Thursday 30 October 2014

MAMA TUNU PINDA ALIPOTEMBELEA RUVUMA KUZUNGUMZA NA WANAVIKOBA NA HAPO NI KATIKA VIWANJA VYA MAJIMAJI AKIPOKEA MAANDAMANO









UPEPO MWINGINE BWANA NOUMA

UPEPO mkali uliozuka katika Kijiji cha Molandi kilichpo katika Kata ya marimba Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma Umeezua Nyumba 10 na kuziacha familia hizo zikiwa hazina makazi.

Aidha taarifa za awali zinaeleza kuwa katika tukio hilo upepo huo umeezua nyuma 7 za bati na nyumba 3 zilizotuku zimeezekwa kwa nyasi na umesababisha hasara ya kumla ya Shiringi Milioni 11.925,000.
Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa zuruba hilo liliwakumba wakazi wa Kijiji hicho Oktoba 12 mwaka huu majira ya saa 7 mchana na kuzusha taharuki kubwa kwa wakazi wa kijiji hicho.

 Taarifa hiyo inafafanua kuwa Sambamba na tukio hilo pia upepo huo ilisomba moto ambao ulisababisha ungua kwa nyasi zilizotuka kuezekea baadhi ya nyumba pamoja na kuunguza uwanja wa timu ya Kijiji hicho ya Nyuki Fc.
Akiongea kwa njia ya simu Diwanai wa wa kata hiyo Bw. Msenga Saidi alidhibitisha kutokewa kwa tukio hilo na kuongeza kuwa kufutia tukio hilo wahanga kutoka katika kaya hizo hivi sasa wanahidhiwa katika nyumba za majirani ambao nyumba zao zilinusulika.

Bw. Msenga aliwataja wahanga wa tukio hilo kuwa ni Bw. Omary Jafari Mchali, Abdalah Said Manjolo, Abdalah Halifa Limbanga na Mohammed Omary Mangwila.

 Kwamujibu wa diwani huyo wahanga wengine ni Said Omari Yazidu, Ommari kazembe Nangwale,Mohammed Kazembe Nangwale, Mohammed Makunganya Mohhammed Juma wandale 

 Nae mwenyekiti wa kamati ya maafa,ulinzi na usalama Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Chande Nalicho pamoja na mambo mengine alisema kuwa baad ay atukio hilo kamati yake iliwatembelea wahanga hao na kuwapa pole.
Alisema wakiwa katika eneo hilo pia walizungumza na wahanga hao pamoja na kuwapatia ushauri wa kufuata hatua za ujenzi imara wa nyumba zao pamoja kupanda miti ya kujikinga ma majanga ya aina hiyo.
Mwisho

SAKAMIMBA TUNDURU MARUFUKU

SERIKALI Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma imepiga marufuku ngoma za Usiku ambazo zimekuwa zikichezwa na watoto wa Kike maarufu kwa jina la SAKAMIMBA.

Sambamba na marufuku ya ngoma hizo pia jamii imeaswa kuachana na utaratibu wa mila potofu za kuwacheza jando na unyago watoto wenye umri mdogo ili kuendelea kulinda maadili ya destuli za mwafrika. 
Aidha taarfa hiyo pia imewataka watendaji wa vijiji,kata na maafisa tarafa kuratibu, kusimamia na kuzuwia shughuli za Sherehe ambazo zitakuwa hazizingatii maadali katika maeneo yao.

Hayao yalisemwa na Mkuu wa Wilayab ya Tunduru Bw. Chande Nalicho wakati akiongea na wananchi wa Kijiji cha songambele kilichopo katika tarafa ya Nakapanya wilayani himo na akawataka wananchi kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinaratibiwa na kutekelezwa kwa Watoto wenye umri mkubwa ikiwa ni tofauti na sasa ambapo wazazi na walezi hao wamekuwa wakiwacheza wakiwa na umri mdogo.

Akifafanua taarifa hiyo dc, Nalicho alisema kuwa mtindo wa wanafamilia hao kuwapeleka na kuwacheza unyago kwa watoto wa kike na jando kwa watoto wa kiume wakiwa na umri mdogo umekuwa ukidhalilisha utamaduni wetu.
Alisema kwani baada ya watoto hao wenye umri mdogo baada ya kumaliza mafunzo hayo huenda kutoa siri za mafunzo hayo kwa wenzao na kufanya majaribio kwa vitendo mambo yote waliyojifunza.

“mafunzo hayo ni hatari na nijanga kubwa hasa kwa watoto wa kike ambao baada ya kumaliza mafunzo hayo huenda kufanya majaribio kwa vitendo mambo yote waliyojifunza” alisema Dc, Nalicho.
Alisema kufuati jamii kuendelea kupuuza taratibu za kutekeleza wajibu wao katika malezi ya Watoto wao hasa wakike vitendo hivyo ndivyo ambavyo vimekuwa vikipelekea watoto wa kike kupata mimba wakiwa katika umri mdogo.
Mwisho
Wanafunzi  130 wa shule ya sekondari MBUNGA iliyopo katika kijiji cha NAIKESI kata ya KITANDA katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Wameshindwa kumaliza kidato cha nne kwa kukatisha masomo yao kutokana na kupata mimba na utoro na kifo na kukariri darasa.

WATEJA WA NMB TAWI LA SONGEA WALIOJISHIDIA BAISKELI KATIKA SHINDANO LA WEKA NA USHINDE








Sunday 31 August 2014

WAKAZI WA TUNDURU WAHIMIZWA KUSHIKAMANA BILA KUJALI ITIKADI ZA DINI ZAO ILI KUJILETEA MAENDELEO.







CHAMA cha mapinduzi Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma kimewataka waumini wa Dini kuachana na tabia za kubaguana kutokana na tofauti hizo na badala yake waunganishe nguvu zao bila kujali uwepo wa itikadi za dini zao ili kuendana sawa na maandiko ya vitabu vitakatifu.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) wilayani humo Sheikh Ajili Kalolo wakati akiongea katika uzinduzi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya itakayo milikiwa na waumini wa Dini ya kiislamu ya Islamiki High School na kwamba mbali na tofauti za dini ya kiislam na kikristo, vitabu vyake havizungumzii kubaguana.

Sheikh Kalolo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema kuwa  vitendo na tabia za utengano na ubaguzi ni adui mkubwa ambaye anarudisha nyuma hatua za maendeleo zinazo dhamiliwa kufanywa na taasisi au jamii yoyote kote duniani.

Aidha Sheikh Kalolo aliwaomba watu na taasisi mbalimbali kujitoa katika kusaidia ujenzi wa shule hiyo na kuifanya ianze kutoa huduma iliyodhamiliwa kufanywa kwa wakati na kuwawezesha vijana kusoma elimu dunia na elimu ya dini na akatumia anafasi hiyo kuwapongea wahisani waliokubali kuijengea taasisi hiyo jengo la utawala, na darasa moja.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa Shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha sita, Ustadh Maulid Juma alisema kuwa kwa awamu ya kwanza ujenzi wa shule hiyo umepanga kughalimu jumla ya Shilingi Milioni 350 na kwamab fedha hizo zinatarajiwa kutokana na michango ya waumini wa dini hiyo. 
  
Alisema kwa kuanzia tayari waumini hao wemefanikisha kuchangia fedha ambazo zimeisaidia taasisi hiyo kumiliki na kupimiwa eneo la ardhi lenye ukubwa wa hekta 30, kukusanya vifaa mbalimbali vilivyo pangwa kutumika katika ujenzi huo na kufatua tofari zaidi ya laki Tatu.

Akitoa ufafanuzi baada ya taarifa hiyo katibu wa Ujenzi wa shule hiyo Sheikh Mohammed Chingwalo alisema kuwa kamati yake imepanga kuanza na ujenzi wa Madarasa Matatu, Nyumba mbili za Walimu pamoja, jengo la Utawala na Mabweni mawili hali ambayo itawezesha shule hiyo kuanza kufanya kazi kwa kusajiri wanafunzi kuanzia mhura wa masomo mwaka 2016/2017. 

Alisema katika kuhakikisha kuwa ujenzi huo ujenzi huo umepangwa kukalika mwaka 2019 ambapo shule hiyo itaanza kuchukua wanfunzi wa kidato cha tano na sita katika mikondo miwili ya masomo ya Sanaa na Sayansi.

Wakiongea kwanyakati tofauti mwenyekiti wa Baraza la waislamu Tanzania Wilayani humo Shekhe Ndawambe Salum, mwakirishi wa maustadh Sheikh Husein Mahusein pamoja na mwakirishi wa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Sheikh Athuman Nkinde pamoja na mambo mengine waliwahimiza waumini wa dini hiyo kuunganisha nguvu zao ili kuharakisha ujenzi wa shule hiyo.

‘’ ili kuiwezesha shule yetu kuyafikia mafanikio na kuiwezesha kuanza kutoa huduma kwa haraka inafaa tupendane,  tuunganganishe nguvu zetu bila kujali itikadi za imani wa dini zetu” alisisitiza Shekih Ndawambe.

Akitoa taarifa za maendeleo ya elimu Wilayani humo mwakilishi wa mafisa elimu wa Shule za msingi na Sekondari Mwl. Abudul Kazembe pamoja na kuwapongeza kwa juhudi za ujenzi wa shule hiyo aliwataka wazazi na walezi wa watoto kuondokana na tabia ya kuwakataza watoto wao kwenda shule pamoja na mazuwio ya kuwakataza kunya zizuri katika matokeo ya mitihani yao yakumaliza darasa la saba .

Mwl. Kazembe aliwatahadharisha kuwa endapa hawata timuza wajibu wao katika kuhamasisha na kusiamaia maendeleo ya elimu ipo hatari ya juhudi hizo kutozaa matunda kwani baada ya kukamilika kwa majengo hayo hawataweza kuwapata wananfunzi wenye sifa za kwanda kusoma katika shule yao. 

IMEANDIKWA NA STEVEN AUGUSTINO - TUNDURU



WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI MAPOSENI, DARAJA MBILI, NA NAMIHOLO KATIKA MJI WA PERAMIHO WAKIJADILI MCHANGO WA RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA SEKTA YA ELIMUE KATIKA SEKTA YA ELIMU










Saturday 30 August 2014

AJALI YA GARI KUGONGA PIKIPIKI KATIKA MJI MDOGO WA PERAMIHO PICHA ZOTE NA OSWALD NGONYANI

                                       GARI LILILOGONGA MUENDESHA PIKIPIKI
                                                   MASHUHUDA WA AJALI HIYO
                      KIJANA ALIYEGONGWA AKIWA AMELALA CHINI NA KUUMIA MGUU

WAFANYAKAZI 45 WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU WANUSURIKA KUFA BAADA YA BASI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUPINDUKA.


ZAIDI ya Wafanyakazi 45 wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoni Ruvuma wamenusulika kufa baada ya Basi lenye namba za usajiri T 966 AXQ mali ya  kampuni ta Ng’itu Expres walilokuwa wakisafiria kupinduka.

Sambamba na tukio la ajali hiyo taarifa zinaeleza kuwa watu wane (4) wamejeruhiwa kutokana na kuumia sehemu mbalimbali za miili yao  kukimbizwa katika Hospitali ya serikali ya Wilaya ya Tunduru.

Wakiongea kwa njia ya simu baadhi ya manusula hao walisema kuwa ajali hiyo ilitokea katika eneo la Lumesule mpakani mwa Wilaya zaTunduru Mkoni Ruvuma na Mangaka Mkoani Mtwara.

Kwamujibu wa taariha hizo watumishi hao ambao walifuatana na wakuu wao wa idara walikuwa wana kwenda Wilayani Masasi Mkoani Mtwara kwa ajili ya kushirki katika Mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa hamalshauri yao Marehem Robert Nehatta.

Akifafanua taarifa za tukio hilo Dkt. Jacob Madondola ambaye ni kati ya manusula hao alieleza kuwa mbali na gari hilo kuwa katika mwendo kasi chanzo cha ajali hiyo kilisababishwa na kuchomoka kwa Stelingi na kumshinda dereva.

 Katika taarifa hiyo mashuhuda hao waliwataja watu waliojeruhiwa kaatika ajali hiyo kuwa ni Bw. John Kamwela (afisa Biashara wa Halmashauri hiyo), Bi. Malisela Mapunda(afisa manunuzi wa halamsahauri hiyo), Mwl. Joseph Makina ( msaidizi wa afisa elimu wa Shule za Sekondani Wilayani humo) pamoja na Bw.Joseph Mtauchila (Mkaguzi wa ndani).

Mganga mfawidhi katika Hospitali ya Wilaya Dkt. Joseph Ng’ombo amekiri kuwapokea majeruhi hao na kuwapatia matibabu na kwamba halizao zinaendelea vizuri. 

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya Simu, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho  ametoa pole kwa wahanga hao alisema kuwa ajali hiyo imetokea katika mazingira ya uzembe wa wamiriki wa gari hilo kutolifanyia uchunguzi wa kina wa mara kwa mara.

Alisema Maremu Robert Nehatta alifariki Dinua usiku wa kuamkia Agost 26 mwaka huu akiwa katika Hospitali nchini India ambako alienda kwa ajili ya matibabu ya Figo yaliyokuwa yakimsumbua.

TUPE MAONI YAKO