Na,Steven Augustino
Tunduru
Wazazi na Walezi
wameaswa kushirikiana na Serikali kusimamia na kufuatilia kwa
karibu mienendo na maendeleo ya Watoto wao hasa wa kike zikiwa ni juhudi za
kuhakikisha kuwa watoto hao wanafanya vizuri katika masomo
yao na kujiletea maendeleo yao.
Wito huo umetolewa kwa niaba
ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw.Chande Nalicho na Mtendaji wa Kata ya Muhuwesi
Bw. Shaibu Ngoronje wakati akiongea katika mkutano wa Wadau wa elimu
uliofanyika katika Kijiji cha Mhuwesi ukiwa ni mwendelezo wa juhudi za
Mradi wa Usimamizi na Utetezi wa Haki ya Mtoto wa kike kupata elimu .
Akifafanua taarifa hiyo
Bw.Ngoronje alisema ili kufanikisha adhima hiyo serikali imejipanga kutoa elimu
kwa kuwaomba wazazi pia walezi kujitoa kuchangia chakula cha mchana kama
kivutio ili kuwaongezea nguvu ya kusoma watoto hao katika masomo yao.
Alisema Takwimu hizo zilifafanua kuwa katika kipindi cha Mwaka 2007-2010 jumla ya waliotarajiwa kuandikishwa shule ni watoto wa kike 17,386, walioandikishwa ni 14,692 ambao ni Sawa na asilimia 85.49% na waliosajiliwa ni 13,411, na waliofanya mitihani wa kumaliza darasa la saba walikuwa 13,097 ambao ni sawa na asilimia 97.65%, huku kukiwa na anguko la watoto 314 ambao waliacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba wakiwa shuleni pamoja na utoro.
No comments:
Post a Comment