50 YA SALUJI KWA AJILI YA KUSAIDIA UJENZI WA HOSTELI KWA SHULE SEKONDARI YA MAHANJE


Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti 

MDAU wa elimu wilaya ya Songea Jabir Kilahama ametoa msaada wa mifuko hamsini ya simenti kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa hosteli kwa shule ya sekondari ya mahanje iliyopo Madaba ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu wanafunzi kwenda shuleni hapo.

Akizungumza jana mara baada ya kukabidhi msaada huo ,Mkurugenzi wa Lutukira mixed Farm L.T.D Kilahama alisema ameguswa na matatizo ya ukosekanaji wa hosteli hivyo akaona naye anajukumu la kusaidia ujenzi huo hivyo ametoa msaada wa simenti mifuko 50 .

"Nimevutiwa kuchangia maendeleo ya elimu kwa wananchi wa wilaya ya songea kwani elimu ndiyo msingi wa masiha, nimetoa mifuko hamsini kwa ajili ya ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa shule ya sekondari mahanje,"alisema.

Akipokea msaada huo jana Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph alimpongeza Kilahama kwa msaada alioutoa ambapo amewataka wadau wengine wenyeuwezo wajitokeze kusaidia maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo.

Amesema, bado wilaya inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya ujenzi wa mabweni, maabara za sayansi,nyumba za walimu, madarasa , matundu ya vyoo pamoja na ukosekanaji wa madawati.

JESHI LA ZIMAMOTO LATOA ELIMU YA KUKABILIANA NA JANGA LA MOTO SONGEA

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu 
Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Ruvuma Baraza Mvano
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu akizima moto
Askari wa Jeshi la zimamoto

Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Ruvuma  limetoa elimu kwa wananchi juu ya kukabiliana na majanga ya moto katika sehemu za kazi, majumbani na mashambani. 

Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani hapa BARAZA MVANO amesema jeshi hili limelazimika kutoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto kwa kuwa wanachi wanapopatwa na mataizo ya kuunguliwa nyumba ama mali zao hawatoi taarifa kwa wakati.

Amesema jeshi hili lina majukumu mengi yakiwemo ya kuzima moto wenye madhara, kuokoa maisha ya watu na mali zao , kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto , kukusanya madhuhuli ya serikali na kutoa mafunzo ya kinga na taadhari.

Pia amesema jeshi hilo limejiwekea mikakati ya kuelimisha wananchi katika wilaya zote tano za mkoa wa Ruvuma namna ya kuzima moto ili kupunguza madhara ya moto na wananchi kuelewa majukumu ya jeshi hilo.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabiti Mwambungu akatumia nafasi hiyo kuwataka wale wote wenye tabia za kuchoma moto barabarani na kwenye makazi ya watu waache  mara moja. Kwani uchomaji wa moto ni uhalibifu  wa mazingira na usababisha madhara makubwa sana hivyo serikali haitawafumbia macho.

Pia amewaomba wananchi wawafichue wale wote wenye tabia hizo sababu wanawafahamu hivyo wasiwaogope kuwafichua ili kukomesha majanga haya ya moto

Saturday, 12 January 2013

SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MAPINDUZI ZANZIBAR LEO

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikagua gwaride la Vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za kutimiza Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wakati alipomaliza kukagua gwaride la  Vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za kutimiza Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zabzibar.{Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho  Kikwete,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Salmin Amour Juma,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.

Wednesday, 9 January 2013

tarime kuchafuka tena

chacha1 7f8be
huku tarime inaonekana kama kuishi border ni mkosi sasa mkuu wa wilaya amezuia mahindi yasisafirishwe kwenda ndani ya maeneo mengine ya nchi kwa utashi wake mwenyewe
huku akisingizia kuwa yana sumu bila vipimo
lakini pia ameungana na TRA TARIME wanadai kila lorni 1 kulipa fine ya dola elf 5 je swali ukilipa fine ya dola elfu 5 sumu inaisha?
hii pia ni unyanyasaji mpya ulioibuka hapa mbaya zaidi madereva wa malori haya wanak amatwa na kupigwaa
tunaomba wizara ya kilimo,kazi ajira na vijana,viwanda na biashara,watusaidie kuliko kuingia uhalifu huku
sisi ni wakulima halali wa nchi kama sasa hata tutashindwa kujiajiri kwa mavuno tutafanya kazi gani?

TARIME IMEKUWA KISIWA HUWEZI KUFANYA KAZI KWA UHURU MAMLAKA ZINATUMIKA VIBAYA
sasa tunaamuliwa kuchoma moto shehena ama tusage mahindi tule!! zaidi ya tani mia 5 tutakula mpaka lini? na t ukisaga sumu inaisha?
kwa niaba ya wakulima na wasafirishaji wa nafaka Tarime
chacha heche katibu wa muda
chacha 399e5

TUPE MAONI YAKO