Rais wa baraza la maaskofu Tanzania akiwa na wazee wa shirika la Mt. Agustino nje ya Kanisa la moyo Mt. Yesu Parokia ya Kihesa jimbo la Iringa mara baada ya Misa ya uzinduzi hii leo |
Baadhi ya wazee wa shirika la Mt. Agustino wakiwa nje ya Kanisa. |
Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akiongea na wazee nje ya Kanisa. |
==============================================
Na Gustav Chahe
RAIS wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amesema wazee wasisahaulike katika huduma muhimu ili waendelee kutoa mang’amuzi yao mbalimbali katika jamii.
RAIS wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amesema wazee wasisahaulike katika huduma muhimu ili waendelee kutoa mang’amuzi yao mbalimbali katika jamii.
Mhashamu
askofu ameyasema hayo katika maadhimisho ya Misa Takatifu iliyokuwa
maalum kwa uzinduzi wa shirika la wazee na wastaafu mbalimbali la
Mtakatifu Agustino iliyofanyika katika Kanisa la Kiaskofu la Moyo
Mtakatifu wa Yesu Parokia ya Kihesa jimbo la Iringa hii leo.
Amesema
wazee ni tunu ya familia na hivyo kuwatenga wazee hao ni kumkosea Mungu
kwa kuwa wao ndio mashahidi wa misingi ya Baraka.
Askofu
Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa jimbo la Iringa amesema ndio
wanaoendeleza mapokeo mbalimbali yaliyo katika misingi ya maadili na
kuongeza kuongeza mang’amuzi ya changamoto mbalimbali zinazoikabili
jamii ya watanzania.
Amesema
wazee wahudumiwe kwa upendo bila kubaguliwa na wapewe haki stahiki bila
kusumbuliwa kwa kuwa ni haki yao kupata mahitaji muhimu kama walivyo
wengine.
“Kanisa
linashuhudia uwepo wa Yesu Kristo na hawa wazee ndio mashahidi wa
misingi ya wokovu na Baraka za Mungu. Wahudumiwe bila kubaguliwa”
amesema.
Vile vile amesema katika familia wazee wanarithisha tunu za familia hasa katika maadili na mafundisho yenye hekima na busara.
Hata
hivyo ameitaka jamii kuwa na upendo kwa rika mbalimbali ambazo zipo
katika jamii kwa kuwa upendo ndicho kiini cha imani na amani.
“Upendo
unalea, unaleta nguvu, unafariji na ndicho chanzo cha amani na furaha
kwa binadamu anayehitaji kufarijiwa na kuhudumiwa sawasawa na mwingine”
amesema.
Amesema
tunu za nchi ambazo ni zawadi ya kutoka kwa Mungu ziwanufaishe wazee
ambao kwa namna moja au nyingine ndio washauri wa mambo mbalimbali na
pale wanapohitaji haki zao kusiwe na ubabaishaji.
Ubabaishaji wa makusudi katika utoaji huduma ni kinyume na haki za binadamu ambao ni haki yao kupata huduma.
Amewataka
viongozi mbalimbali walio na mafundisho ya kikristo kutumia mafundisho
ya upendo katika kuihudumia jamii bila kujali rika na hasa kuwapa
kipaumbele wazee ambao umri wao umekwenda.
Naye
Mwenyekiti wa shirika hilo William Myonga amesema lengo la kuanzisha
shirika hilo ni kuwaunganisha wazee kwa ajili ya kutathimini yale
yaliyowakumba wakati wa ujana.
Amesema
yapo mengi ambayo katika ujana yamekuwa kikwazo kwao kiasi cha
kusababisha kumtumikia Mungu ipasavyo na hivyo kupitia shirika lao
watapata nafasi ya kukumbushana na kumuomba Mungu.
Mhamasishaji
wa shirika hilo Licas Mwasimile amesema wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali hasa katika kupokelewa katika majimbo mbalimbali.
Mwasime
amesema changamoto mojawapo ni pale wanapohamasisha na kuambiwa kuwa
shirika halitambuliwi kitaifa licha ya kuwa elimu na maelezo juu ya
kulitangaza shirika hilo yanajitosheleza.
Ametoa
kilio cha wazee hao kwa baraza la baaskofu kuwasaidia kupokelewa kwa
urahisi katika majimbo yao ili kuwawzesha utume wao kuwa mwepesi.
Shirika
la Mtakatifu Agustino limeshafika katika majimbo 22 ambapo kwa kanda ya
nyanda za juu kusini limeshaingia katika majimbi ya Mbeya, Mbinga,
Songea na Iringa.
Mlezi wa shirika hilo Padre Gregory Mashtaka amewataka wazee wa shirika hilo kuwa na mshikamano pamoja na mawasiliano.
“Si kwamba mmekwisha kufika, huu ni mwanzo tu. Hali yetu ni ya uzee. Hivyo, tuipokee kwa furaha” amesema Pd. Mashtaka.
Amewataka wazee hao kuwa washiriki walio hai na si hoi kwa kuishi kwa ushirikiano na kuwa na maisha ya utakaso.
Katika uzinduzi huo, jumla ya wazee 89 walipokelewa katika shirika hilo la Mtakatifu Agustino.source mzee wa matukio Iringa.
No comments:
Post a Comment