Friday, 31 May 2013

Mrehemu Ernest Zulu azikwa Maposeni Songea


Na Nathan Mtega,Songea


MWILI wa marehemu aliyekuwa mwandishi wa vikao vya Bunge la Tanzania Ernest Zulu umezikwa katika makaburi ya kichifu yaliyopo Maposeni Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma huku mazishi hayo yakifanyika bila kuhudhuriwa na familia yake jambo ambalo liliwashangaza baadhi ya watu waliohudhuria mazishi hayo.

  Wakiongea kwa sauti za chini kwenye mazishi hayo baadhi ya wakazi wa Peramiho walisema kuwa wameshangazwa kuona wasifu wa marehemu ukisomwa na kuonyesha kuwa marehemu amewaacha watoto wanne na mke mmoja lakini cha ajabu hawaonekani kwenye msiba huo.

      Kwa upande wake kaka wa marehemu  chifu Emmanuel Zulu akiwashukuru mamia ya watu walioshiriki kwenye mazishi hayo akiwemo akiwemo  Mbunge aliyetumwa na bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kuja kuwakilisha mazishi hayo Abdukalim Shaha wa jimbo la Mafia Zanzibar alisema kuwa yeye hana  cha zaidi ya kumshukuru Mungu aliyetenda mambo hayo.

      Aidha kwa upande wake Mbunge Abdukalim Shaha akitoa salaamu za bunge amewataka viongozi wa dini zote kuendelea kujenga mshikamano wa kuliombea taifa lisiingie kwenye machafuko maana amani ikitoweka hakuna atakayekuwa huru kwa kufanya kazi zake.

        Alisema kuwa marehemu Ernest Zulu alitokea katika familia ya kichifu lakini kafanya mambo mazuri mengi katika taifa kwa sababu wazazi wake walikuwa wakihimiza amani na utulivu vidumu siku zote na siyo vinginevyo hivyo jamii inapaswa kuiga na kuendeleza moyo huo wa uzalendo.

        Alisema kuwa hali ya sasa  inayojitokeza katika vikao vya bunge kwa baadhi ya viongozi kutaka kushikana mwilini hivyo ni vyema jamiin kwa ujumla ikasaidiana kumuomba Mungu aweze kuepusha balaa hasa kwa kuwakemea vijana waachane na ushabiki usiyokuwa wa msingi.

      Hata hivyo aliipongeza ofisi ya mkuu wa wilaya ya Songea kwa kazi nzuri ya kufanikisha maandalizi ya mazishi hayo kwa kuwapokea wageni na kufanikisha kuwapa huduma na kuwa hiyo wanaenda kuiweka kwenye rekodi ya ofisi ya Mbunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

    Lakini pamoja na wakazi hao kuhudhuria kwenye mazishi hayo wakiwemo viongozi wa safari ya mwisho ya Ernest Zulu lakini wananchi hao walionyeshwa kutoridhika kwa kutokuwepo Mbunge hata mmoja wa mkoani hapo zaidi ya wawakilishi.

Thursday, 30 May 2013

Kampuni ya usambazaji mbegu ya PANNAR SEED kanada ya kusini yatoa jezi 28 na mipira 5 kwa Timu za vijijini Songea


Meneja wa kanda ya kusini Torio Mafie toka kushoto kwako akiwa ameshikilia mpira pamoja na jezi wakati akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Songea jana ofini kwake.
............................................
Hii ni baaada ya kukamilika kwa msimu wa mavuno kwa wakulima wa wilaya ya SONGEA mkoani RUVUMA sasa kampuni ya usambazaji mbegu ya PANNAR SEED kanda ya nyanda za juu kusini imetoa vifaa vya michezo wa soka kwa wakulima ili kufufua michezo wakati wakiwa waanajiandaa kwa msimu mwingine wa kilimo.

Kampuni ya PANNAR SEED imetoa jezi 28 na mipira mitano vyenye thamani ya shilingi milioni 2 na laki moja ambapo MENEJA WA KANDA YA KUSINI TORIO MAFIE amesema msaada huo waliotoa ni ishara kuwa wapo pamoja na wakulima ili kuwapa vijana shughuli mbadala wakati wa mapumziko ya msimu wa kilimo
Mkuu wa wilaya ya SONGEA JOSEPH MKIRIKITI Akipokea  jezi na mipira kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya
PANNAR SEED
Mkuu wa wilaya ya SONGEA JOSEPH MKIRIKITI akitabasamu kwa furaha baada ya wakulima kuwezeshwa vifaa vya michezo ,
 Hataa hivyo kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya SONGEA amesema bado mahitaji ya vifaa vya michezo ni makubwa hivyo ameziomba kampuni mbalimbali zinazojihusisha na shughuli za kiuchumi na kijamii wajitokeze kufadhiri timu za vijiji wilayani hapa

 

Kinana: Akemea wanaowania urais 2015

kinana 3361e
Kinana (katikati)
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesisitiza kwamba Chama kitamwadhibu bila huruma mwanachama yeyote anayejipitisha-pitisha katika maeneo mbalimbali na kufanya kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.

Kinana alisema hayo jana wakati akizungumza na Kamati ya Siasa na mkoa wa Iringa, katika kikao maalum, kilichofanyika kabla  ya kwenda mkoani Njombe ambako ameanza ziara ya siku saba mkoani humo.


Kinana alisema, katazo la wanachama kujipitisha-pitisha na kupiga kampeni za kuwania urais au nafasi yoyote kabla ya muda  halitoki midomoni mwa viongozi bali ni kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.


"Ndugu zanguni, nawakumbusha kwamba kwa hili hatuna mzaha nalo, hivyo hakikisheni kila mmoja wenu kama kiongozi hajihusishi kwa namna yoyote kushiriki katika kutumiwa na wanachama hao wanaojipitishajiptisha", alisema Kinana na kuongeza;

"Ni lazima Chama kiwe kikali kwenye jambo hili, kwa sababu kama kitawaacha watu hawa kukiuka taratibu na kanunzi za Chama wanazidi kukifanya chama kuwa na makundi mengi ambayo yatakipeleka pabaya," alisema Kinana


Kinana alisema,  kazi walioyonayo wale wote wanaokitakia mema Chama, ni kumuunga mkono Mwenyekiti, Rais Jakaya katika kazi ya kuhakikisha CCM inakamilisha utekelezaji ilani yake ya Uchaguzi kwa kiwango kinachostahili na siyo muda kujipitisha pitisha mtu binaafsi kwa wanachama huku utekelezaji wa ilani ukisinzia.


Alisema kuwa hivi sasa kazi ya CCM ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha miaka miwili ya nusu kabla ya kumalizi kwa awamu ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.

"Ni wazi kazi yatu CCM ni kuhakikisha tunatekeleza ilani ya uchaguzi kwa vitendo na si mamneno kama wanavyofanya wengine. ni kazi kubwa imefanyika chini ya uongozi wa Rais Kikwete na katika kipindi cha miaka miwili iliyobaki tumedhamiria kuifanya zaidi", 


Alisema moja ya maeneo ambayo licha ya kuwepo changamoto za hapa na pele lakini yamefanikisha sana utekelezaji wa ilani ya CCM,  ni kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ambapo watendaji walio wengi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi.


"Kwa kweli CCM lazima hawa tuwapongeze maana kuna wengine kazi yao imebaki kuwashambulia huku wakijua watendaji hao hawana fursa ya kujitete mbele ya jamii. chapeni kazi nasi tupo nyuma yenu, na kila wakati tutakuwa tukitambua juhudi na kazi kubwa mnayoifanya kwa jamii," alisema Kinana.

BAADHI YA WADAU WALIOHUDHULIA KATIKA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZIWA INAYOFANYIKA KITAIFA MKOANI RUVUMA

 Baadhi ya Wanafunzi walio hudhulia viwanjani hapo
 Waandishi wa habari hawakuwa nyuma pia

SIKU YA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA KUMI NA SABA(17) YA WIKI YA MAZIWA SONGEA-RUVUMA YAFANA



Mkuu wa mkoa wa RUVUMA SAID MWAMBUNGU amezindua maadhimisho ya 17 ya wiki ya maziwa nchini na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuwa na utamaduni wa kunywa maziwa kwa wingi kwa lengo la kuboresha afya zao

Akizungumza na wananchi na wadau wa maziwa katika viwanja vya manispaa ya SONGEA MWAMBUNGU alisema  kati ya lita bilioni 1.6 za maziwa zinazozalishwa hapa nchi kwa mwaka ni wastani wa lita 11.6 tu zinazonywewa na mtu mmoja wa mkoa wa Ruvuma kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na viwango vya kimataifa vya lita 200 kwa mtu kwa mwaka.
Maadimisho hayo ya wiki ya maziwa ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mkoaniMkoani Ruvuma ambapo MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU aliwaamasisha wananchi wa mkoa wake kuongeza kasi ya unywaji wa maziwa sambamba na kufuga ng’ombe wa kisasa wanaotoa maziwa mengi badala ya ng’ombe wa asili ambao uzalishaji wao ni mdogo.

Maadhimisho haya yameambatana na maonyesho ya bidhaa mbalimbali za maziwa pamoja utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa unywaji maziwa, usindikaji na uzalishaji wake hata hivyo baadhi ya wadau wa maziwa kutoka vyama vya usindikaji maziwa wamesema maziwa mengi yanayozalishwa hapa nchini yanashindwa kuwafikia wanywaji kutokana na asilimia chache zinazosindikwa.
Wiki ya maziwa iliyozinduliwa leo mkoani hapa itaendelea kwa siku nne zijazo ambapo hapo kesho madereva wa pikipiki maarufu kama YEBOYEBO, wafungwa na wagonjwa hospitalini watagawiwa maziwa ya bure kama sehemu ya uhamasishaji


Monday, 27 May 2013

BREAKING NEWS: WATU NANE WAFALIKI DUNIA NA WENGINE KUMI NA MOJA MAJELUHI KATIKA AJALI YA GARI - NAMTUMBO

 

Hili ndilo lori lililopata ajali katika kijiji cha Hanga
..............................................
Watu nane wamefariki dunia  baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka kijiji cha mputa wilaya ya Namtumbo kwenda Songea  kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Hanga eneo la Bombambili wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma .
Roli hilo lilikuwa limebeba magunia ya ufuta, mpunga wakiwemo na abiria

 Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma  Deusdedit  Nsimeki amesema ajali hiyo imetokea jana Tarehe 26.05.2013 majira ya saa nne na nusu( 4:30 usiku  katika kijiji cha Hanga eneo la bombambili mkoa wa Ruvuma, chanzo cha ajili hiyo ni mwendokasi na dereva kuendesha gari akiwa amelewa,

Ajali hiyo  imehusisha gari lenye namba za usajili T.677 ADL  aina ya Isuzu lori , mali ya mfanyabiashara wa mazao maarufu kwa jina la Mtazamo. likiendeshwa na dereva aitwae CHRISTIN NYONI mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa LIHULI SONGEA,
Baada ya ajali hiyo kutokea dereva wa gari hilo amekimbia na kutelekeza gari porini hadi sasa jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya jitihada za kumtafuta ili sheria ifuate mkondo wake.

Kamanda wa Polisi amesema gari  hilo liliacha njia baada ya kugonga daraja na kupinduka na kusababisha vifo vya watu nane(8)  na majeruhi kumi na moja (11) ambao
wote wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu.

Kutokana  na ajali hiyo mbaya kamanda wa polisi wa  Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki ametoa wito kwa wamiliki wa magari ya mizigo kutopakia mazao pamoja na abiria na atakayekiuka atachukiliwa hatua kali za kisheria.
Pia ametoa wito kwa wamiliki/wasimamizi wa magari kuwa wanatakiwa kuhakikisha magari ya mizigo,mazao hayapakii abiria na atakaye kiuka agizo hili hatafikishwa mahakamani mala moja 
ambapo


Saturday, 25 May 2013

WATOTO WATANO WALIOZALIWA JANA WAFARIKI NA KUZIKWA BILA MAMA YAO KUSHUHUDIA


 
 Mwalimu Sofia Mgaya akiwa amelala na watoto wake wote watano  kitandani  mara baada ya kujifungua jana.

Na Juma Nyumayo, Songea
WATOTO watano waliozaliwa hai jana wamefariki baada ya kuishi takribani saa 10 tu toka wazaliwe na kuzikwa bila kushuhudiwa na mama yao..
Watoto hao wamekwisha zikwa katika makaburi ya Lilambo nje kidogo ya Manispaa ya Songea njia ya kuelekea Peramiho kwa Shangazi yake mama yao wakati mama yao akiendelea kupata matibabu Hospitali ya mkoa, Songea.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Luwawazi, Mwl. Msigwa, ameuambia mtandao huu mara baada ya kutoka mazikoni kuwa watoto hao wote watano wamefariki jana saa tatu usiku.
Vifo hivyo, vimethibitishwa na Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma hapa Songea,  Dkt Benedict Ngaiza kuwa wote walifariki jana.
Akizungumzia mazishi hayo, Mwl. Msigwa amesema  kila mtoto amezikwa katika kaburi lake.
"Tumewazika kila mmoja na kaburi lake, nilishaamua nikawazike nyumbani kwangu Msamala, lakini kwa bahati alijitokeza Shangazi yake mwalimu anayeishi huko Lilambo ambako tumefanya maziko hayo," alisema Mwl. Msigwa.
 Alifafanua kuwa licha ya kupewa miili ya marehemu hao mapema walichelewa kuzika kwa  kuwasubiri wazazi wa mwalimu Sofia, wakitokea huko Ludewa mkoani Njombe kushiriki Mazishi hayo," alisema Mwl Msigwa ambaye ameendelea kupata simu za pongezi za kupata watoto watano kwa mpigo kwa mwalimu wa shule yake.
Wakati maziko hayo yanaendelea tayari mipango katika taasisi na Ofisi ya Manispaa ya Songea ilikuwa ikifanywa namna ya kumsaidia mwalimu huyo namna ya kuwale watoto hao wakiongozwa na Meya wa Manispaa Mhe. Charles Muhagama.
Watoto hao watano walipatikana jana kwa wakati mmoja baada ya kufanyiwa upasuaji wa uzazi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea.
 Awali akizungumza na waandishi wa habari,  Mganga Mkuu mfawidhi wa hospitali hiyo,  Dkt. Ngaiza alimtaja mwanamke huyo aliyejifungua watoto hao watano kuwa ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari, Sophia Mgaya (28) ambaye ni mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea na kuwa hali za watoto hao ziliendelea vizuri pamoja na kuzaliwa chini ya umri wa kawaida wa kuzaliwa ambao ni miezi tisa.
 Alisema kuwa mama huyo alipokuwa akihudhuria kliniki hospitalini hapo uchunguzi uliokuwa ukionyesha kuwa tumboni mwake kuna watoto wanne ambao walikuwa wakiendelea vizuri tumboni humo lakini mnamo Mei 24 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi alianza kusikia uchungu na kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa upasuaji na kukutwa akiwa na watoto watano hai tumboni mwake.
 Dkt. Ngaiza alisema kuwa watoto watatu ni wa kiume na wawili ni wa kike na wote wako hai na wamewekwa katika chumba maalumu kwa sababu wamezaliwa wakiwa na umri wa wiki thelathini na nne(miezi nane) na siyo miezi tisa kama ilivyo kawaida.
 Aidha alisema kuwa watoto hao wamezaliwa wakiwa na uzito mdogo huku mwenye uzito mkubwa akiwa gramu 730 na mwenye uzito mdogo akiwa na gramu 430 na huo ukiwa ni uzazi wake wa pili huku mama mzazi wa mwanamke huyo aliwahi kujifungua watoto watatu na wote wako hai na mmoja ni mtoto wa kiume anasomo kidato cha sita katika shule ya wavulana ya Songea.
 Alisema kuwa tukio hilo ni la kihistoria kutokea katika hospitali hiyo kwa sababu kumekuwepo na matukio ya akina mama kujifungua watoto wawili au watatu na siyo zaidi ya idadi hiyo kama ilivyotokea kwa mama huyo.
Watoto hao walikuwa na uzito mdogo kuanzia kuanzia wa kwanza aliyekuwa na uzito wa gramu 730, wa pili gramu 810, wa tatu gramu 670, wa nne gramu 820, na watano alikuwa na uzito wa gramu 43o. 




 

Friday, 24 May 2013

Rais dkt Shein amtembelea Sheha Aliyetiwa Tindi kali

000000

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuangalia Sheha wa Shehia  ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja,Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) jinsi alivyoathirika na  Tindikali alilomwagiwa na Mtu asiyejuilikanwa  huko Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake,Sheha huyo yupo katika Hospitali ya Mnazi mmoja kwa matibabu,wa  kushoto Dk.Slim Mohamed Mgeni,[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.] MG 0000
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Sheha wa Shehia  ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja,Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) aliyetiwa Tindikali na Mtu asiyejuilikanwa  huko Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake,Sheha huyo yupo katika Hospitali ya Mnazi mmoja kwa matibabu,wa pili kulia Kaka yake Sheha Sudu Mgeni Saidi.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

ZAO LA TUMBAKU LAWANUFAISHA WANAFUNZI VIJIJINI

 Baadhi ya maofisa wa kampuni ya uzalishaji zao la tumbaku mkoani Ruvuma wakikabidhi madawati katika shule ya msingi  Mkongo Nakawale katika wilaya ya Namtumbo ikiwa ni huduma wanazotoa katika vijiji vinavyozalisha Zao hilo.



TEMBO WAENDELEA KUTEKETEA RUVUMA MMOJA AKAMATWA

Friday, May 24, 2013

Kwa kweli kila ndugu zangu ninapotazama picha hii natamani kuwepo mjadala wa kitaifa juu ya hatma ya rasilimali hii ya wanyamapori hususani Tembo, maana kuna kila dalili kuwa kama hali itaendelea hivi sio muda mrefu Tembo watapukutika kama walivyopukutika Faru.
Hizi ni pembe za ndovu zilizokamatwa huko nchini China baada ya kubambwa na vyombo vya usalama vya China.
Tembo wakiwa na furaha lakini hizo pembe walizonazo ndizo zinazowaponza.

CHADEMA WARUHUSIWA KUFANYA MKUTANO SONGEA.

Habari tulizozipata hivi punde zinasema Baada ya Mkutano wa pamoja kati ya viongozi wa vyama vya siasa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, hatimaye Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA kimeruhusiwa kufanya Mkutano wake wa kampeni ya M4C uliopangwa kufanyika tarehe 26 Mei 2013. Mkutano huo utafanyika Mjini Songea katika eneo la Matarawe Mjini Songea.

Hata hivyo katika makubaliano hayo, CHADEMA imekataliwa kufanya maandamano kama ilivyopangwa awali ambapo ilitangazwa kuwa Mkutano wa hadhara ungetanguliwa na maandamano ambayo yangeanzia katika Chuo Kikuu Huria hadi Matarawe.

Kufutwa na baadaye kuruhusiwa kwa Mkutano wa CHADEMA kumeleta mkanganyiko kwa wananchi wa Manispaa ya Songea kutokana na kubadilika kwa maamuzi ya Dola katika kipindi kifupi.

Habari pia zinaeleza kuwa Baada ya Mkutano wa CHADEMA hapo Mei 26, Chama Cha Mapinduzi CCM pia kitafanya mkutano wake hapa Songea Juni 02, 2013 ambapo Katibu Mkuu wa CCM Abdulahaman Kinana anatarajiwa kufanya Mkutano huo ikiwa ni sehemu ya ziara ya viongozi waandamizi wa Chama hicho nchi nzima. Mikutano hiyo ina lengo la kukagua uhai wa Chama pamoja na kutembelea na kuzungumza na mabalozi wa nyumba kumi, viongozi wa mashina ambayo ni uti wa mgongo wa Chama, matawi, kata, wilaya na mkoa.




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki

Wednesday, 22 May 2013

NILIYEKUTANA NAYE

                                                    ESTER HAULE( MRS MTEGA)

Cathy habari imekutana na mwanadada makini sana katika anga za ujasiliamali ambaye anafaa kuigwa na wanawake wengine. Ester ni mfanyakazi katika sekta ya afya kitengo cha utoaji dawa. ni mke wa mwandishi wa habari Nathani Mtega. Pamoja na kuwa mfanyakazi katika duka la dawa muhimu lakini yeye binafsi anajishugulisha na biashara ya uuzaji wa dawa katika duka lake mwenyewe lililopo katika eneo la msamala.Mpaka sasa amefanikiwa kujenga nyumba nzuri katika eneo la msamala anakoishi na malengo yake ni mengi ikiwemo kuendelea na kazi yake pamoja na kuendeleza duka la mume wake lililopo katika kata ya mjimwema songea ambalo nalo analisimamia na kuhakikisha linasonga mbele. Sifa nyingine ya Ester ni mcheshi, mkarimu na anapenda sana kupika.Ester ni mkazi wa Songea mkoani Ruvuma, Mungu akujalie ufanikiwe malengo yako.

Monday, 20 May 2013

MWENYEKITI WA CCM, RAIS KIKWETE AFANYA KIKAO MUHIMU NA WABUNGE WA CCM LEO MJINI DODOMA

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini wakati wa kikao chake na wabunge wa CCM, leo Mei 19, 2013, katika ukumbi wa jengo la White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine kushoto ni Spika wa Bunge Anna Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kikao chake na wabunge wa CCM, leo Mei 19, 2013, katika ukumbi wa jengo la White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine kushoto ni Spika wa Bunge Anna Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula.
  Wabunge wa CCM wakiwa kwenye kikao chao na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete leo kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Wajumbe kwenye kikao hicho wakibadilishana mawazo ukumbini. Walioketi mbele, Kushoto ni Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakiah Meghji na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migoiro na Mbunge wa Urambo na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai na Katibu wa NEC Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib kwenye kikao hicho.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro(kulia) akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Mbunge wa Same Anne Kilango Malecela.
 Mbunge wa Songea na Waziri wa Mambo ya Ndani,Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akitaniana kuhusu Uyanga na Simba na Mwenyekiti wa Simba, Mbunge wa Tabora Aden Rage nje ya ukumbi kabla ya kuanza mkutano huo. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya.
Mbunge wa Bunga Steven Wasira (kulia) akibadulishana mawazo na wabunge wenzake, Dk. Kamani na Mkullo kabla ya kikao kuanza
Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan (kushoto) akibadilishana mawazo na wabunge wenzake Khamis Kagasheki na Shabiby nje ya ukumbi
Wabunge wakifurahia jambo nje ya ukumbi wakati wa mkutano huo, Kutoka kushoto ni Dk. Mary Mwanjelwa,  Ritha Kabati, Angela Kairuki, Beatrice Shelukindo na Vicky Kamata
Shabiby akizungumza na Angela Kairuki
Vicky Kamata na Ana Kilango Malecela ukumbini
Dk. Asha-Rose Migiro akimsalimia Mama Anna Kilango Malecela
Dk Maua Daftari na Samiah Suluhu ukumbini
Job Ndugai akimpongeza Mbunge wa Igunga Dk. Dalaly Peter Kafumu kurejeshewa Ubunge
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akimsalimia Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa wakati wa kikao hicho cha Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete na wabunge wa CCM
Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe akimsikiliza kwa makini Mbunge mwenzake Innocent Kalogeris  wakati wa mkutano huo. Picha zote na BASHIR NKOROMO

TUPE MAONI YAKO