RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA BALOZI TANDAU DAR.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Waziri
wa Zamani wa Kazi ,Marehemu Balozi Alfred Tandau wakati wa mazishi
yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Marehemu
Alfred Tandau ambaye alishika nyadhifa mbalimbali serikalini alifariki
tarehe 30 Mwezi Aprili wiki iliyopita. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.
Picha na Ikulu
No comments:
Post a Comment