Monday 8 July 2013

NJIA TANO ZA KUPUNGUZA TUMBO


WAMAWAKE wengi wanatamani kuwa na matumbo madogo, lakini wengi hushindwa kufikia ndoto hiyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za uzazi na kupenda chakula. Makala hii inaangalia njia rahisi ya kupunguza tumbo.
1. Uangalifu katika kula
 

Epuka chakula chenye wanga, mafuta mengi na sukari. Badala yake unaweza kula matunda na mboga za majani. Vile vile samaki wa baharini si wabaya kwani hawana mafuta mengi.
2. Namna ya kula
 

Usiache kula kwani jambo hilo litakunyima nguvu, unatakiwa kula milo mitatu mpaka minne lakini kwa kiasi kidogo. Unatakiwa kukaa zaidi ya saa tatu kabla ya kula mlo mwingine.
3. Mazoezi ya kawaida
 

Sio lazima ufanye mazoezi makali kwa ajili ya kupunguza tumbo. Unaweza kufanya zoezi la kutembea badala ya kupanda basi, kama hufiki mbali sana. Kama unaweza kuogelea, unaweza kufanya hivyo mara kwa mara, hiyo pia itakusaidia.
4. Zoezi maalum
 

Kama unaweza kufanya zoezi la kulala chali na kukaa, 'abs exercise' unaweza kufanya kwa dakika chache kila siku. Hiyo itasaidia kukomaza misuli ya tumbo hivyo tumbo kutokulegea.
5. Kunywa maji
 

Maji yanasaidia mmeng'enyo wa chakula, hilo husaidia mtu kuwa na afya njema. Kwa kuwa mtu akiwa katika hatua za awali za kupunguza tumbo husikia njaa mara kwa mara, ni bora anywe maji badala ya kula.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO