Thursday, 30 May 2013

SIKU YA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA KUMI NA SABA(17) YA WIKI YA MAZIWA SONGEA-RUVUMA YAFANA



Mkuu wa mkoa wa RUVUMA SAID MWAMBUNGU amezindua maadhimisho ya 17 ya wiki ya maziwa nchini na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuwa na utamaduni wa kunywa maziwa kwa wingi kwa lengo la kuboresha afya zao

Akizungumza na wananchi na wadau wa maziwa katika viwanja vya manispaa ya SONGEA MWAMBUNGU alisema  kati ya lita bilioni 1.6 za maziwa zinazozalishwa hapa nchi kwa mwaka ni wastani wa lita 11.6 tu zinazonywewa na mtu mmoja wa mkoa wa Ruvuma kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na viwango vya kimataifa vya lita 200 kwa mtu kwa mwaka.
Maadimisho hayo ya wiki ya maziwa ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mkoaniMkoani Ruvuma ambapo MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU aliwaamasisha wananchi wa mkoa wake kuongeza kasi ya unywaji wa maziwa sambamba na kufuga ng’ombe wa kisasa wanaotoa maziwa mengi badala ya ng’ombe wa asili ambao uzalishaji wao ni mdogo.

Maadhimisho haya yameambatana na maonyesho ya bidhaa mbalimbali za maziwa pamoja utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa unywaji maziwa, usindikaji na uzalishaji wake hata hivyo baadhi ya wadau wa maziwa kutoka vyama vya usindikaji maziwa wamesema maziwa mengi yanayozalishwa hapa nchini yanashindwa kuwafikia wanywaji kutokana na asilimia chache zinazosindikwa.
Wiki ya maziwa iliyozinduliwa leo mkoani hapa itaendelea kwa siku nne zijazo ambapo hapo kesho madereva wa pikipiki maarufu kama YEBOYEBO, wafungwa na wagonjwa hospitalini watagawiwa maziwa ya bure kama sehemu ya uhamasishaji


No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO