Head of
Primary Medical Centre Bwa. Siwawi Konteh (wa pili kulia) ambaye pia ni
mratibu wa mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja ili kuokoa Afya ya Mama na
Mtoto akizungumzia Malengo Makuu ya mradi huo kuwa ni kuongeza kiwango
na matumizi ya Huduma ya Afya ya Mama Mjamzito na Watoto na kushirikiana
na kujifunza kuhusu Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto. Kutoka kushoto ni
Acting Medical Director wa Aga Khan Hospital Dr. Ambrose Chanji,
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib, Mkurugenzi
Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Dr. Sebastian Ndege na Kulia ni Mkuu
wa Kitengo cha Rasilimali Watu cha Hospitali hiyo Bw. Anis Nazrani.
Mkurugenzi
Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege
(wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi magari ya kubeba
wagonjwa kwa hospitali ya Aga Khan ambapo amesema vifo kadhaa
vinavyotokea katika hospitali nyingi kwa sasa vinawahusisha akinamama na
watoto wasio na hatia ambao hukosa huduma za awali za haraka zikiwemo
usafiri na hivyo katika kujali hilo wametoa magari hayo.
Aidha
amesema Ndege Medics inashukuru kuwa sehemu ya mradi endelevu wa
kujaribu kuokoa maisha ya akina mama na watoto ambao lengo lake ni
kuchangia katika kuboresha afya ya uzazi wa mama na watoto wachanga
katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mwanza, Mbeya na Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na
Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr.
Sebastian Ndege wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba
wagonjwa kwa Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha
Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania
No comments:
Post a Comment