Hii ndio hali halisi kwa barabar itokayo Songea kuelekea Tunduru katika maeneo ya kijiji cha Namingwea
Barabara ambayo inatokea Songea kuelekea Tunduru ambayo
inafanyiwa ukarabati na makampuni mawlili tofauti ambayo ni Sogea Satom ambayo
inadhamana ya utengenezaji wa barabara kuanzia Mjini Songea mpaka katika Wilaya
ya Namtumbo ambayo inaonekana kuendelea vizuri na ukarabati huo na wapo katiaka
hatuwa za mwisho za ukarabati huo.
Na kuanzia katika Wilaya ya Namtumbo mpaka wilayani Tunduru
Kampuni ambayo inadhamana ya utengenezaji wa barabara hiyo ni Progressive
ambayo inamilikiwa na wahindi,licha ya kampuni hiyo kusitishiwa mkataba wake wa
ujenzi wa barabara hiyo lakini bado watumiaji wa barabara hiyo wapo katika
wakati mgumu hasa katika kipindi hiki cha mvau.
Magari mengi yakiwemo ya abiria na vilevile ya mizigo
yameshindwa kuendelea na safari katika maeneo ya kijiji cha Namingwea kilichopo wilayani Tunduru kutokana
na halimbaya ya barabara na kusababisha magari hayo kukwema(kunasa)katika eneo
hilo ivyo kusababisha abiria kushidwa kuendelea na safari zao na hata kukosa
huduma muhimu kwani eneo hilo lipo polini sana na hivyo kuhatarisha maisha yao.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Tunduru bwana Chande Nalicho alipo
kuwa anatoka Mjini Songea kurudi na kurudi katika wilaya yake ya Tunduru naye
pia alikumbana na tatizo hilo ambapo alinasa katika eneo hilo la kijiji cha
Nmigwea zaidi ya mala tatu(3) na kulazimika kushika chepe na Jembe kwa ajiriya
kufanya jitihada za kulitoa gari ambalo lilinasa katika tope zito ilikuendelea
na safari na zoezi hilo lilichukuwa takribani saa nzima mpaka kufanikisha
kupita katiak eneo hilo la Namingwea.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru wa kwanza kushoto na Mkurugenzi wa wilaya hiyo wa pili kutoka kulia wakiwa mzigoni
Wananchi wengi wamekuwa waathirika wakubwa kwani hakuna njia
nyingine ya usafiri wanayoitegemea kutoka songea kuelekea Tunduru na kutoka
tunduru kuekekea songea na wakaiomba serikali ilingalie kwa umakini zaid lakini
pia Mkuu wa wilaya hiyo nae pia akiwa ni mmoja wa waathirika wa ubovu wa
barabara hiyo pia aliiomba mamlaka husika
na ujenzi wa barabara hiyo iliangalie suala hilo kwa umakini mkubwa
sana..
No comments:
Post a Comment