MWANDISHI
wa Habari wa kituo cha Radio Kwizera wilayani Kakonko mkoani Kigoma,
Issa Ngumba (45) ameua kwa kunyongwa na kisha kupigwa risasi mkono wa
kushoto huku simu zake mbili na Bastora iliyotumika kumshambulia ikiacha
kando ya mwili wake porini.
Habari
ambazo zimepatikana na kutoka wilayani Kakonko mkoani Kigoma na
kuthibitishwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Frasser Kashai, pamoja
na Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Kigoma (KPC) Deo Sonkolo
imedai mwandishi huyo amekutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na watu
ambao hawajajulikana.
Akizungumza
na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Sonkolo alisema kwamba mara baada
ya kupata taarifa waliwasiliana na waandishi wa wilaya ya Kibondo ambao
waliwahi kufika eneo la tukio na kushuhudia uchunguzi wa Daktari Primus
Ijumaa aliyeeleza kuwa mwili wa marehemu umenyonga ikiwa ni pamoja na
kupigwa risasi mkono wa kushoto.
Mwili
wake umepatikana jana katika pori la Mlima Kajuluheta kijiji cha
Muhange, wilayani humo majira ya asubuhi baada ya wananchi kufanya msako
wa siku tatu tokea Jumapili siku moja baada ya kutoonekana kwake.
“Sisi
tunaelekea wilaya ya Kakonko toka Kigoma mjini, lakini walioshuhudia
mwili huo huko eneo la tukio waneleza kwamba kando ya mwili wake
kumekutwa Bastora moja, haijafahamika iwapo ilikuwa inamilikiwa na
marehemu ama nani, simu zake mbili na kwa mujibu wa Dkatari maiti
inaonekana kunyongwa shingo na kupigwa risasi mkononi,” alieleza
Sonkolo.
Imeelezwa
kwamba bastora iliyokutwa eneo la tukio imekutwa na ikiwa na risasi
tano huku mifuko ya suruali ya marehemu ikiwa na noti moja ya Tsh10,000.
Kwa
upande wake kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Frasser Kashai
akithibitisha kuwapo kwa tukio hilo lakini alisema kwa sasa jeshi lake
linangoja taarifa ya daktari aliyefanya uchunguzi wa mwili wake ikiwa ni
pamoja na taarifa ya awali ya uchunguzi wa jeshi hilo toka eneo la
tukio.
Aidha
akizungumza na gazeti hili Naibu Mharari wa kituo cha Radio Kwizera
kinachorusha matangazo kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera, Seifu Upupu,
alisema kwamba tokea Januari 5 mwaka huu walikuwa majira ya saa 11
walikuwa wakijaribu kuwasiliana naye na simu zake zilikuwa zikiita bila
ya kupokelewa mpaka jana ambapo zilikuwa hazipatikani.
Chanzo: www.dj-sek.blogspot.com
No comments:
Post a Comment