Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti
MDAU wa
elimu wilaya ya Songea Jabir Kilahama ametoa msaada wa mifuko hamsini ya
simenti kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa hosteli kwa shule ya sekondari ya
mahanje iliyopo Madaba ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu wanafunzi
kwenda shuleni hapo.
Akizungumza
jana mara baada ya kukabidhi msaada huo ,Mkurugenzi wa Lutukira mixed Farm
L.T.D Kilahama alisema ameguswa na matatizo ya ukosekanaji wa hosteli hivyo
akaona naye anajukumu la kusaidia ujenzi huo hivyo ametoa msaada wa simenti
mifuko 50 .
"Nimevutiwa
kuchangia maendeleo ya elimu kwa wananchi wa wilaya ya songea kwani elimu ndiyo
msingi wa masiha, nimetoa mifuko hamsini kwa ajili ya ujenzi wa hosteli ya
wanafunzi wa shule ya sekondari mahanje,"alisema.
Akipokea
msaada huo jana Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph alimpongeza Kilahama kwa
msaada alioutoa ambapo amewataka wadau wengine wenyeuwezo wajitokeze kusaidia
maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo.
Amesema,
bado wilaya inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya ujenzi wa mabweni, maabara
za sayansi,nyumba za walimu, madarasa , matundu ya vyoo pamoja na ukosekanaji
wa madawati.
No comments:
Post a Comment