Tuesday 30 April 2013

Hotel ya Double by hilton Tanzania watoa msaada wa taa 200 kwa shule za Msingi Songea- Ruvuma

Waziri wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika akiipongeza  Hoteli ya DoubleTree by Hilton kwa kuona umuhimu  wa elimu kwa kukabidhi taa mia mbili kwa Shule za Msingi zilizopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma , Shule zilizopewa msaada huo ni Shule ya msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang'ula , Taa hizi  zinazotumia Nishati ya jua pia ni rafiki wa mazingira.
" Taa hizi zitawasaidia kuepeuka kutumia vibatari na mishumaa muda wa kujisomea kwa sababu ni hatari kwani vimekuwa vikisababisha majanga ya kuungua kwa watoto wengi nchini ".
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joesph Joseph Mkirikiti alie kaa katikati na kutoka kulia kwake ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by Hilton  Tanzania Bw. Judd Helman na alie kaa kushoto ni mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata wakati wa hafula ya kukabidhi msaada wa taa zinazotumia nishati ya jua.
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph mkirikiti akiteta jambo na mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata (kushoto) juu  ya matumizi ya taa zinazotumia nishati ya Jua ambazo pia ni rafiki wa mazingira kwa Wanafunzi wa darasa la Saba. Kulia ni  Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by Hilton  Tanzania Bw. Judd Helman .
Toka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata akiwa ameshikilia taa na wakatikati ni mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph mkirikiti  akiwa ameshikilia taa na wa mwisho ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Judd helman
 Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Judd helman akimkabidhi moja ya taa inayotumia nishati ya Jua mwanafunzi wa Shule ya Msingi Liumbu iliyopo ndani ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma .
Waziri wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika hapa ni umati wa wanafunzi (Viongozi wa leo)  kila mmoja akitaka ampe mkono wa pongezi baada ya kumalizikla hafla ya kukabidhi taa za nishati ya jua kwa shule nne za manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
Wanafunzi  toka  katika shule nne za msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang'ula na  wakifatilia kwa makini hutuba iliyokuwa ikitolewa kabla ya  kukabidhiwa taa zinazotumia Nishati ya jua ambazo zimetolewa na Hoteli ya DoubleTree by Hilton. 

Wanafunzi hao wameishukuru Hoteli hiyo na kusema taa hizo zitawasaidia kujisomea hata kipindi ambacho Umeme umekatika majumbani hivyo kuongeza uwezo wao kielimu na kupunguza matumizi ya kununua mafuta ya taa kwa ajili ya kusomea

Naye Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata amesema
"tumeamua kufanya kampeni hii ambayo ni endelevu tutakuwa tukigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira vile vile tunaomba wahisani wengine nao wajitokeze".


Chanzo: www.demashonews.blogspot.com

Sunday 28 April 2013

AJALI MBAYA YA MPOTEZA MTUMISHI WA MUNGU.



                Hili ndilo gari ambalo  limesababisha  kifo cha paroko ( picha na Gogers Stivin Mselu wa FG Blogu Mafinga)
             A
PAROKO  wa kanisa la RC parokia ya Ifunda Alphonce Mhamilawa amefariki  dunia katika ajali mbaya ya gari  iliyotokea katika eneo la Saba  saba Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Mashuhuda  wa  ajali  hiyo wameeleza kuwa ajali  hiyo ilitokea  majira ya saa 2 usiku  wa  kuamkia  leo wakati paroko  huyu akitoka mkoani Njombe katika  shughuli  ya Mazishi

Mmoja kati ya mashuhuda  hao Bw  Saugo Ndemo  alisema  kuwa paroko  huyo alikuwa akiendesha gari dogo Paina ya Toyota  Hilux (Pick Up) yenye  namba  za usajili  T434 APP mali ya Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Ifunda.

Ndemo  alisema  kuwa chanzo  cha ajali  hiyo ni Paroko  kuligonga gari aina ya Lori  kwa  nyuma na kuwa lori  hilo halikuweza  kusimama .

Alisema  kuwa  paroko  huyo alifia eneo la tukio baada ya  ajali  hiyo  iliyopelekea  kichwa  chake  kupasuka .

Mmoja kati ya askari  wa usalama barabarani ambae hakutaka  kutaja jina lake kwa  kuwa si msemaji  mkuu  wa  jeshi la  polisi alisema  kuwa  chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi.

Pia alisema   kuwa lori ambalo  paroko  huyo aliligonga  linasadikika  kuwa lilibeba mbao huku  likivutana na  lori  jingine na baada ya ajali  hiyo halikuweza  kusimama.

Mkuu wa mkoa Ruvuma azipongeza halmashauri kwa kupata hati safi

Mwisho.

Watoto wa ukoo mmoja wa MSIGWA wakutana kujadili mikakati ya maendeleo ya familia zao

    Mama irene mwenyeji wa mahali mkutanno ulipofanyika akiwakaribisha wajumbe chakula


                                                                     Kazi na dawa






                                                               hapana chezea njaa



          Majira ya saa nane usiku bado mjadala ni mkali kwa wale wanaofanya mchezo na maisha.

Saturday 27 April 2013

MBUNGE LEMA WA ARUSHA ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI

Na Mahmoud Ahmad, Arusha
  Jeshi la polisi mkoani hapa limemtia mbaroni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mhe Godless Lema kwa tuhuma za uchochezi kwa wanafunzi kwenye chuo cha uhasibu mwanzoni mwa wiki katika vurugu zilizotokea chuoni hapo baada ya mwenzao kuuwawa juzi usiku huko maeneo ya njiro jijini hapa.
 
Kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa Mhe Lema  alikamatwa huko nyumbani kwake Njiro majira ya saa 9 usiku. 
 
Afande  Sabas alisema jeshi hilo linaendelea na mahojiano na mtuhumiwa na kuwa katika tukio hilo zaidi ya watuhumiwa 14 walifikishwa mahakamani jana na kuwa hao hawezi kuwaongelea kwani kesi yao ipo kwenye chombo hicho cha sheria. 
 
 Pia kamanda Sabas alisema kuwa Mh Lema anashikiliwa kutokana na vurugu zilizotokea juzi kwenye chuo cha uhasibu na kuwa atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu.
Kwa upande mwengine Kamanda Sabas  alisema kuwa zaidi ya hao watu 14 na Mhe. Lema hakuna mtuhumiwa mwingine aliyakamatwa. Awali ilisemakana wakili wake Albert Msando nae amekamatwa.
 
 Mnamo siku ya Jumatatu mwanafunzi mmoja aliuwawa kwenye mitaa ya Njiro jijini Arusha na watu wasiojulikana hali iliyoleta tafrani hadi wanafunzi hao walipoleta vurugu chuoni hapo na polisi kutumia mabomo ya machozi kuwatawanya.
 
Sekeseke hilo lilimalizwa na jeshi la polisi baada ya wanafunzi kutotii amri ya mkuu wa mkoa huo Magessa Mulongo na kuanza kuingia barabarani kuandamana.

GARI LITAKALOGOMBANIWA MEI MOSI KATIKA MPAMBANO WA NDONDI KATI YA FRANCIS CHEKA NA THOMAS MASHALI

  Picha kutoka kapingaz blog.

Msemaji wa mpambano wa Thomasi Mashali na Fransic Cheka akiwa nyuma ya gari kuwaonesha wana habari gari hilo litagombaniwa kama zawadi na mabondia hao

RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO AKAGUA GWARIDE

1      Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama lililoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam 2

Thursday 25 April 2013

WANACHUO CHA UALIMU SONGEA WASHEREKEA MAHAFALI YA 17


                                                       Moses Msigwa akivishwa taji
                                   Kushoto ni Moses Msigwa na dada yake katika picha ya ukumbusho
                                                                       Hongera Moses
                                                                      Wahitimu
                                                                     Wamependeza
                                                                       pozi hilo


Wanachuo wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika mahafali ya 17 ya chuo hicho. Changamoto kubwa ikiwa ni uchakavu wa ukumbi wa kulia chakula.

WANACHUO 575 WA CHUO CHA UALIMU SONGEA WAHITIMU

Kulia ni MOSES MSIGWA akiwa na wanachuo wenzake baada ya kupata zawadi ya kuhitimu chuo.

Wednesday 24 April 2013

WILAYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA YABAINI VIKWAZO VYA ELIMU






Na Steven Augustino, Tunduru
 

Imebainishwa kuwa Mahusiano mabaya kati ya Walimu na Wanafunzi na
Wanafunzi wadaiwa kukataa kukaa katika mabweni na Hosteli ni miongoni
mwa vikwazo vya maendeleo ya elimu Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na
kupelekea Wilaya hiyo kupata matokeo mabaya kwa wanafunzi waliofanya
mitihani ya Kidato cha Pili Nne katika kipindi cha mwaka 2011/2012 .
 

Hayo yalibainishwa na afisa elimu Sekondari Mwl. Ally Mtamila wakati
akiwasilisha taarifa ya matokeo ya kidato cha pili na cha Nne
katikakipindi cha mwaka 2011/2012 kuongeza kwa kuwataka wzazi
kushiriki katika usimamiaji wa Watoto wao kuwa nma hamasa ya kupenda
masomo pamoja na kukemea watoto wanaokwepa kuingia darasani ambao
wamekuwa wakiachwa waendelee kucheza wakati wenzao wakiwa darasani
zikiwa ni juhudi za kuinua taaluma kwa watoto wao.
 

Kwa mujibu wa tarifa hiyo mwaka 2011 matokeo ya Kidato cha pili Wilaya
hiyo ilifaulisha kwa wastani wa asilimia 35%, huku takwimu hizo kwa
upande wa matokeo ya Kidato cha Nne katika kipindi cha mwaka 2012
zikionesha kuwa Wilaya hiyo ilifaulisha kwa wastani wa asilimia 59.46%
kiwango kilichodaiwa kuwa ni kidogo na kiliifanya Wilaya yao kushika
nafasi ya mwisho kimkoa.
 

Awali aikifungua Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru  Chande Nalicho
pamoja na kubainisha kuwa pamoja na serikali kuwa na vipaumbele
vingine vya maendeleo lakini Elimu ni muhimu ilikujiletea mabadiliko
ya kweli.


 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Nalicho aliendelea kueleza kuwa Ili kuwaletea maendeleo wananchi wa
Tdr ni lazima wilaya ijikite katika kusimamia elimu na kuhalalisha
uwepo wao na kwamba wasipo wakazania kusomaa shuli maendeleo
yanayopiganiwa na serikali hayatakuwa na maana yoyote kwao.
Katika taarifa hiyo Mkuu Dc. Nalicho akatolea mfano wa Takwimu za
ufaulu wa wanafunzi 2764 waliochaguliwa kujiunga na masomo ya
sekondari  hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu ni asilimia 60% ya  watoto
wote waliochaguliwa  kujiunga na masomo ya sekondari.
 

 Akizungumzia upande wa Shule za Msingi  Mwaka 2011Shule ya Msingi
Nakapanya ilifaulisha Watoto 26 lakini takwimu zinaonesha kuwa  watoto
wote hawakwenda shule na kuongeza kuwa hali hiyo inawakatisha tama
hata walimu wa shule za msingi zinazofaulisha watoto hao Serikali
inayo mikakati
 

Wakichangia kwa nyakati tofauti Mwl. Issa Ngajime alisema kuwa chanzo
cha kushamiri kwa utoro,uchangiaji hafifu wa chakula mashuleni na
wanafunzi kukataa kukaa katika hostel zilizojengwa katika shule zao
Viongozi wa serikali za Vijiji wanastahili kubeba lawama huku
wakiwataka viongozi kutochanganya elimu na Siasa kwa kuboresha mbinu
za kufundishia na kuchukua hatua kwa Wanafunzi ambao wamekuwa
wakibainika kuchaguliwa wakiwa hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu.
 

 Mkuu wa shule ya Mgomba Mwl. Elis Banda alisema kuwa tatizo wanafunzi
kukataa kukaa katika Hosteli linatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya
watoto wanaosoma katika shule hizo kuwa ni wakazi wa maeneo husika na
akapendekekeza kuwepo kwa utaratibu wa kutenga Shule za kanda kwa
ajili ya kupeleka wanafunzi kutoka maeeneo tofauti huku akiitaka
serikali kutoa maelekezo ya vitabu vya kununuliwa tofauti na sasa
ambapo kumekuwa na maelekezo ya kuwataka wakuu wa shule kutumia vitabu
kutoka katika kampuni ya EMACK  ambapo alishauri kupunguzwa kwa idadi
ya vitabu vya kufundishia.
 

Wadau hao waliendelea kubainisha vikwazo vingine kuwa ni pamoja na
Muingiliano wa sekula pia ni kikwazo cha Willaya kufanya vizuri kwani
sasa wanalazimishwa kusajiri watoto wote kufanya mitihani bila
kuangalia wakati huo mamlaka zikiwataka walimu kuwafukuza watoto
wasiofika shule katika kipindi cha miezi mitatu  huku serikali wakati
huo ikihamasisha na kuwapeleka shule wanafunzi wa kidato cha kwanza
walichelewa kuripoto Shuleni ni kikwazo kingine ambacho kimekuwa
kikiwafanya walimu kufundisha kwa kulipua na kushindwa kulamiza
silabasi.
 

Ujauzito pia tatizo lakini Bodi za shule zimekuwa zikifanya kazi ya
ziada lakini kila wanapofuatilia matokeo ya kesi Polisi huwa
hawapatiwi majibu ya maendeleo ya kesi husika hali inayo wakosesha
imani.
 

Mkuu wa Shule ya sekondari Lukumbule Mwl. Mathias Katto akabainisha
vikwazo vingine kuwa shule zao kutokuwa na walimu wa masomo ya
Sayansi,Shule kutokuwa na maktaba,Watoto kutoka katika maeneo husika
na miundombinu ya Nyumba wanazoishi n imbovu zinvuja na kwamba siyo
rafiki kwa Walimu.
 

Marafiki hao wa elimu pia wakanyooshea kidole mila na destuli potofu
za kuwafundisha watoto wadogo hasa wa kike mafunzo ya kuishi kiunyumba
ambayo hutolewa kupitia katika jando, Unyago
na Msondo na ngoma ya Sakamimba hali ambayo imekuwa ikipelekea baadhi
ya wanafunzi kuishi kwa wanaume huku wakiwa wanaendelea na masomo.
Mwisho

Monday 22 April 2013

Soma Kwa Makini Baadhi ya Dondoo Za Bajeti Ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika iliyosomwa Bunge Mjini Dodoma Leo Ambayo Serikali itatumia Shilingi 328,134,608,000/-Mwaka Ujao Wa Fedha.

 

  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza
--
 KILIMO KUTUMIA SHS. 328,134,608,000 KATIKA MWAKA WA FEDHA UJAO
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika inatarajia kutumia jumla ya shilingi 328,134,608,000/- katika mwaka ujao wa fedha.

Takwimu hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza wakati akiwasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2013/14.

Alisema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi 247,094,320,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya kawaida na Shilingi 81,040,288,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya maendeleo.

Chiza aliongeza kuwa  Shilingi 210,175,943,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengine (OC) kwa ajili ya Wizara hiyo .

Aidha ,shilingi 25,602,969,000 ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Wizara na Shilingi11,315,408,000 ni Mishahara (PE) ya Bodi na Taasisi zote zilizoko chini ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Kwa upande shughuli za maendeleo, Chiza alisema kuwa Wizara hiyo imetenga kiasi cha shilingi 23,927,000,000 ikiwa ni fedha za ndani na shilingi 57,113, 288,000 ni fedha za Nje.

Wabunge wanatarajia kujadili bajeti ya Wizara ya Kilimo , Chakula na Ushirika kwa kipindi cha siku mbili ambapo itahitimishwa kesho.

Katika hatua nyingine Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhe. Chiza amesema Serikali inatarajia kufufua Kituo cha Kilimo Anga ili kukiwezesha kuwa na ndege na Wataalam watakaosaidia kudhibiti milipuko ya visumbufu vya mazao hasa Nzige.

Mhe. Chiza amesema kwa kiasi kikubwa Serikali imekuwa ikitegemea huduma ya ndege kukodi kutoka kwenye mashirika ya kikanda ya kudhibiti nzige wekundu na nzige wa jangwani ambazo wakati mwingine hazipatikani wakati zinazohitajika.

Kufuatia hali hiyo amesema Wizara katika mwaka wa fedha 2012/13 imekamilisha viwango vya kiufundi (Technical Specifications) kwa ajili ya kutangaza zabuni ya ununuzi wa ndege moja ya kunyunyuzia viuatilifu.
---

SERIKALI ITAENDELEA KUWAENDELEZA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO NCHINI

SERIKALI inatekeleza mkakati wa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini kwa kuwatambua wao na mahitaji  ya mitaji na vifaa ili kutekeleza kazi yao kwa ufanisi.

Kauli hiyo imetolew na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Julius Masele wakati akijibu swali na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani leo mjini Dadoma aliyetaka kujua ni lini wachimbaji wadogo wadogo wa Ng’ombeni, Kalalami, Kigwase watatambuliwa na Serikali na kupewa kipaumbele kwenye uchimbaji, na kupewa mikopo ya kujikimu wakati wakitafuta Madini.

Amesema kuwa katika kutambua umuhimu wa wachimbaji wadogo wadogo Wizara hiyo imeshakwishatoa imetoa jumla ya viwanja 612 vya uchimbaji mdogo wa madini katika maeneo ya Ng’ombeni, Kalalani na Kigwase ikiwa ni hekta 3,864. 

Aidha, Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa na Wakala wa Jiolojia inaendelea kubainisha maeneo yanayofaa kwa uchimbaji mdogo ili yaweze kutengwa kisheria na kugawiwa kwa wachimbaji hao.

Masele alisema kuwa katika utekelezaji wa mkakati huo unashirikisha wachimbaji wenyewe kwa kuimarisha vyama vyao vya kimkoa na chama cha kitaifa (FEMATA) na kujadili masuala yao katika vikao vya pamoja vya kila baada ya miezi sita baina ya wawakilishi wao na Wizara.

Ameongeza kuwa Wizara ya Nishati na Madini inakamilisha taratibu za Mfuko rasmi wa kuwaendeleza wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kupata mikopo ya vifaa vya uchimbaji wenye tija.

Aidha , Naibu Waziri huyo amewasisitiza wachimbaji wadogo wadogo kuwa mikopo hiyo wanayopata inapaswa itumike vizuri katika malengo waliyoombea ili wajihakikishie kuzalisha madini mengi na kujiongezea kipato.
--

UDHIBITI WA VISUMBUFU VYA MAZAO

SERIKALI itafufua kituo cha Kilimo Anga kwa kukiwezesha kuwa na ndege na Wataalam ili kujenga uwezo wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Masoko kudhibiti milipuko ya visumbufu vya mazao hasa Nzige.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza wakati akiwasilisha Bungeni Makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo leo.

Mhe. Chiza amesema kwa kiasi kikubwa Serikali imekuwa ikitegemea huduma ya ndege kutoka kwenye mashirika ya kikanda ya kudhibiti nzige wekundu na nzige wa jangwani ambazo wakati mwingine hazipatikani wakati zinazohitajika hali ambayo husababisha Wizara kutegemea kukodisha ndege kutoka sehemu nyingine.

Amesema Wizara katika mwaka wa fedha 2012/13 imekamilisha viwango vya kiufundi (Technical Specifications) kwa ajili ya kutangaza zabuni ya ununuzi wa ndege moja ya kunyunyuzia viuatilifu.

Aidha, Wizara itaweka utaratibu wa kuingia ubia na makampuni binafsi na taasisi zinazotoa huduma kama hizo ili kukijengea uwezo kituo cha Kilimo Anga.

Wakati huo huo, Wizara ya Kilimo, Ushirika na Chakula ilisambaza lita ,6000 za kiuatilifu cha kudhibiti milipuko ya viwavijeshi katika mikoa ya Rukwa, Katavi, Mbeya, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Geita. Dodoma, Morogoro na Tanga kunusuru hekta 16,418 za mazao ya nafaka.
---

SERIKALI IMEFANIKIWA KUONGEZA WATAALAM WA KILIMO NCHINI HADI KUFIKIA 7,974

Wataalam wa ugani wameongezeka kutoka 3,379 waliokuwepo mwaka 2007 hadi kufikia 7,974 mwezi Juni jana(2012) baada ya Serikali kuajiri wahitimu kutoka vyuo mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Adam Kighoma Malima wakati akijibu swali Mhe. Mch. Dk. Getrude Rwakatare (Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi).

Amesema kuwa mwaka 2007 Serikali ilifanya tathmini ya upatikanaji wa huduma za ugani nchini na kubaini kwamba mojawapo ya vikwazo vikubwa vya upatikanaji wa huduma za ugani kwa ufanisi nchini ni upungufu mkubwa wa wataalam.

Malima ameongeza kuwa matokeo ya tathmini hiyo yalionyesha kuwa kulikuwepo na wataalam 3,379 nchini ikilinganishwa na mahitaji halisi ya wataalam 15,082.

Amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo , Serikali ilianza kutekeleza Mpango wa kuimarisha huduma za Ugani nchini ambapo kuanzia mwaka 2007 Serikali imevifufua vyuo 13 vya kilimo nchini (MATIs) vilivyo chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.

 “Ukarabati mkubwa wa vyuo vitatu MATI Ukiriguru, Maruku na Naliendele-Mtwara na ukarabati mdogo kwa baadhi ya vyuo kumi vingine umefanyika”. Mhe. Malima alisema.

Aidha, Mhe. Malima amesema kuwa vyuo viwili vya mashirika yasiyo ya kiserikali vilishirikishwa katika kutoa mafunzo yaliyolenga kuongeza idadi ya wataalam wa Ugani na vyuo hivo kwa sasa vina uwezo wa kudahili wanafunzi 3,500 kwa wakati mmoja ikilinganishwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 600 uliokuwepo kabla ya mwaka 2007.
 
* Habari zote za Bunge na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma.

TUPE MAONI YAKO