Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wakata
miwa wa mashamba ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar chini
ya kocha mkuu Merky Mexime wanatarajia kuwasili kesho jiji la Maji
Chumvi, Dar es salaam tayari kwa kipute cha kufunga pazia la ligi kuu
soka Tanzania bara msimu wa 2012/2013 dhidi ya maafande waliohaha
kiukweli kujinusuru na makasi wa kushuka daraja na hatimaye kufanikiwa,
JKR Ruvu ya Mkaoni Pwani.
Meneja wa klabu hiyo, David Bugoya ameimbia FULLSHANGWE
Kuwa wanawasili kesho mchana na jioni watapasha misuli kusubiri kipute
cha kesho kutwa (Mei 18) mwaka huu katika uwanja wa Chamazi maeneo ya
Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
“Tumejiandaa
kwa muda mrefu na hapo kesho tutafika na kumalizia mazoezi yetu Dar es
salaam, kocha wetu amefanya marekebisho ya makosa yaliyokuwepo katika
kikosi chetu hivyo tuna matumaini ya kufanya vizuri”. Alisema Bugoya.
Akizungumzia
hali ya wanandinga wao, Bugoya alisema wachezaji wote wapo salama na
hakuna majeruhi mpaka sasa, hivyo mwalimu anajua nini cha kufanya ili
kupata kikosi cha kuwafunga JKT Ruvu wakiwa nyumbani kwao.
“Mchezaji
wetu Hussein Javu sasa yuko fiti sana, mchezo uliopita alifunga mabao
mawili, sasa yuko vizuri zaidi na tutamtumia ipasavyo katika mchezo wetu
wa kesho kutwa uwanja wa Chamazi”. Alisema Bugoya.
Mtibwa
Sugar katika msimamo wa ligi kuu wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi 39
kibindoni, wakati wapinzani wao wa mwisho JKR Ruvu chini ya kocha mpya
Keny Mwaisabula “Mzazi” wapo nafasi ya 10 na pointi 26.
Kwa
upande wa kocha Keny Mwaisabula amesema kuwa kikosi kipo shwari na
wamejiandaa vizuri kukabiliana na Mtibwa, lakini hesabu zake kubwa ni
msimu ujao wa ligi ambapo ataiongoza timu hiyo kurithi mikoba ya kocha
aliyejiuzulu kuifundisha klabu hiyo Charles Kilinda.
“Kikosi
cha JKT Ruvu ni kizuri sana, kina wachezaji wanaojua soka,
kinachokosekana ni kujiamini pamoja na kuwajenga kisaikolojia, kazi hii
nitaifanya vizuri baada ya msimu huu kumalizika, ili kuhusu mchezo wa
kesho kutwa tumejiandaa vizuri”. Alisema Mwaisabula.
Timu
za Mgambo Shooting, Polisi Morogoro, Africa Lyon na Toto Africans zina
hali ngumu sana na tunaweza kuzungumza mengine baada ya mei 18 mwaka huu
kwa maana ya tatu kati ya hizo kushuka daraja na kutoa nafasi kwa Mbeya
City, Rhino Rangers na Ashant United kucheza ligi hiyo baada ya
kufanikiwa kupanda msimu huu.
No comments:
Post a Comment