WATOTO WATANO WALIOZALIWA JANA WAFARIKI NA KUZIKWA BILA MAMA YAO KUSHUHUDIA
Mwalimu Sofia Mgaya akiwa amelala na watoto wake wote watano kitandani mara baada ya kujifungua jana.
Na Juma Nyumayo, Songea
WATOTO watano waliozaliwa hai jana wamefariki baada ya kuishi takribani saa 10 tu toka wazaliwe na kuzikwa bila kushuhudiwa na mama yao..
WATOTO watano waliozaliwa hai jana wamefariki baada ya kuishi takribani saa 10 tu toka wazaliwe na kuzikwa bila kushuhudiwa na mama yao..
Watoto
hao wamekwisha zikwa katika makaburi ya Lilambo nje kidogo ya Manispaa
ya Songea njia ya kuelekea Peramiho kwa Shangazi yake mama yao wakati
mama yao akiendelea kupata matibabu Hospitali ya mkoa, Songea.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Luwawazi, Mwl. Msigwa, ameuambia mtandao huu
mara baada ya kutoka mazikoni kuwa watoto hao wote watano wamefariki
jana saa tatu usiku.
Vifo
hivyo, vimethibitishwa na Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa
Ruvuma hapa Songea, Dkt Benedict Ngaiza kuwa wote walifariki jana.
Akizungumzia mazishi hayo, Mwl. Msigwa amesema kila mtoto amezikwa katika kaburi lake.
"Tumewazika
kila mmoja na kaburi lake, nilishaamua nikawazike nyumbani kwangu
Msamala, lakini kwa bahati alijitokeza Shangazi yake mwalimu anayeishi
huko Lilambo ambako tumefanya maziko hayo," alisema Mwl. Msigwa.
Alifafanua
kuwa licha ya kupewa miili ya marehemu hao mapema walichelewa kuzika
kwa kuwasubiri wazazi wa mwalimu Sofia, wakitokea huko Ludewa mkoani
Njombe kushiriki Mazishi hayo," alisema Mwl Msigwa ambaye ameendelea
kupata simu za pongezi za kupata watoto watano kwa mpigo kwa mwalimu wa
shule yake.
Wakati
maziko hayo yanaendelea tayari mipango katika taasisi na Ofisi ya
Manispaa ya Songea ilikuwa ikifanywa namna ya kumsaidia mwalimu huyo
namna ya kuwale watoto hao wakiongozwa na Meya wa Manispaa Mhe. Charles
Muhagama.
Watoto
hao watano walipatikana jana kwa wakati mmoja baada ya kufanyiwa
upasuaji wa uzazi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo
mjini Songea.
Awali
akizungumza na waandishi wa habari, Mganga Mkuu mfawidhi wa hospitali
hiyo, Dkt. Ngaiza alimtaja mwanamke huyo aliyejifungua watoto hao
watano kuwa ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari, Sophia Mgaya (28) ambaye
ni mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea na kuwa hali za watoto hao ziliendelea
vizuri pamoja na kuzaliwa chini ya umri wa kawaida wa kuzaliwa ambao ni
miezi tisa.
Alisema
kuwa mama huyo alipokuwa akihudhuria kliniki hospitalini hapo uchunguzi
uliokuwa ukionyesha kuwa tumboni mwake kuna watoto wanne ambao walikuwa
wakiendelea vizuri tumboni humo lakini mnamo Mei 24 mwaka huu majira ya
saa 4 asubuhi alianza kusikia uchungu na kufikishwa hospitalini hapo na
kufanyiwa upasuaji na kukutwa akiwa na watoto watano hai tumboni mwake.
Dkt.
Ngaiza alisema kuwa watoto watatu ni wa kiume na wawili ni wa kike na
wote wako hai na wamewekwa katika chumba maalumu kwa sababu wamezaliwa
wakiwa na umri wa wiki thelathini na nne(miezi nane) na siyo miezi tisa
kama ilivyo kawaida.
Aidha
alisema kuwa watoto hao wamezaliwa wakiwa na uzito mdogo huku mwenye
uzito mkubwa akiwa gramu 730 na mwenye uzito mdogo akiwa na gramu 430 na
huo ukiwa ni uzazi wake wa pili huku mama mzazi wa mwanamke huyo
aliwahi kujifungua watoto watatu na wote wako hai na mmoja ni mtoto wa
kiume anasomo kidato cha sita katika shule ya wavulana ya Songea.
Alisema
kuwa tukio hilo ni la kihistoria kutokea katika hospitali hiyo kwa
sababu kumekuwepo na matukio ya akina mama kujifungua watoto wawili au
watatu na siyo zaidi ya idadi hiyo kama ilivyotokea kwa mama huyo.
Watoto
hao walikuwa na uzito mdogo kuanzia kuanzia wa kwanza aliyekuwa na
uzito wa gramu 730, wa pili gramu 810, wa tatu gramu 670, wa nne gramu
820, na watano alikuwa na uzito wa gramu 43o.
No comments:
Post a Comment