Dkt. Hussein Mwinyi
Akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa Mwaka wa Fedha wa 20013/2014,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi alisema chanjo hiyo
aina ya TAMOVAC-01 imeshirikisha watu 60 katika Mkoa wa Mbeya.
Hii ni mara ya pili kwa Serikali
kufanya utafiti kama huo. Mara ya kwanza ulihusisha wanajeshi, askari
polisi na magereza wapatao 60 wa Dar es Salaam ambao walipewa dawa na
kuachwa waendelee na maisha yao ya kawaida kwa muda wa miaka mitano.
Hata hivyo, alipoulizwa jana jioni kuhusu utafiti huo wa awali ulipoishia Dk Mwinyi alisema: “Huu ni utafiti mwingine ule wa awali ulikatizwa.” Alisema utafiti wa awamu ya pili unaendelea na umeonyesha mafanikio makubwa.
Hata hivyo, alipoulizwa jana jioni kuhusu utafiti huo wa awali ulipoishia Dk Mwinyi alisema: “Huu ni utafiti mwingine ule wa awali ulikatizwa.” Alisema utafiti wa awamu ya pili unaendelea na umeonyesha mafanikio makubwa.
Alisema taasisi hiyo pia iliendelea na
utafiti wa awamu ya tatu wa chanjo ya malaria iitwayo RTS, S/AS01E na
matokeo yake kwa watoto wa rika la wiki sita hadi 12 yalionyesha kuwa
ina ubora sawa na chanjo zitolewazo kwa watoto na inazalisha viini
kinga.
“Chanjo hii ilipunguza watoto kuugua malaria mara kwa mara kwa kiwango cha asilimia 30 kwa mwaka mmoja wa ufuatiliaji,” alisema.
“Chanjo hii ilipunguza watoto kuugua malaria mara kwa mara kwa kiwango cha asilimia 30 kwa mwaka mmoja wa ufuatiliaji,” alisema.
Alisema utafiti huo ulihusisha vijiji
34 vya Wilaya za Handeni na Korogwe na jumla ya watoto 1,505 chini ya
miezi 17 walipata chanjo ya malaria au chanjo ya kilinganishi na
walikamilisha kupatiwa dozi ya nyongeza ilipofikia robo ya nne ya mwaka
2012 na ufuatiliaji unaendelea.
Alisema Serikali imepata mafanikio
katika juhudi za kudhibiti magonjwa ya Ukimwi na malaria kutokana na
utafiti uliofanywa mwaka 2011/12 kuhusu viashiria vya magonjwa hayo
kuonyesha kuwa malaria imepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2007/08 hadi
asilimia 10 mwaka 2011/12.
Alisema taasisi hiyo itaendelea na
utafiti wa chanjo dhidi ya Ukimwi na awamu hii itahusisha washiriki 80
katika Mkoa wa Mbeya lakini pia itaendelea na hatua ya kwanza ya utafiti
ujulikanao kama R 262 utakaochunguza aina nyingine ya chanjo ya DA na
MVA dhidi ya Ukimwi kwa lengo la kubaini ubora na usalama wa chanjo hiyo
mpya kwa kuchanja washiriki 20 mkoani Mbeya.
Waziri Mwinyi alisema wizara imeomba
cha Sh47,282,941,000 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
ambao kati ya fedha hizo Sh36,1000,000 ni fedha za ndani na
Sh435,182,941,000 zinatoka kwa asasi za kimataifa na wadau wa maendeleo.
Alipoulizwa baadaye sababu za bajeti
hiyo kuwa tegemezi kwa zaidi ya asilimia 80, alisema Serikali imeamua
kupeleka fedha nyingine katika matumizi mengine ya msingi baada ya
kuhakikishiwa kupatiwa fedha na wahisani.
Alisema wizara pia imepanga kuajiri wataalamu 612 wa kada mbalimbali na kuwapandisha vyeo watumishi 707.
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Antony Mbassa alizungumzia tatizo
la dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi (ARV) na kuitaka Serikali
kutoa taarifa juu ya makopo 4,000 kama yameondolewa sokoni ili watumiaji
wasiathirike.
Mwaka jana gazeti hili lilifichua taarifa za kuwapo ARV bandia sokoni baadhi zikiwa zimeanza kutumiwa.
Taarifa hizo ambazo zilithibitishwa na
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), ziliibua mjadala ambao
uliilazimu Serikali kuwasimamisha maofisa kadhaa wa Bohari ya Dawa
(MSD).
Dk Mbassa alizungumzia dawa ya
‘Kikombe cha Babu wa Samunge’ inayotolewa na Mchungaji Ambilikile
Mwaisapile akitaka ifanyiwe utafiti na kushauri kuanzishwa kwa taasisi
ya kitaifa ya takwimu za dawa za asili na kuibua mipango
itakayohamasisha wananchi kutumia tiba asili. Chanzo:
www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment