Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahmoud Mgimwa akijibu swali bungeni.
……………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-Maelezo,Dodoma
SERIKALI imejidhatiti katika kudhibiti ujangili na biashara
haramu ya mazao ya maliasili kwa kuridhia na kutekeleza mikataba minne
ya kudhibiti ujangali wa tembo na unaovuka mipaka na kulinda mapori ya
akiba.