BABA
Mtakatifu Francis, amekubali ombi la Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea,
Norbert Mtega (68),pichani, kustaafu katika utume wa kuongoza jimbo
hilo.Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde,
kutoka kwa Balozi wa Papa nchini, Askofu Mkuu Frascisco Padilla,
ilieleza kuwa, Papa amekubali ombi hilo.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, ombi la Askofu Mtega kwa Papa, lilitokana na
kuwa na matatizo ya kiafya, hivyo kushindwa kuwahudumia waumini
inavyopaswa. Hata hivyo, kikanisa ni siri ya mtu mwenye hadhi ya Askofu,
anapoomba kwa Papa kustaafu.
“Baba
Mtakatifu Francis amekubali ombi la Mhashamu Askofu Mkuu Norbert Mtega,
kustaafu kutoka majukumu ya utawala wa kichungaji wa Jimbo Kuu la
Songea, kwa sababu ya kiafya,” ilieleza taarifa hiyo.
Hata
hivyo haikufafanuliwa maradhi yanayomsumbua Askofu Mtega, ambaye pia
kiumri ni miongoni mwa maaskofu wakongwe katika kanisa hilo nchini.
Katika hatua
nyingine, Papa amemteua Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, wa Iringa, kuwa
msimamizi wa kitume wakati kiti cha Askofu wa Jimbo Kuu la
Songea, kikiwa wazi, kwa mamlaka ya kiti kitakatifu (Mamlaka ya
Vatican)
.
Kwa
kawaida, hakuna muda maalum wa uteuzi wa Askofu Mkuu mwingine kuongoza
jimbo, panapotokea askofu amestaafu utume, lakini huchukua hata miezi
sita hadi mwaka kufanyika uteuzi. Hivi sasa jimbo hilo linaongozwa moja
kwa moja kutoka Vatican kwa usimamizi wa Askofu Ngalalekumtwa.
Askofu
Mkuu Mtega alizaliwa katika kijiji cha Kinyika (Lupanga-Njombe), Agosti
17, 1945. Alipata daraja la Upadri Novemba 14, 1973, aliteuliwa kuwa
Askofu wa Jimbo la Iringa Oktoba 28, 1985.
Aliwekwa
wakfu na Papa John Paul II Januari 6, 1986, huko Roma II, na miezi
miwilli baadae, Machi 9, 1986 alisimikwa Iringa. Aliteuliwa kuwa Askofu
Mkuu wa Songea Julai 6, 1992 na kusimikwa huko Songea Septemba 20 mwaka
huo huo.
Mwisho.
Katika hatua
nyingine, Papa amemteua Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, wa Iringa, kuwa
msimamizi wa kitume wakati kiti cha Askofu wa Jimbo Kuu la
Songea, kikiwa wazi, kwa mamlaka ya kiti kitakatifu (Mamlaka ya
Vatican)
.
No comments:
Post a Comment