Saturday, 5 January 2013

MUONEKANO WA MADARAJA MBALIMBALI NDANI YA MANISPAA YA SONGEA

Dararaja hii linatenganisha  matalawe na mabatini

 Daraja hili linatumiwa na watu wengi ambalo nikiunganishi kati ya wakazi wa matalawe na wakazi wa mabatini,

Daraja hili lipo matalawe barabara ya kwenda bombambili, swali langu nikwamba kwa mtu mwenye ulemavu je ataweza kuvuka? 
Hili nalo tutavuka wale wazima ila kwa walemavu na watoto hawawezi kuvuka
Hili linatenganisha matalawe na mji mwema ambalo lina unafuu lakini kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Ruvuma sijui kama litabaki salama.
Hayo ni majia ya mvua ambayo yanatililika na kusababisha mmomonyoko wa  ardhi pembeni ya daraja .
Hayo ni baadhi ya madaraja ambayo demashonews wamepata kuyatembelea na kupata picha za madaraja hayo ambayo yanatenganisha mitaa na kata, Uwenda yapo mengine yenye hali mbaya zaidi ya haya ambayo tumepata picha zake.

Je? Serikali imesahau kuwa kunamadaraja yanatakiwa kutengenezwa au taarifa kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa hawapeleki sehemu husika  au ndio tunangoja hadi yatokee madhala ndipo hatua zichukuliwe?

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO