Na Nathan Mtega,Songea
MWILI wa marehemu
aliyekuwa mwandishi wa vikao vya Bunge la Tanzania
Ernest Zulu umezikwa katika makaburi ya kichifu yaliyopo Maposeni Peramiho
wilayani Songea mkoani Ruvuma huku mazishi
hayo yakifanyika bila kuhudhuriwa na familia yake jambo ambalo liliwashangaza
baadhi ya watu waliohudhuria mazishi hayo.
Wakiongea kwa sauti za chini kwenye mazishi
hayo baadhi ya wakazi wa Peramiho walisema kuwa wameshangazwa kuona wasifu wa
marehemu ukisomwa na kuonyesha kuwa marehemu amewaacha watoto wanne na mke
mmoja lakini cha ajabu hawaonekani kwenye msiba huo.
Kwa
upande wake kaka wa marehemu chifu Emmanuel
Zulu akiwashukuru mamia ya watu walioshiriki kwenye mazishi hayo akiwemo akiwemo
Mbunge aliyetumwa na bunge la jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuja kuwakilisha mazishi hayo Abdukalim Shaha
wa jimbo la Mafia Zanzibar
alisema kuwa yeye hana cha zaidi ya
kumshukuru Mungu aliyetenda mambo hayo.
Aidha kwa upande wake Mbunge Abdukalim Shaha
akitoa salaamu za bunge amewataka viongozi wa dini zote kuendelea kujenga
mshikamano wa kuliombea taifa lisiingie kwenye machafuko maana amani ikitoweka
hakuna atakayekuwa huru kwa kufanya kazi zake.
Alisema kuwa marehemu Ernest Zulu
alitokea katika familia ya kichifu lakini kafanya mambo mazuri mengi katika
taifa kwa sababu wazazi wake walikuwa wakihimiza amani na utulivu vidumu siku
zote na siyo vinginevyo hivyo jamii inapaswa kuiga na kuendeleza moyo huo wa
uzalendo.
Alisema kuwa hali ya sasa inayojitokeza katika vikao vya bunge kwa
baadhi ya viongozi kutaka kushikana mwilini hivyo ni vyema jamiin kwa ujumla ikasaidiana
kumuomba Mungu aweze kuepusha balaa hasa kwa kuwakemea vijana waachane na
ushabiki usiyokuwa wa msingi.
Hata hivyo aliipongeza ofisi ya mkuu wa wilaya
ya Songea kwa kazi nzuri ya kufanikisha maandalizi ya mazishi hayo kwa
kuwapokea wageni na kufanikisha kuwapa huduma na kuwa hiyo wanaenda kuiweka
kwenye rekodi ya ofisi ya Mbunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Lakini pamoja na wakazi hao kuhudhuria
kwenye mazishi hayo wakiwemo viongozi wa safari ya mwisho ya Ernest Zulu lakini
wananchi hao walionyeshwa kutoridhika kwa kutokuwepo Mbunge hata mmoja wa
mkoani hapo zaidi ya wawakilishi.
No comments:
Post a Comment