Wednesday, 15 May 2013

SISTER WA BANDIA AKAMATWA

 
 Mwanamke - anayejiita Sister Phylis Wanjiru Kamau, raia wa Kitui nchini Kenya akiwa ofisi za kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, baada ya kukamatwa.
Taarifa za kipolisi, za kukamatwa kwa Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.

JESHI la polisi mkoa wa Iringa limemkamata mwanamke Phylis Wanjiru mwenye umri wa miaka 44 aliyevalia mavazi ya kitawa wa masister wa kanisa Kathoriki, ambapo baada ya kupekuliwa amekutwa na baadhi ya vielelezo vilivyobaini kuwa ni tapeli.

Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya Kenya amekamatwa na jeshi la polisi baada ya masister wenzie kubaini kama si mmoja wao, kutokana na kushindwa kufanya baadhi ya masuala  ambayo ni msingi wa utawa wao.

Akizungumzia mkasa huo, kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema mwanamke huyo kabila lale ni Muwembu wa Kituo nchini Kenya amekamatwa majira ya saa kumi jioni tarehe 13, katika nyumba hizo za masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.

Aidha Kamuhanda amesema mwanamke huyo ambaye awali aligoma kutoa maelezo ya kina juu ya ujio wake nchini Tanzania, katika upekuzi walimkuta na baadhi ya chip (Line) za makampuni mbalimbali ya simu ya ndani na nje ya nchi.

Kamuhanda amesema Sister huyo bandia alikutwa pia akiwa na hati za kusafiria (Passport) mbili, moja ikiwa niya Africa Mashariki yenye namba Ke. 020659 huku hati ya nyingine ikiwa na jumuiya ya Kenya namba A. 1790366.

Amesema Sister huyo feki katika hati hizo ilionyesha kuwa alitembelea nchi ya Rwanda, Uganda pamoja na nchini Tanzania ambapo siku za hivi karibuni alikuwa Mkoani Mara Tarime.

Kamuhanda ameitaka jamii kuwa makini na wageni mbalimbali, huku akiwaasa kuacha tabia ya kuwaamini watu kwa muonekano wao, kutokana na mwanamke huyo kutumia njia hiyo ambayo inamfanya kila mtu kumuamini.


No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO