Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu
Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Ruvuma Baraza Mvano
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu akizima moto
Askari wa Jeshi la zimamoto
Jeshi la
zimamoto na uokoaji mkoani Ruvuma limetoa elimu kwa wananchi juu ya
kukabiliana na majanga ya moto katika sehemu za kazi, majumbani na
mashambani.
Kamanda wa
jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani hapa BARAZA MVANO amesema jeshi hili
limelazimika kutoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto kwa kuwa wanachi
wanapopatwa na mataizo ya kuunguliwa nyumba ama mali zao hawatoi taarifa kwa
wakati.
Amesema
jeshi hili lina majukumu mengi yakiwemo ya kuzima moto wenye madhara, kuokoa
maisha ya watu na mali zao , kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto ,
kukusanya madhuhuli ya serikali na kutoa mafunzo ya kinga na taadhari.
Pia amesema
jeshi hilo limejiwekea mikakati ya kuelimisha wananchi katika wilaya zote tano
za mkoa wa Ruvuma namna ya kuzima moto ili kupunguza madhara ya moto na
wananchi kuelewa majukumu ya jeshi hilo.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabiti Mwambungu akatumia nafasi hiyo
kuwataka wale wote wenye tabia za kuchoma moto barabarani na kwenye makazi ya
watu waache mara moja. Kwani uchomaji wa moto ni uhalibifu wa
mazingira na usababisha madhara makubwa sana hivyo serikali haitawafumbia
macho.
Pia amewaomba wananchi wawafichue wale wote wenye tabia hizo sababu
wanawafahamu hivyo wasiwaogope kuwafichua ili kukomesha majanga haya ya moto
No comments:
Post a Comment