Tuesday 17 September 2013

TASWIRA YA MKUTANO KATI YA WAANDISHI WA HABARI NA WADAU WA HABARI RUVUMA













Na Steven Augustino, Tunduru
 

BAADHI ya Wakulima wa Korosho katika Kijiji cha Ligoma Kata ya
Namsakata Wilayani Tunduuru Mkoani Ruvuma wameonesha mashaka ya
kupatikana kwa mafanikio kupitia mpango wa Sensa ya Mikorosho na
kuwasaji Wakulima hao.
 

Mashaka hayo yalioneshwa na Liputa Ntenda Mbwana,Selemani Mohamed
Ally, Rashid  Ibrahimu  na Ishiwa Adam Njuga  wakati wakiongea na
waandishi wa habari ikiwa ni muda mfupi baada ya kusajiliwa  na
kuongeza kuwa endapo hakuta kuwa na udhibiti wa visumbufu vya soko la
mazao yao nguvu kubwa na lasilimali ya taifa inayotumika itakuwa
imeteketea bule.
 

Wakulima hao ambao walikuwa wakiongea kwa nyakati tofauti katika
mahojiano hao walivibainisha visumbufu hivyo kuwa ni pamoja na
kutokuwepo kwa mikakati ya kudumu ya kuwatafutia wakulima soko la
uhakika la mazao yao,bei mzuri  na udhibiti wa wanunuzi holela ambao
wanafahamika na Serikali na hununua kwa kutumia mfumo usio rasmi kwa
kutumia vipimo vya kangomba.
 

Aidha Wakulima hao waliuelezea mfumo huo kuwa ni mzuri na unaweza
kuwaletea manufaa makubwa endapo mipango na mikakati yake itatekelezwa
kwa vitendo na kwamba endapo mikakati hiyo itaishia katika makaratasi
kama ilivyo katika mipango mingine iliyowahi kuibuliwa na kufukiwa zao
hilo halitaendelea kamwe.
 

Awali wakiongea katika ufunguzi wa mafunzo ya Wataalamu wa Idara ya
Kilimo, watendaji Kata , Vijiji  watakao tekeleza zoezi hilo la
usajili wa Wakulima hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Klasta ya
Walimu Mlingoti kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya korosho Tanzania
(CBT) Sifuni Fadhili na Mkurugenzi wa Kilimo na Ubanguaji wa zao hilo
Luseshelo Silomba walimweleza Mkuu wa Wilaya hiyo Chande Nalicho
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa zoezi hilo kuwa zoezi
hili likikamilika litaisaidia serikali kuandaa na kupanga mikakati ya
uhakika na kuwainua wakulima wa zao hilo nchini.
 

Alisema kutokana na muhimu zoezi hilo Bodi ya Korosho Tanzania
imejipanga na kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika kwa uhakika na
kwamba kwavile wao ndio watakao iwakilisha bodi ya korosho katika
zoezi hilo pia aliahidi kuwatembelea mara kwa mara wakati watakapo
hitajii ya mikorosho na uzalishaji wake hasa katika uandaaji wa
hahitaji ya madawa wakati wa kupulizia.
 

Nae Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Mudhihir Mohamed
Mudhihir alimweleza Mkuu wa Wialaya hiyo kuwa Bodi ya korosho Tanzania
imedhamini na kuuenzi mchango wa wakulima wa zao hilo na kuamua
kufanya uzinduzi huo Kitaifa katika Tarafa za Namasakata na Nakapanya
Wilayani Tundnuru.
 

Alisema katika utekelezaji huo Bodi ya Korosho Tanzania kwa
kushirikiana na Mfuko wa kuendeleza tasnia ya zao la Korosho Tanzania
wamepanga kufanya usajili wa Mikorosho na wakulima wa zao hilo katika
Wilaya zote 41 zinazolima zao hilo.
 

Akiongea na Wakulima hao katika uzinduzi wa Sensa hiyo ya Mikorosho na
usajiri wa wakulima hao Mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya tunduru Chande
Bakari Nalicho pamoja na mambo mengine aliwataka Viongozi wote katika
maeneo yao kuacha tabia za kufanya kazi kwa mazowea na akawaasa
kutimiza wajibu wao kwavitendo ili kufanikisha zoezi hilo.
 

Dc Nalicho aliendelea kubainisha baadhi ya faida za mpango huo kuwa ni
pamoja na kuisaidia Serikali kupanga na kuandaa mikakati itakayo
wasaidia wakulima kusimamia na kuhudumia mazao yao kwa uhakika,
itaongeza uzalishaji na kudhibiti wanunuzi holela wa Korosho hizo
kutoka kwa wakulima kwani wataweza kuwahoji watu wasio wakulima yaliko
mashamba yao na waliko zitoa korosho wanazo ziuza.
Mwisho

Saturday 14 September 2013

PIGA KURA MARA NYINGI UWEZAVYO ILI KUIWEZESHA DEMASHONEWS IWEZE KUNYAKUA TUZO YA THE BEST GENERAL BLOG TANZANIA


Mpendwa msomaji tunashukuru kwa mapendekezo kupitia kura zako, hatimaye blog hii ya ww.demashonews.blogspot.com imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea tuzo ya THE BEST GENERAL BLOG, Tunakuomba hivi sasa uipigie kura blog hii ili iweze kuchukua tuzo hiyo. 

Ili kupiga kura yako tafadhali bonyeza link hii  the best General Blog na uchague palipoandikwa demashonews.blogspot.com

Asante kwa ushirikiano wako, piga mara nyingi uwezavyo

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUTOANDIKA HABARI ZITAKAZOVURUGA AMANI NA UTULIVU WA NCHI YETU.





Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakihakikisha wanapata kwa usahihi  wa habari

KINANA SHINYANGA KUNUFAIKA NA VIWANDA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi katika uzinduzi wa mradi wa vibanda vya biashara katika uwanja wa Kambarage huku akishuhudiwa na Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqinq.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwa baiskeli kutoka Uwanja wa Kambarage kuelekea uwanja wa Shycom kwenye mkutano wa hadhara.
Balozi wa China nchini Dk.Lu Youqinq akiwapungia wananchi wakati akielekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Shycom,Shinyanga mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Balozi wa China nchini wakiwasubiri wenzao tayari kuelekea kwenye uwanja wa Shycom ambapo mkutano mkubwa ulifanyika.
Kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Balozi wa China nchini na Mbunge wa Shinyanga mjini Steven Masele wakiendesha baiskeli kuelekea kwenye uwanja wa Shycom ambapo mkutano mkubwa na wa kihistoria ulifanyika leo tarehe 13 Septemba 2013.
 
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiingia kwenye uwanja wa Shycom na baiskeli tayari kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara.
 
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto),Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqinq na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye , Balozi wa China alipata fursa ya kuelezea kwa wananchi wa Shinyanga namna uwekezaji utaweza kuunufaisha mkoa huo ambapo viwanda vya nguo, kusindika mafuta, asali na bidhaa zitokanazo na mifugo vinategemewa kujengwa katika mkuo huo na kutoa nafasi kwa ajira ,kuinua uchumi ,elimu na kuondoa kabisa umasikini.

Friday 13 September 2013

TUNAOMBA UIPIGIE KURA DEMASHONEWS IWEZE KUNYAKUA TUZO YA THE BEST GENERAL BLOG TANZANIA


Mpendwa msomaji tunashukuru kwa mapendekezo kupitia kura zako, hatimaye blog hii ya ww.demashonews.blogspot.com imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea tuzo ya THE BEST GENERAL BLOG, Tunakuomba hivi sasa uipigie kura blog hii ili iweze kuchukua tuzo hiyo. 

Ili kupiga kura yako tafadhali bonyeza link hii  the best General Blog na uchague palipoandikwa demashonews.blogspot.com

Asante kwa ushirikiano wako, piga mara nyingi uwezavyo

Thursday 12 September 2013

KINANA- SERIKALI TATU TANZANIA ITASHANGAZA DUNIA.

 
Aonya zitasababisha machafuko 
 

Asema Tanzania itashangaza dunia
   

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendeleza msimamo wake wa kupinga muundo wa Serikali tatu kuingizwa katika Katiba mpya, kikisema kuwa muundo huo ni hatari kwa umoja na mshikamano wa taifa.
Chama hicho kimeonya kuhusu muundo huo na kusema kuwa Serikali zaidi ya mbili zinaweza kuvuruga ustawi wa taifa, kwani ni rahisi zaidi nchi kuingia katika machafuko.
Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Kinana alisema muundo wa Serikali tatu ni mzigo kwa taifa na kwamba Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na marais watatu, jambo ambalo halipo duniani kote. 
“Katiba ni jambo muhimu kwa ustawi wa nchi yetu, lakini katika hili la kuwa na Serikali tatu ni hatari, kwani kwa mujibu wa rasimu yetu ya sasa, inaonyesha kuwa kila Serikali itakuwa na mamlaka kamili.
“Ikiwa kutatokea serikali moja kati ya hizo tatu na moja ikasema sasa inanunua vifaa vya kujilinda, basi ile ya Zanzibar nayo itafanya hivyo na ile ya Muungano pia itafanya hivyo.
“Hata kama kuna vita serikali moja ikasema hatutaki nyingine itasema tunataka, mwishowe mtaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kinana na kuendelea: 
“Kwa hali hiyo, ninachotaka kuwaambia ni kuwa Katiba Mpya itaandikwa na maisha yale yale yataendelea. Afrika Kusini, India na Kenya wamebadili katiba zao, lakini hali ya maisha ya wananchi wao iko vilevile,” alisema.
Katika mkutano huo, Kinana alisema msimamo wa chama chake kuhusu muundo ni Serikali mbili na kueleza kuwa chama chake kitaheshimu maoni ya Watanzania kuhusu muundo wowote bila shinikizo la kisiasa.
Alisema hatua ya kuwa na wingi wa Serikali kuna hatari ya nchi kuwa na Bunge la Mabwenyenye na Bunge la Makabwela, ambapo alisema kuna hatari ya fedha za walipa kodi kutumika vibaya.
Kinana alionya hatua ya kuwa na ukubwa wa Serikali ambayo itakuwa mzigo kwa Watanzania, ambao wamekuwa wakiendesha kwa kulipa kodi zao.
“Hivi sasa nchi ipo katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya, ninapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa CCM itakuwa tayari kupokea maamuzi yoyote yatakayoamuliwa na wananchi.
“…. Na ikiwa mtaamua kuwa ya Serikali mbili, tatu hata tano sawa, lakini kubwa katika hili CCM hatuhitaji mchakato huu ufanyike kwa kuingiliwa kwa shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani au hata taasisi ambazo zimejificha kwa mlango wa nyuma.
“Sisi tulisema wazi tunapenda tuendelee na Serikali mbili, lakini katika hili tambueni kuwa na Serikali nyingi zaidi kuna hatari ya kuingia katika mifarakano na hata vita,” alisema Kinana.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa hatua ya baadhi ya watu kupita na kupandikiza chuki kuhusu Katiba Mpya, mawazo yao yanatakiwa kupimwa, kwani watu hao wana lengo la kuvunja badala ya kuimarisha umoja.
“Ni muhimu kuandika Katiba mpya ambayo itasaidia kuweka misingi bora na imara ya uongozi, lakini si kuwa na Katiba yenye utitiri wa kila aina ya Serikali, hili hapana, ila ikiwa mtaamua nyie wananchi wenyewe sisi hatuna pingamizi,” alisema.
Mapema Agosti mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, aliwataka wanachama wa CCM kujiandaa kisaikolojia na muundo wa Serikali tatu, ikiwa Watanzania wataamua hivyo.
Rais Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari kupitia vikao vya NEC mjini Dodoma, ambapo alisema mwaka 1992, kundi kubwa la wananchi lilipinga kuingia katika mfumo wa vyama vingi, lakini lilisikilizwa na nchi ikaingia kwenye mfumo huu

habari na udakuspecially .com 

Wednesday 11 September 2013

POLISI TANZANIA KUPATA MAFUNZO YA UPELELEZI NCHINI UTURUKI

Mademu jumla
Na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi la Uturuki limetoa ufadhili wa masomo kwa  askari kumi na saba ( 17) wa Jeshi la Polisi Tanzania kupata mafunzo mbalimbali yakiwemo ya upelelezi wa wahalifu na mbinu za uchunguzi wa kimaabara pamoja na usimamizi na uendeshaji wa gari la matukio yatakayochukua muda wa mwezi mmoja nchini Uturuki.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI) Kamishina Robart Manumba aliyasema hayo jana wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika Makao Makuu ya Polisi.
Alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya maboresho yanayolenga kuwaongezea askari weledi na kuwajengea uwezo wataalamu wa Maabara ya uchunguzi ya Polisi juu ya mbinu mbalimbali za kiuchunguzi na  upelelezi pamoja na matumizi sahihi ya vifaa  vya kiupelelezi.
Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia wataalamu wa Maabara ya uchunguzi ya Polisi kuweza kufanikisha kuwakamata wahalifu na kutambua   uhalifu uliotendeka kwa haraka,  hivyo, kupunguza uhalifu nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Maabara ya uchunguzi ya Jeshi la Polisi Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Abdularahaman Kaniki alisema kuwa mafunzo hayo ni muendelezo wa ushirikiano uliopo baina ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi la Uturuki ambao ulianza katika mafunzo ya upelelezi na ukusanyaji wa vielelezo katika eneo la tukio uliofanyika hapa nchini mwishoni mwa mwezi juni mwaka huu.
Aidha, aliwataka askari waliochaguliwa kushiriki mafunzo hayo kutumia fursa hiyo kujifunza kwa bidii ili kuongeza ufanisi pamoja na kuboresha utendaji  katika  maeneo mbalimbali ya upelelezi na Maabara ya  uchunguzi ya Polisi ili kufanikisha utambuzi wa uhalifu na wahalifu kwa haraka.

Mnyarwanda AJINYONGA baada ya kuamriwa arudi kwao RWANDA


Raia wa Rwanda amejinyonga kwa kamba chumbani kwake, tukio linalohusishwa na zoezi linaloendelea hivi sasa nchini la kuwasaka wahamiaji haramu na kuwarejesha makwao.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, marehemu anatajwa kuwa ni Francis Mathias (75), ambaye alikuwa mkazi wa kitongoji Kikukuru kata Kikukuru, tarafa Mabira wilayani Kyerwa mkoani Kagera.


Mwenyekiti wa kitongoji cha Kikukuru, Joseph Leo, jana alilithibitishia NIPASHE kutokea kwa tukio hilo na kuwa alipata taarifa hizo kutoka kwa binti wa marehemu juzi saa 3:00 asubuhi.


“Baada ya kupata hizo taarifa niliongozana na mgambo, tulipofika mlango wa chumba chake ulikuwa umefungwa kwa ndani, tukafanikiwa kuuvunja tukaingia ndani na kukuta amejitundika kwa kamba,” alisema Leo na kuongeza kuwa marehemu alikuwa mfugaji na mkulima.


Alisema kuwa kabla ya kujiua, mzee huyo alichana fedha za Kitanzania zinazokadiriwa kufikia Shilingi 


milioni saba zikiwamo noti za Sh. 5,000 na za Sh. 10,000, ambazo zilikutwa ndani ya chumba chake.


Leo alisema baada kushuhudia alipiga simu kwa Ofisa Mtendaji wa Kata Kikukuru ambaye alifika na kupiga ngoma na watu walikusanyika kushuhudia kilichotokea na baadaye kwenda kutoa taarifa  katika kituo cha Polisi.


Alipotakiwa na NIPASHE kuthibitisha kama kweli mwananchi wake aliyejinyonga alikuwa raia wa Rwanda, Leo alithibitisha na kufafanua kuwa tayari alikwisha kumuorodhesha kwa lengo la kurejeshwa kwao katika opereshani iliyoanza Jumamosi ya kuwarejesha makwao wahamiaji haramu wanaoishi mkoani Kagera.


Aliongeza kuwa aliwahi kumhoji marehemu Mathias ambaye alimweleza kuwa alikuja Tanzania kutoka Rwanda tangu mwaka mwaka 1976.


Naye Ofisa Tarafa ya Mabira, Nicolaus Rugemalira, alisema uchunguzi wa awali wa kimazingira umeonyesha kuwa kulikuwa na mgogoro wa familia baada ya marehemu kutaka wauze mali zao zote warudi Rwanda, lakini familia yake haikukubaliana naye kutokana na mkewe kuwa raia wa Tanzania.


“Mke wake ni Mtanzania, inaonekana baada ya familia yake kukataa uamuzi wake wa kuuza mali zote ili waondoke, aliamua kuchukua uamuzi huo,” alisema Rugemalira.


Akizungumzia tukio hilo, binti wa marehemu, Melania Francis, alithibitisha kuwapo ugomvi kati ya baba yake na mama yake hali iliyosababisha mama yao kuondoka bila kufahamika alikoelekea.


Alisema siku ya tukio aliamka na kuwaandaa wadogo zake kwenda shuleni na baada ya hapo alikwenda shambani kuona kama vibarua wameanza kazi ya kulima, lakini aliporudi nyumbani alishangaa kuona mlango wa chumba cha baba yake bado umefungwa wakati haikuwa kawaida yake kulala hadi saa moja.


Melania alisema alibisha hodi bila majibu, akajaribu kufungua ikashindikana na alipochungulia aliona fedha nyingi zimetapakaa ndipo alipokimbia kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji.


“Nafahamu baba alikuwa na uwezo wa kumiliki fedha hizo, lakini sikufahamu anazihifadhi wapi,” alisema binti huyo wa marehemu.


Alisema wamezaliwa watoto watano katika familia hiyo na kwamba ndugu zake wawili walitoweka na kubakia watatu na kuongeza kuwa kuwa anatambua kuwa baba yake alikuwa raia wa Rwanda.


Alipotakiwa kueleza kama anafahamu alikoelekea mama yake, binti huyo alidai kuwa hafahamu ingawa anafahamu kuwa ni mzaliwa wa Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera.


Kutokana na kutoweka kwa mama huyo pamoja na wanafamilia wengine, uongozi wa eneo hilo unaendelea na ufuatiliaji ili kujua wanafamilia wengine wamekwenda wapi.

-NIPASHE

SOMA TANGAZO KUTOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII:NAFASI ZA AJIRA KWA MADAKTARI, MADAKTARI WA MENO, TABIBU, TABIBU WASAIDIZI NA WATAALAMU WA MAABARA

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, inawatangazia Wahitimu wa taaluma zilizotajwa hapo juu kuwa zipo nafasi za kazi katika Mikoa na Halmashauri zote nchini isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam na Halmashauri zake.

Waombaji wanatakiwa kuambatanisha nyaraka zifuatazo katika maombi yao:-

  1. Vyeti vya Elimu ya Sekondari.
  2. Cheti cha Kuhitimu mafunzo ya taaluma husika.
  3. Kwa wale wanaotakiwa  Kwa mujibu wa sheria  kufanya mafunzo kwa vitendo, wawasilishe cheti cha kuhitimu mafunzo hayo.
Mwisho wa kupokea maombi ni wiki mbili kuanzia tarehe ya tangazo hili kutoka. Aidha, juu ya bahasha iandikwe nafasi inayoombwa.

Majina ya watakaopangiwa vituo vya kazi yatatangazwa kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz

Barua zote zipitie Posta. Aidha, barua zitakazoletwa kwa mkono hazitopokelewa
Maombi hayo yatumwe kwenye anuani ifuatayo:- 

KATIBU MKUU,
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.

Tuesday 10 September 2013

MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA ST JOSEPH SONGEA YAFANA







Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi dokta Shukuru Kawambwa amewataka wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini waliokopeshwa mikopo kwa ajili ya kupata elimu ya juu warejeshe mara wanapopata ajira ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kunufaika na mikopo hiyo.

Dokta kawambwa amesema hayo wakati akitoa hotuba katika mahafali ya nne ya chuo kikuu cha mtakatifu joseph kinachoto mafunzo ya tekinologia ya mawasiliano kilichopo songea mkoani Ruvuma.



Dokta kawambwa ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wajiri kushirikianan na serikali kuwatambua wafanyakazi wanaodaiwa mikopo na kuhakikisha wanalipa kwani kati ya shilingi trilioni 1.45 ni bilioni 35 tu ambazo zimesharudishwa.


Akizungumzia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma diploma ambalo ni ombi la jumiya ya chuo cha matakatifu joseph waziri wa elimu huyo amesema serikali itaangalia uwezekano lakini ni ngumu kwa hata wanafunzi wa shahada sio wote wanaopata mikopo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya songea mheshiwa Joseph Mkirikiti amekihakikishia kuwa ombi la kupata eneo  la ekari 2000 kwa ajili ya chuo cha kilimo litafanyiwa kazi hata kama sio zote kwa mara moja.


Naye askofu wa jimbo la mbinga JOHN NDIMBO amesema chuo hicho kinachukua wanafunzi wa dini mabalimbali na hata wasiokuwa na dini kwa lengo la kuboresha mahusiano mema . Katika mahafali ya mwaka huu jumla ya wanachuo 97 wamehitimu wakiwemo 59 wa shahada na 38 stashahada.

Chuo kikuu cha st joseph kinadhaminiwa na DMI na tayari kina vituo katika mikoa ya ARUSHA , SONGEA, DAR ES SALAAM. Na njombe.

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI MGENI RASMI KATIKA CHUO KIKUU CHA ST.JOSEPH RUVUMA -SONGEA

                                 Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi SHUKURU KAWAMBWA

Saturday 7 September 2013

WAKATI NI WAKO WA KUIPIGIA KURA DEMASHONEWS IWEZE KUNYAKUA TUZO

Mpendwa msomaji tunashukuru kwa mapendekezo kupitia kura zako, hatimaye blog hii ya ww.demashonews.blogspot.com imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea tuzo ya THE BEST GENERAL BLOG, Tunakuomba hivi sasa uipigie kura blog hii ili iweze kuchukua tuzo hiyo. 

Ili kupiga kura yako tafadhali bonyeza link hii  the best General Blog na uchague palipoandikwa demashonews.blogspot.com

Asante kwa ushirikiano wako, piga mara nyingi uwezavyo

Wednesday 4 September 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MKEWE MAMA SALMA KIKWETE WASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU MKUU WA KANISA LA EAGT MAREHEMU DR. MOSES KULOLA

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho na kuweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Muasisi na askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Marehemu Dkt. Moses Kulola wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika katika viwanja vya kanisa huko Bugando Mwanza leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bibi.Elizabeth Kulola mjane wa Marehemu Askofu Dkt.Moses Kulola,aliyekuwa muasisi na Askofu Mkuu wa Kanisa laEAG(T) wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika viwanja vya kanisa huko Bugando Mwanza leo. 
Picha na  Freddy Maro - Ikulu

Tuesday 3 September 2013

NDOA MBILI ZILIFUNGWA KWA SIKU MOJA KATIKA KANISA KATOLIKI MATOGORO SONGEA -RUVUMA

                                                       Father Mlelwa aliyefungisha ndoa hizo
                                               Fransis Haule na jacline Musa
                                       Hapa ni katikapicha ya ukumbusho baada ya kufunga ndoa
      Shangwe zinapozidi  basi maharusi hubebwa mgongoni hii ni ndoa ya BENEDICTO na DOMITILA
                                       Maharusi wanatoka nje  kuelekea ukumbini
                                                        Hongereni sana Fransis na Jacline

CHRISTINA MAHUVE AKIINGIA UKUMBINI HUKU AKIRUSHA PIPI KWA WALIOUDHURIA KATIKA SHEREHE YA SEND OFF


                                              HAPA AKIWA NA MPAMBE WAKE
                                             HAPA ANAMPA KEKI MJOMBA WAKE

Monday 2 September 2013

WANAJUMUIYA YA MTAKATIFU YAKOBO MTAA WA MTAKUJA BOMBAMBILI SONGEA WAKIADHIMISHA MISA YA SHUKURANI YA MAZAO




                                          PADRE SIMON NDUNGURU AKITO MAHUBIRI

                                          PADRE SIMON NDUNGURU AKIBARIKI MAJI

TUPE MAONI YAKO