Tuesday, 19 February 2013

KAMPUNI YA GAME FRONTIERS OF TANZANIA WAMEFANIKIWA KUKAMATA NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA MILION MIAMBILI - NAMTUMBO.


Gari la Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA likirejea katika Ofisi ya Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la SELOU likitokea ndani ya Pori 
Pembe za ndovu, Risasi na Silaha zilizokamatwa
Mwandishi wa Habari wa Tbc Bw. Gerson Msigwa akiangalia moja ya nyara zilizokamatwa
Mwandishi wa habari wa demashonews akiwa ameshika risasi zilizokamatwa

Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA kwa kushirikiana askari wanyamapori wa Selou na Askari wa vijiji vinavyozunguka pori la Akiba la Selou wamefanikiwa kukamata meno ya tembo 15 yenye thamani ya milion miambili, Risasi 9, Bunduki moja aina ya RIFFLE 458 na Gobole moja ambavyo hutumika kuulia wanyama .

Doria hiyo imechukua takribani siku tatu katika pori la Akiba la Selou ikiwa ni sehemu ya kuwatafuta majangili wanaofanya mauaji ya wanyamapori katika pori hilo,
Akizungumza na mwandishi wetu Bw. Mohamed Mpapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni hiyo ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA, Amesema kuwa hiyo ni kujituma kutokana na motisha ya fedha anayoitoa mwezeshaji wa kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA ndio chachu ya mafanikio ya kukamata meno,bunduki na risasi.

 Akiendelea kuzungumzia tukio hilo Bw. Mohamed Mpapa amesmea baada ya majangili kuwaona Game Frontiers Tanzania wakiwa katika doria ndani ya pori hilo huku wakiwa wamekamilika kimapigano majangili hao waliweza kukimbia na kuacha nyara hizo baada ya kuona nguvu yao ni ndogo katika kupambana na kundi la doria.

Ameongezea kwa kusema Kampuni yake imefurahishwa na mafanikio na ushirikiano uliopo kati yao, Serikali na wanavijiji kukabiliana na ujangili unaoendelea kuwamaliza tembo katika Pori la Akiba la Selou pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kuwafichua majangili.

Nae Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la Selou Bw. Bernald Lijaji amesema Pembe zilizokamatwa ni 15 pamoja na Bunduki aina ya RIFLE 458,Gobole moja na Risasi 9 aina ya 458 vimekamatwa katika Doria iliyofadhiriwa na Mwekezaji wa Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA

Monday, 18 February 2013

WATANZANIA WAWIKA NDANI YA MAONYESHO YA MAVAZI YA KIMATAIFA LONDON


  

 Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe akiwa na mwanamuziki Freddy Macha aliyetumbuiza shughuli hii na gitaa lake. Picha na Fred Mchaki

Changamkieni punguo la gharama za umeme – Mama Kikwete



IMG_8060
  
Na Anna Nkinda – Maelezo , Lindi
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa (NEC) Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa kijiji cha Kitumbikwela  na Mingoyo wilayani Lindi mjini kuchangamkia punguzo la kuingiza umeme katika nyumba zao na kuepukana na gharama za mafuta ya taa ambazo zinapanda mara kwa mara.


Mama  Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais aliyasema hayo jana wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wananchi hao katika ziara yake ya kichama ya  kuwashukuru wanachama wa CCM kwa kumchagua kuwa mjumbe wa NEC kutoka wilaya ya Lindi mjini.

Alisema kuwa miaka ya nyuma gharama za kuweka umeme majumbani zilikuwa kubwa na kufikia  shilingi milioni mbili na nusu lakini hivi sasa zimeshuka hadi shilingi laki nne na arobaini elfu fedha ambazo hata mwananchi wa kawaida anaweza akajiwekea  akiba na kuzipata.
Mama Kikwete alisema, “Kuweka umeme katika  nyumba yako si utajiri kwani gharama za uwekaji zimepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma  jambo la muhimu ni nyumba iwe imeezekwa vizuri na kuwekwa nyaya za kuingiza umeme ndani ya nyumba (wire ring).

Hata kama hauna hela unaweza kuweka akiba yako kidogokidogo kila mwaka pale unapouza  mazao na baada ya miaka michache utakuwa umepata fedha yote, nawasihi wananchi wenzangu hakikisheni kuwa umeme utakapofika kijijini mnautumia kwani wenzenu wanatamani kuwa na umeme lakini bado haujawafikia”.

Aidha Mama Kikwete pia aliwashimiza wanawake wajitokeze kwa wingi katika miradi ya kukopa mbuzi lipa mbuzi na kopa ng’ombe lipa ng’ombe kwani wakipata fedha kidogo pamoja na za waume zao pato la familia litaongezeka  na hivyo kujikwamua kimaendeleo.

Akiwa katika kijiji cha Mingoyo aliwasihi  wazazi kuwalea vijana wao katika maadili mema na kuwaelekeza pale ambapo wanapokosea kwani utandawazi unawaharibu vijana wengi na kujikuta wanajiingiza  katika matendo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya na uvutaji wa bangi.
“Baadhi ya vijana wanaona fahari kuwa na wapenzi wengi jambo ambalo ni la hatari kwa kuwa unajiandalia mazingira ya kupata kirahisi maambukizi ya virusi vya Ukimwi na takwimu zinaonyesha kuwa kwa kila watanzania mia moja sita wanamaambukizi. Muache tabia hiyo  na kufuata vitabu vitakatifu vya dini vinavyosema kwani ugonjwa huu hauna dawa zaidi ya dawa za kupunguza makali tu”, alisema Mjumbe huyo wa NEC .

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mingoyo Jamridi Mandowa alisema kuwa tangu Serikali ilipotangaza kuanza kwa mradi wa kusambaza umeme vijijini, kupunguza gharama za ufungaji wa umeme majumbani na kusogeza muda wa kupokea maombi wananchi wamejitokeza kwa wingi kutuma maombi lakini kasi ya usambazaji ni ndogo hawaelewi tatizo ni kitu gani.
Naye Diwani wa Kata ya Msinjahili ambaye ni Meya wa Lindi Mjini Frank Magali alisema kuwa kata yake inamradi wa kopa ng’ombe lipa ng’ombe na kopa mbuzi lipa mbuzi ambapo kwa upande wa ng’ombe walipata majike nane na dume mmoja na kuwakopesha wananchi ambao kwa kiasi kikubwa wamenufaika na mradi huo.

Mama Kikwete alifanya mikutano ya hadhara na kujibu maswali ya  wananchi  wa kata za Msinjahili, Mingoyo na Mitandi na kuwakabidhi kadi  wanachama  wapya wa CCM  37, Umoja wa vijana 37, Umoja wa Wanawake  92 na Jumuia ya Wazazi  73.

Mwadhama Kardinal Pengo azunguzia kifo cha Padri Zanzibar, wauaji waacha ujumbe baada ya mauaji.



Moja ya vipeperushi vilivyokamatwa mjini Zanzibar alipopigwa risasi Padri wa Kanisa Mpendae alichokionyesha Mwadhama kardinali Polycap Pengo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
Pengo asikitishwa na tukio la kuuwa kwa Padri Mushi lililotokea Mjini Zanzibar na kuwaasa wakristu kutolipiza kisasi maana kufanya hivyo yanaweza kutokea machafuko makubwa zaidi, la msingi alilosisitiza ni kwamba wale wanaopaswa kulinda usalama waangalie sana tunakoelekea siyo kuzuri ukilinganisha na matukio yanayoendelea
 
Pengo aliyekuwa anazungumza huku akiwa mwenye hudhuni hakuzungumza kwa muda mwingi sana na baada ya hapo alisema nawashukuru sana waandishi hayo ndiyo niliyokuwa nayo na kuongeza kuwa leo sitajibu maswali yoyote asante sana na kuondoka ukumbini

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 HAYA HAPA



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa na QT.

Jumla ya watahiniwa waliofaulu kwa Mujibu wa Matokeo hayo ni  23520 kuanzia dara la I hadi la II  huku katika mchakato huo wasichana waliofaulu katika mchakato huo ni 7178 na wavulana ni 16342.Aidha Waziri Kawambwa amesema kuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza ni 1641, daraja la pili ni 6495 na daraja la tatu ni 15426 na walio feli ni 24903.

Shule bora ni pamoja na St. Francis Girl ya Mbreya, Marian Boys ya Bagamoyo, Fedha Boys DSM, Marian Girls Bagamoyo, na Simini ndizo zipo tano bora huku shule nyingine ni Kanosa, Jude, St. Mary.

KUPATA MATOKEO HAYO BOFYA HAPO CHINI
MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012 

Sunday, 17 February 2013

BARAZA LA MADIWANI MBINGA MKOANI RUVUMA LAGAWANYA WATUMISHI NA MALI KWA WILAYA MBILI

 Baadhi ya madiwani wa wilaya ya mbinga wakiwa katika kikao cha kugawana watumishi na mali za wilya ya mbinga kuwa za 
wilaya mbili wilaya ya Nyasa na Wilaya ya Mbinga

Madiwani hawa ndio watakao gawanyika na kumikia wilya hizo mbili.

NYUMBA YA GHOROFA MOJA KIJIJI CHA LIPUMBA WILAYANI MBINGA MKOA WA RUVUMA


Nyumba hii ya ghorofa moja imejengwa katika kijiji cha lipumba katika wilaya ya Mbinga Mkoani  Ruvuma ambayo Rais wa kwanza wa Tanzania alimsaidia bati za kupaua mwenye nyumba baada ya kuwa imeezekwa  kwa nyasi . inasadikiwa .

TUPE MAONI YAKO