Friday, May 24, 2013
Kwa kweli kila ndugu
zangu ninapotazama picha hii natamani kuwepo mjadala wa kitaifa juu ya
hatma ya rasilimali hii ya wanyamapori hususani Tembo, maana kuna kila
dalili kuwa kama hali itaendelea hivi sio muda mrefu Tembo watapukutika
kama walivyopukutika Faru.
Hizi ni pembe za ndovu zilizokamatwa huko nchini China baada ya kubambwa na vyombo vya usalama vya China.
Tembo wakiwa na furaha lakini hizo pembe walizonazo ndizo zinazowaponza.
CHADEMA WARUHUSIWA KUFANYA MKUTANO SONGEA.
Habari tulizozipata hivi
punde zinasema Baada ya Mkutano wa pamoja kati ya viongozi wa vyama vya
siasa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, hatimaye Chama cha
Democrasia na Maendeleo CHADEMA kimeruhusiwa kufanya Mkutano wake wa
kampeni ya M4C uliopangwa kufanyika tarehe 26 Mei 2013. Mkutano huo
utafanyika Mjini Songea katika eneo la Matarawe Mjini Songea.
Hata hivyo katika
makubaliano hayo, CHADEMA imekataliwa kufanya maandamano kama
ilivyopangwa awali ambapo ilitangazwa kuwa Mkutano wa hadhara
ungetanguliwa na maandamano ambayo yangeanzia katika Chuo Kikuu Huria
hadi Matarawe.
Kufutwa na baadaye
kuruhusiwa kwa Mkutano wa CHADEMA kumeleta mkanganyiko kwa wananchi wa
Manispaa ya Songea kutokana na kubadilika kwa maamuzi ya Dola katika
kipindi kifupi.
Habari pia zinaeleza
kuwa Baada ya Mkutano wa CHADEMA hapo Mei 26, Chama Cha Mapinduzi CCM
pia kitafanya mkutano wake hapa Songea Juni 02, 2013 ambapo Katibu Mkuu
wa CCM Abdulahaman Kinana anatarajiwa kufanya Mkutano huo ikiwa ni
sehemu ya ziara ya viongozi waandamizi wa Chama hicho nchi nzima.
Mikutano hiyo ina lengo la kukagua uhai wa Chama pamoja na kutembelea na
kuzungumza na mabalozi wa nyumba kumi, viongozi wa mashina ambayo ni
uti wa mgongo wa Chama, matawi, kata, wilaya na mkoa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki
No comments:
Post a Comment