WAKATI kukiwa na Sinto fahamu juu ya upatikanaji
wa Soko la Uhakika la
kuuzia Korosho Wakulima wa zao hilo wilaya
Tunduru mkoani
Ruvuma,wameiomba serikali itoe kibali cha
kuruhusu korosho zao kuuzwa
kwa wafanyabiashara binafsi ili kuwaepusha na
hasara wanayoendelea
kuipata wakati huu ambapo wanasubiri
malipo yao ya mwaka uliopita.
Kilio hicho kumepazwa katika nyakati tofauti na
wakulima hao na
kuungwa Mkono na Viongozi walioshiriki katika
Mkutano Mkuu wa Dhalula
wa Chama kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya
Tunduru (TAMCU) kilicho keti
katika ukumbi wa Chama hicho
Wakifafanua taarifa hiyo wakulima hao walisema
kuwa hali hiyo
inatokana na muda wa uvumilivu kupita na
hata kuvuka kikomo hivyo
wameamua kuchukua maauzi hayo ya kuitaka
serikali ichukue hatua haraka
ili wasiendelee kupata hasara kama ilivyotokea
katika msimu wa mwaka
2010/2011.
Walisema katika msimu huu zaidi ya tani 500 ya
zao ilo hazikununuliwa
hali mabayo iliwasababishia hasara na matatizo
mengi wakulima hao
ambao kwa sasa wakulima hao hawataki
kusikia tena neno la ushirika
kwani unawasababishia umasikini na kukubali
kuuza mazao yao ikiwemo la
korosho kwa walanguzi wanaonunua kwa bei ndogo
kuliko kusubiri bei ya
serikali ambayo haina uhakika.
Akizungumzia hali ya Mkanganyiko huo Meneja wa
Chama Kikuu cha
Ushirika cha wakulima wa Tunduru (TAMCU) Bw.
Imani kalembo alidai kuwa
hali hiyo inatokana na Chama hicho kukosa sifa
za Kukopesheka baada ya
kushindwa kurejesha Deni la zaidi ya shilingi
Bilioni.2.8 kati ya
fedha zilizokopwa msimu uliopita.
Alisemsa deni hilo lilishindwa kulipika kufutia
ubabaishaji wa
wanunuzi wakubwa ambao alitelemsha bei kwa kiasi
kikubwa na kukifanya
chama chao kuuza Korosho zao kwa Bei ya Tsh.850
kwa kilo moja kutoka
Tsh. 1200 walizonunulia kutoka kwa wakulima na
kusabishiwa hasara hiyo
No comments:
Post a Comment