Friday 30 August 2013

KUELEKEA SIKU YA MAHUJAA ASKARI WA JWTZ BRIGEDIA YA KUSINI YA FANYA USFI KATIKA MANISPAA YA SONGEA MKOANI RUVUMA

                                     Hapa ni katika ghuba lililopo katika soko la Manzese Songea
                                                     Takataka zilikuwa zinaziba barabara

                                                      Hapa ni hospitali ya mkoa wa Ruvuma


Thursday 29 August 2013

WALEMAVU WAKUTANA RUVUMA KUTOA MAONI YAO YANAYOPENDEKEZWA KUINGIA KWENYE KATIBA MPYA


                                         Hapa wakiwa kwenye makundi kujadili maoni




                                                               Wanafunzi wa Songea boys

                                    Wanfunzi wa shule ya msingi luhila nao walishiriki

Tuesday 27 August 2013

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU FACULT YA JOURNALISM WALIPOTEMBELEA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA KWA MAFUNZO ZAIDI

                                          Mwenye shati jeupe ni Vicenti kazimoto kutoka UDSM

                   Mariamu Juma kutoka Sauti Mwanza na Rashid Issa kutoka UDSM
 Wa kwanza kushoto ni Rauph Mohamedi kutoka Musoma collage wakielekea kwenye ghala la Tumbaku

STORY YA PUNDA

Siku moja punda wa mkulima alianguka ndani ya kisima. Mnyama huyo alipiga kelele kinyonge kwa masaa kadhaa wakati mkulima akijaribu kufikiri nini cha kufanya.
 
Hatimaye, aliamua kwakuwa punda wake alikuwa mzee, na pia kisima hicho kilihitaji kufunikwa juu, Akaona hapakuwa na haja ya kumtoa.
 
Akaita majirani zake wote waje kumsaidia. Wao wote wakachukua makoleo na kuanza kuchota taka kwa koleo na kuzitupia ndani ya kisima.
 
Mara ya kwanza, punda aligundua nini kilikuwa kinatokea akapiga kelele kwa nguvu. Basi, ikawashanganza wale watu punda aliponyamaza ghafla!
Baada ya kutupa taka kadhaa kwenye hicho kisima. Huyo mkulima alishangazwa na kile alichokiona. Kwamba kila koleo la taka lililorushwa juu ya mgongo wa punda, punda alikuwa akifanya kitu cha kushangaza. Alikuwa akijitikisa ili taka zimwagike chini huku akipiga hatua moja kuja juu.

Kadri mkulima na majirani walivyoendelea kutupa uchafu kwa koleo juu ya punda yule, alizidi kutikisa mgongo wake na kupiga hatua moja kuja juu. Muda mfupi baadae, kila mtu alishangaa jinsi punda alivyozidi kutokeza ndani ya kisima na kuja juu.



FUNZO:
Maisha yatakutupia kila aina ya uchafu. Ili utoke nje ya kisima wahitaji kujitikisa na kuchukua hatua moja juu. Kila tatizo ulilonalo, ni jiwe la kukuwezesha kukanyaga na kupiga hatua kuja juu. Tunaweza kutoka nje ya kisima kirefu kwa kuongeza bidii ya kupiga hatua moja kuja juu bila kuacha na kutokata tamaa kamwe. Tikisa itikisa uchafu mbali na kuchukua hatua kuja juu.
Kumbuka kanuni 5 rahisi ili uwe na furaha:
1. Weka huru moyo wako mbali na chuki - Samehe.

2. Weka huru akili yako mbali na wasiwasi - Wengi hushindwa kabisa kipengele hiki.

3.Tosheka / rizika na ulichonacho.

4. Toa zaidi.

5. Tarajia vichache kutoka kwa watu lakini zaidi kutoka kwako mwenyewe
.

Una uchaguzi wa aina mbili ...
i) Tabasamu na funga ujumbe huu,
ii) au tuma ujumbe huu kwa mtu mwingine ili ashiriki somo hili

Imetumwa na: Dr. Emeria A. Mugonzibwa - Mwanga.
 

JESHI LA POLISI LAMWAGA AJIRA


JESHI la Polisi nchini, limetangaza ajira mpya kwa vijana waliohitimu kidato cha nne na sita mwaka jana. Taarifa za jeshi hilo, ambazo zimewekwa kwenye mtandao wa jeshi hilo, zinasema vijana katika mikoa yote wanatakiwa kufika kwenye ofisi za makamanda wa polisi mikoa kwa ajili ya usaili.

Taarifa hiyo, ilisema kila mkoa umepangiwa siku yake na kwamba kila kijana anapaswa kuwa na vyeti halisi vya elimu yake pamoja na cheti cha kuzaliwa. “Kwa wale wote walioomba nafasi hii, wanapaswa kufika kwenye ofisi husika, hasa vijana waliohitimu kidato cha nne mwaka 2012 na wale waliohitimu kidato cha sita mwaka 2013.

“Katika kundi hili, wapo waliochaguliwa wajitokeze kwenye usaili kabla ya kujiunga na jeshi la polisi,” ilisema taarifa hiyo.

“Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha, ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili.

“Jeshi la Polisi, halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili ilhali jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.

“Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, ilisema kuwa kila mwombaji anapaswa kuwa na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa.

“Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema ni mapema kutoa idadi kamili ya vijana wanaotakiwa kwa sababu bado wapo kwenye mchakato.

“Siwezi kukwambia tunachukua wangapi, tumetangaza nafasi za kazi bado tupo kwenye mchakato… hii inategemeana na bajeti yetu tuliyonayo, tukikamilisha tutawaambia tu,” alisema Senso.

Monday 26 August 2013

BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA BMT LAFANYA MAFUNZO YA WAAMUZI WA MICHEZO KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI _RUVUMA

Na Mhaiki Andrew, Songea


BARAZA la michezo la Taifa(BMT) kwa kushirikiana na Mashirikisho matatu ya michezo ikiwemo Soka(TFF), riadha(RT) na wavu(TAVA) wataendesha mafunzo ya waamuzi wa michezo hiyo kwa wanafunzi wa Sekondari na shule za msingi mkoani Ruvuma, mafunzo hayo yanatarajia kuanza kufanyika (Jumatatu).


   Akizungumza na mwandishi wa habari hii  jana, Afisa Michezo,Utamaduni na vijana mkoa wa Ruvuma, Hassan Katuli alisema kuwa mafunzo hayo yatafanyika kwa siku nne kwa lengo la kuwapata waamuzi ambao watachezesha mashindano ya UMISSETA na UMISHUMTA kwenye ngazi ya mkoa.


   Alisema mafunzo hayo yatashirikisha wilaya zote sita za mkoa wa Ruvuma na Maofisa Michezo ndio walioachiwa majukumu ya kuraatibu na kuteua washiriki wa kushiriki mafunzo hayo kwa kuteua vijana kutoka shule za msingi na Sekondari katika wilaya zao,wilaya hizo sita kuwa Nyasa, Namtumbo, Tunduru, Mbinga, Songea Manispaa na Songea vijijini.


   Alisema kila wilaya itateua vijana 10 kuhudhuria mafunzo ya soka, 12 watahudhuria mafunzo ya uamuzi wa mpira wa wavu na wanafunzi 13 watapata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya uamuzi wa riadha ambayo yataendeshwa kwa vitendo na nadharia na wanafunzi ambao wanaotarajia kumaliza elimu ya msingi na Sekondari hawataruhusiwa kuhudhuria mafunzo hayo.


  Katuli, pia alisema Afisa michezo  hatakaye shindwa kuteua wanafunzi wa kuhudhuria mafunzo hayo kutokana na chuki zake binafsi alidai ofisi ya Mkuu wa mkoa itamchukulia hatua kwa kumwajibisha kwa kufuata misingi ya utumishi wa umma, ili kuweza kudhibiti uzembe ambao unaweza kujitokeza na kuwepo na visingizio vya kushindwa kutekeleza hilo


    Alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa wanafunzi kwani yatakuwa yanamjengea uwezo na hamasa ya kupenda michezo kwa kujiendeleza baadaye, punde atakapomaliza elimu ya msingi na Sekondari , badala ya kutegemea kuomba waamuzi kutoka kwenye vyama na kwenda kuchezesha mashindano ya UMISSETA na UMISHUMTA kila mwaka.


MWISHO

HATIMAYE "FOOLISH AGE" YA LULU MICHAEL YARUHUSIWA BAADA YA KUZUIWA

 
Bodi  ya   ukaguzi  wa  filamu  Tanzania  imeridhia  na  kuiruhusu  filamu  ya  Foolish Age  ya  Lulu  Michael  iingie  sokoni  baada  ya  kuizuia  hapo  juzi....

Filam  hiyo  ilizuiliwa   kutokana  na  mavazi  ya  nusu  uchi  yaliyokuwa  yamevaliwa  na  washiriki  wake  na  kumtaka  Lulu  Michael  aifanyie  marekebisho  kwa  kuviondoa  vipande  hivyo  ambavyo  vilikuwa  kinyume  na  maadili  ya  kitanzani....

Filamu hiyo  ambayo yupo Lulu, Diana Kimaro, Jengua na Hashim Kambi itazinduliwa tarehe 30 mwezi huu katika ukumbi wa Mlimani City

Kupitia  account  yake  ya  instagram, Lulu  amepost  ujumbe  huu.

 

DILLISH TOKA NAMIBIA AIBUKA MSHINDI WA BIG BROTHER AFRICA 2013

 
Fainali za Big Brother zimefikia  tamati  usiku  huu  zikiwa  na  washiriki  watano  ambao  ni  Beverly, Melvin, Cleo, Elikem  na  Dillish.

Mshiriki  wa  kwanza  kutolewa  alikuwa  ni  Beverly  akifuatiwa  na  Melvin  huku  Elikem  akiwa  ni  mshiriki  wa  tatu  kutolewa..

Mchujo  huo  uliwafanya  Cleo  na  Dillish  waingie  katika  masaa  ya  fainali za  mwisho  ambapo  Cleo  alielemewa  na  kutolewa  huku  akimwacha  Dillish  akichekelea  $300,000  za  ushindi  wa  shindano  hilo....

Agalia  jinsi  kura  zilivyopigwa:
 Angola: Dillish
Botswana: Cleo
Ghana: Elikem
Kenya: Dillish
Ethiopia: Beverly
Malawi: Cleo
Namibia: Dillish
Nigeria: Melvin
South Africa: Cleo
Sierra Leone: Elikem
Tanzania: Dillish
Uganda: Dillish
Zambia: Cleo
Zimbabwe: Elikem
Rest of Africa: Melvin
Total

Dillish = 5, Cleo = 4, Elikem = 3, Melvin = 2, Beverly = 1.
 
Hongera sana Dillish

Thursday 22 August 2013

HITILAFU YA UMEME

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Felchesmi Mramba, aliyeinua mkono

(katikati), akiwaonesha baadhi ya waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, eneo lililounguzwa na
moto na kusababisha madhara katika nyaya za umeme wa Kampuni ya SONGAS juzi usiku. Tatizo hilo litasababisha kukosekana kwa umeme kwa kipindi cha wiki 2, katika baadhi ya maeneo jijini


Habari na gazeti la majira

KAMATI KUU YA CCM KUKUTANA KESHO



Thursday, August 22, 2013
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo.

  Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kinatarajiwa kufanyika kwa siku mbili Agosti 24 na 25, 2013 mjini Dodoma Chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete.
    Kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitakachofanyika Agosti 23,2013 mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye, maandalizi yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambacho kimeketi kwa Siku tatu kuanzia Agosti 20, 21 na leo 22, 2013 mjini Dodoma.
 Kwa mujibu wa Ndugu Nape, Ajenda Kuu ya kikao cha NEC ni kujadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya Katiba mpya, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mchakato wa chama Kama Baraza la Katiba la kitaasisi  kukamilisha mjumuisho wa mchango na maoni yake Tayari kuwasilisha kwa Tume ya Katiba.
         Ndugu Nape alisema mpaka sasa CCM na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kujadili na kutoa maoni yao kuanzia ngazi ya Chini ya mashina na Matawi.
Mwisho

RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU WAKE


Imeandikwa na Na Magreth  Kinabo  na Eleuteri  Mangi — RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi za juu za utendaji wa Serikalini kwenye nafasi za Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Wizara mbalimbali, ambapo  wapo waliohamishwa, wataopangiwa kazi nyingine na yumo anayestaafu.

Kauli hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Rais amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za Serikali katika ngazi hizo za juu,” alisema Balozi Sefue.

Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo:

  • Dk Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

  • Joyce Mapunjo amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, Biashara na Masoko.

  • Jumanne Sagini amekuwa Katibu  Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) awali alikuwa Naibu Katibu  Ofisi wa Waziri Mkuu - TAMISEMI.

  • Dk Servacius Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, awali alikuwa Naibu Katibu Wizara ya
Fedha.
  • Dk Patrick Makungu amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, awali alikuwa  Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.

  • Alphayo Kitanda amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.

  • Dk Shaaban Mwinjaka amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, Biashara na Masoko.

  • Dk Uledi Mussa amekuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, Biashara na Masoko, awali alikuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

  • Profesa Sifuni Mchome amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya  Elimu na Mafunzo ya Ufundi, awali alikuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.

  • Charles Pallangyo amekuwa Katibu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri.

  • Anna Maembe amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, awali  alikuwa Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo.

  • Sihaba Nkinga amekuwa Katibu  Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo.

  • Sophia Kaduma amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Balozi Sefue aliongeza kwamba:

  • Katibu Mkuu aliyepewa uhamisho ni  Peniel  Lyimo ambaye anahamia Ofisi ya Rais - Ikulu  kwenye “Presidential’s Delivery Bureau” kama Naibu Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi ya Kilimo mwanzoni alikuwa  Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu.

Makatibu wakuu watakaopangiwa kazi nyingine ni:-

  • Sethi Kamuhanda aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo 
  • Kijakazi Mtengwa aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto 
  • Injinia Omari  Chambo aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi

Katibu anayestaafu ni Patrick Rutabanzibwa ambaye alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambaye sasa amestaafu kwa hiari.

Aidha, Balozi Sefue alisema Rais Kikwete pia amefanya uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu wapya na kuwapa uhamisho baadhi yao.  Aliiwataja Naibu Makatibu Wakuu wapya walioteuliwa kuwa ni:-
  • Angelina  Madete amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais  Mazingira

  • Regina Kikuli amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu

  • Zuberi Sumataba amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, anayeshughulikia  suala la elimu katika ngazi za Serikali za Mitaa

  • Edwin Kiliba amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI

  • Deodatus Mtasiwa amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI ambaye atashughulikia saula la afya  upande wa  Serikali za Mitaa.

  • Dk Yamungu Kayandabila amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

  • Profesa Adolf Mkenda amekuwa Naibu Katibu Mkuu ya Fedha anayeshughulikia sera

  • Dorothy Mwanyika amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Fedha anayeshughulikia Fedha za Nje na Madeni

  • Rose Shelukindo amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

  • Dk Selassie Mayunga amekuwa Naibu Katibu Mkuu  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  • Monica Mwamunyange amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi

  • Consolata Mgimba amekuwa  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Elimu na Mafunzo ya Ufundi

  • Profesa Elisante ole Gabriel Laizer amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

  • Armantius Msole amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Balozi Sefue aliwataja Naibu Makatibu Wakuu waliopewa uhamisho kuwa ni:-
  • John Mngondo ambaye amehamishiwa Wizara ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ametoka Wizara ya Uchukuzi katika nafasi hiyo

  • Selestine Gesimba amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, anatoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

  • Injinia Ngosi Mwihava anahamia Wizara ya Nishati na Madini kutokea Ofisi ya Makamu wa Rais

  • Maria Bilia amehamia Wizara ya Viwanda na Biashara kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 

  • Nuru Milao anahamia  Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MSAMALA SONGEA WALIPOTEMBELEA CHUO CHA VETA SONGEA


                                                        Hapa wakiwa katika darasa la komputa
  Wengine wamevutiwa kuendelea na masomo ya komputa baada ya kumaliza kidato cha nne

                          Umwagiliaji bustani ya nyasi kwa kutumia maji ya kwenye chupa maji
        Tekinologia ya kumwagilia bustani ya maua katika chuo cha veta ubunifu wa hali ya juu 
                              Dagaa nyasa waliowekwa karanga watamu sana kwa wali
                            Wakina mama wakiwa wanauza dagaa nyasa katika soko kuu la Songea
                                                         Dagaa nyasa zikiwa juani 

Sunday 18 August 2013

 Baadhi ya waandishi wa habari wa manispaa ya Songea wakiwa kwenye picha ya pamoja na mwezeshaji wa mafunzo ya internet and Journalism aliyekaa katikati.
 Wa kwanza kushoto ni Sengiyumva  Gasiligwa na Saimon Berege wakiwa kwenye picha ya ukumbusho katika jengo la veta
Wa kwanza kushoto ni Saimoni Berege, wa pili ni Lusajo mwalimu wa Veta wa tatu ni Gasiligwa  wa nne Juma Nyumayo na wa tano ni mhariri mkuu wa Peramiho printing Oswald Ngonyani

Friday 16 August 2013

SIKU YA TATU YA MAFUNZO YA INTERNET AND JOURNALISM KWA WAANDIHI WA HABARI WA RUVUMA


 Siku ya tatu waandishi wa habari wa ruvuma wamaliza mafunzo kwa mafanikio Mwenye Red shukuru wa jogoo fm na Emmanuel Msigwa wa Channel ten
                                   Mwandishi wa habari kutoka Namtumbo Ngerangera
                               Joyce Joliga wa mwananchi na Kassian Nyandindi wa Mbinga
                                             Mwezeshaji Saimon Berege akielekeza jambo
                                                    Waandishi wanafuatilia kwa makini

Thursday 15 August 2013

MSHINDI MISS ILALA KULAMBA MILIONI 1,500,000 KESHO

DSC_0134 

MREMBO atakayetwaa taji la Redds Miss Ilala 2013, linalofanyika kesho Agosti  16, ataondoka na zawadi za jumla ya Sh. Milioni 1,500,000,huku mshindi wa pili atajipatia shilingi milioni moja na wa tatu shilingi laki saba.  
Mbali na zawadi hiyo, washindi hao watatu watapata ofa ya ya miezi sita kutoka RIO gym & Spa, iliyopo Quality Center, kutumia vifaa vyote ndani ya gym hiyo ambayo gharama yake ni Milioni 900,000 kwa kila mtu.  
Sh , 400,000 zitakwenda kwa mshindi wa nne na atakayeshika nafasi ya tano yeye ataibuka na Sh 300,000. Washiriki wengine ambao hawatabahatika kuingia katika nafasi ya tano bora, wote watapewa Sh,200,000 kwa maana ya kifuta jasho. Tumelenga zawadi za fedha zaidi, hii ni kutokana na ugumu wa maandalizi kwa warembo ambao hugharamika zaidi, kiasi nasi kuona kuna kila namna ya kuwapunguzia maamivu hayo.  
Shindano hilo, linatarajiwa kuwa na burudani ya kipekee kutoka kundi zima la Tanzania House of Talent (THT) wakiongozwa na mwanadada mwenye sauti ya chiriku, Lina na Barnaba. Kundi la Wanne Star nalo litajumuika katika kuufanya usiku wa kesho kuwa wa burudani tosha kutokana na kuja kivingine kabisa katika nyimbo za asili za Afrika. Warembo watakaopanda jukwaani Julai 5 ni kutoka Kigamboni, Kurasini na Chang’ombe ambao wanawania taji linaloshikiliwa na Miss Tanzania namba tatu, Edda Sylvester walikuwa chini ya wakufunzi Suzy Mwenda na Shadya Mohamed wakati kwenye kucheza nako walikuwa na walimu wawili Super Bokilo na Charles.  
Warembo wataoapanda jukwaani hityo kesho ni 14 Diana Kato, Martha Gewe, Alice Issac, Irine Mwelelo, Clara Bayo, Natasha  
Mohamed, Doris Molel, Upendo Lema, Kabula Kibogoti, Shamim Mohamed, Kazunde Kitereja, Rehema Mpanda, Johanither Kabunga,Anna Johnson.  
Shindano hilo limedhaminiwa na kinywaji cha Redd’s, Dodoma Wine, Gazeti la Jambo Leo, Cloud’s Media, Blogu ya Wananchi (Le Mutuz), Fredito Entertainment, CXC Africa tours & Safaris, RIO Gym& Spa, Smile Internet, Delina Interprises na Kitwe General Traders. Ilala Interteinment  ndiyo inayoandaa mashindano haya, inatanguliza shukrani zake 

wadhamini wetu kwa miaka hiyo, sanjari na vyombo vyote vya habari kwa ujumla wake, kwani ndio waliofanikisha kufanikisha shughuli yetu ya kesho.
by John Bukuku 

SIKU YA PILI YA MAFUNZO YA INTERNET AND JOURNALISM NI VITENDO ZAIDI



        Wawezeshaji wa mafunzo hayo wa kwanza kushoto ni Sengiyumva Gasiliwa na Saimon Berege
         Shukran wa Jogoo fm wa kwanza kushoto, julius konala wa Radio maria na Ennes wa Jogoo fm
   Joyce Joliga mwandishi wa gazeti la mwanachi na Kassiani Nyandindi mwandishi wa habarikutoka Mbinga
                                     Emmanuel Msigwa mwandishi wa channel ten naye akifanya zoezi
  Mwenye red ni Oswald Ngonyani Mhariri mkuu wa printing peramiho na Friday Simbaya wakielekezana kwa vitendo namna ya kutafuta material katika mtandao
 Mwenye tai ni Ngaiwona Nkondora wa Radio Free Afrika  akipongezana na Juma Nyumayo baada ya kufanya vizuri katika mafunzo hayo
       Mwenye shati nyekundu ni Steven Augustino kutoka Tunduru na kassian Nyandindi wa Mbinga


Na Steven Augustino na Catherine Songea
 

WAANDISHI wa Habari Mkoani Ruvuma wameonywa kuamini habari kutoka
mitandao na kuzitumia kuhabarisha umma bila  kuzifanyia utafiti wa
kutosha katika internet na kutumia vyanzo vya kuaminika ikiwemo
kuwahoji wahusika kupata habari za ukweli ambazo zitakuwa na manufaa
kwa wasomaji.
 

 Hayo yameelezwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa namna ya
kuandika Habari kwa kutumia mitandao ya Internet na kutuma picha za
kihabari  Mtandaoni yanayoendeshwa katika Ukumbi wa Veta,Manispaa ya
Songea, Taasisi ya Vyombo vya habari kusini mwa Africa (Media
Institute Of Southern Africa) MISA TANZANIA.
 

Wanahabari hao pia wanafundishwa namna ya kufanya utafiti wa vyanzo
vya habari mbalimbali katika Internet na kufungua njia nyingine za
mawasiliano kama  ‘youtube’, Blogu na namna ya kuzitumia katika tasnia
ya kutengeneza na kutuma habari zikiwa na takwimu sahihi.
 


Awali akiongea katika ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tatu, Afisa
Habari MISA -TANZANIA , Sengiyuva Gasiligwa,  alisema kuwa lengo la
mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kwenda na
wakati hasa katika teknolojia ya kimtandao.
 


Wanahabari hao pia wananolewa ili waweze kujua kwa undani maana ya
internet, ‘Worid Wide Web’ , ‘Computer’,  na matumizi yake kwa manufaa
ya maendeleo ya technolojia, uchumi, siaa na utamaduni na kujali
maadili
Gasiligwa alisema kuwa mafunzo hayo yanayo wahusisha Waandishi wa
Habari za Magazeti, Terevissin na Radio yanafanyika kwa ushirikiano
MISATAN na shirika la VIKES  toka Finland na kwamba kwa kuanzia
mafunzo hayo yalifanyika Mkoani Pemba huku Zanzibar Tanzania Visiwani
na sasa Ruvuma na baadaye mkoani mwanza.
 

Nae mwezeshaji wa mafunzo hayo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini
Iringa,  Saimon Berege,  pamoja na mambo mengine aliwataka Wanahabari
hao kuwa na ari ya kujiendeleza kielimu na kuwakaribisha kwenda kusoma
digrii ya pili (masters) Inayotolewa na chuo hicho.
 

Wakiongea kwa nyakati tofauti wanahabari hao pamoja na kuipongeza
taasisi hiyo kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari
wamesema kuanzia sasa wataweza kufanya kazi za uandishi wa habari wa
kiuchambuzi kwa kuoanisha habari kutoka vyanzo vya mataifa mbalimbali,
kuandika habari kwa kutumia takwimu kutoka katika mitandao na kutumia
taarifa na hotuba zilizopita zilizotolewa na viongozi wa mataifa
mbalimbali duniani .
 

Aidha washiriki hao wameonyesha ushirikiano mkubwa katika uchambuzi wa
mada zilizotolewa na wameomba mafunzo kama hayo yatolewe mara nyingi
iwezekanavyo ili kuwakumbusha kuamsha ari ya waandishi.
 

Mwisho

TUPE MAONI YAKO