Thursday 31 January 2013

BALOZI IIDI AWAJULIA HALI WALIONUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA JAHAZI LILILOKUWA LIKITOKEA TANGA KWENDA ZANZIBAR

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akimfariji mmoja kati ya abiria waliokua katika Jahazi la Sun Rise, Juma Ali Jaku ,  iliyopata ajali na kuzama  kati ya Tanga na Mkokotoni karibu na Mkondo wa Nungwi, ikiwa imebeba jumla ya abiria 32 kati ya hao 21 wameokolewa na 11 kati yao hadi sasa hawajapatikana. Kushoto kwa Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pemba Juma Khamis.
Nahodha wa Jahazi ya Sun Rise, iliyozama kati ya Tanga na Mkokotoni, karibu na Mkondo a Nungwi, Abdulla Saleh, akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, jinsi mkasa huo ulivyowatokea na kuzama baada ya chombo chao kupatwa na dhoruba kali.
**************************************


Nahodha na abiria mmoja ambao ni miongoni mwa  watu 21 walionusurika kufa kati ya 32 waliokuwa wakisafiri na Jahazi lililopata ajali na kuzama liitwalo Sun Rise likitokea Mkoani Tanga kuja Mkokotoni Unguja, wakiwa katika wodi ya Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini A iliyopo Kivunge, Zanzibar wakiendelea kupatiwa  matibabu.

Jumla ya abiria 21 wameokolewa katika ajali hiyo na kupelekwa Kivunge kwa ajili ya kupatiwa huduma ya matibabu ambapo hadi sasa abiria saba watoto wakiwa watatu na watu wazima wane  bado hawajapatikana kutokana na ajali hiyo.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Viongozi wa Juu wa Ofisi yake ambayo ndio inayoratibu masuala ya maafa walifika Hospitali ya Kivunge kuwapa pole majeruhi hao waliobakiwa wakipatiwa huduma za Matibabu.

Nahodha wa Jahazi hiyo Bwana Abdulla Saleh akiwa pamoja na Majeruhi mwenzake Bwana Ali Juma Jaku alimueleza Balozi Seif kwamba ajali hiyo ilitokea kutokana na kuchafuka mara Moja hali ya Bahari.

Nahodha Abdulla alisema chombo chao chenye uwezo wa kubeba abiria 50 kiliondoka bandarini Tanga salama Majira ya Saa nane za Usiku  na walianza kupata mitihani na kuzama mara baada ya kuchafuka kwa bahari majira ya saa 11 za alfajiri.

Akiwapa pole majeruhi hao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar Balozi Seif alisema juhudi alizoonyesha Nahodha huyo katika kusaidia uokozi huo zinastahiki kupongeza na Jamii yote.

Balozi  Seif aliwaombea majeruhi hao kupoa haraka na kuungana na familia zao na kuutaka Uongozi wa Hospitali ya Kivunge kuendelea kuwachunguza Mareruhi hao kutokana na juhudi kubwa waliyoifanya ya kusaidia harakati za uokozi wa wenzao uliopelekea kupoteza nguvu nyingi.

Jahazi hilo la Sun Rise lililokuwa likitokea Tanga kuja Mkokotoni mbali ya kuchukuwa abiria pia lilibeba sanduku nne za maziwa pamoja na  Polo zipatazo 30 za Mkaa.

dr.migiro mkuu mpya chuo kikuu huria


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.

Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania. 
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM

MAELFU YA WAKAZI WA MANISPAA YA SONGEA LEO WAMEJITOKEZA KATIKA MAZISHI YA MWENYE KITI MSTAAFU WA CCM SONGEA MJINI BWANA YASINI DIZUMBA NYUMBANI KWAKE RUHIRA SEKO

Bwana Dizumba alikuwa maarufu sana katika maisha yake,katika manispaa ya Songea na Dar es Salaam pia ambako alikozaliwa na kupata elimu yake.
Katika uhai wake amewahi kufanya shughuli mbalimbali  zikiwemo za michezo, za ulazishaji mali mapoja na shughuli za Chama mpaka anaiga dunia hapo juzi katika hospitali ya Peramiho alikuwa Mwenye kiti wa CCM mstaafu.

Aidha alikuwa kiongozi wa Timu ya majmaji na ikapanda daraja,hivyo watu wengi wanamkumbuka Dizumba kutokana na umarufu wake kwa kuwa alikuwa ni mtu wa watu.
Bw.Dizumba amezikwa nyumbani kwake Ruhira Seko ( Songea Boys ) katika Manispaa ya Songea leo na maelfu ya watu waliofurika katika mazishi yake.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina.

Tuesday 29 January 2013

HATIMAYE LULU AACHIWA HURU URAIANI..MAMA KANUMBA AANGUA KILIO ...!!


Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, akishuka kutoka katika gari lililomleta leo, Mahakama Kuu wakati wa kukamilisha taratibu za kupata dhamana. 

Lulu akiingia Mahakamani huku akisindikizwa na Askari Magereza.
Lulu akiingia mahakamani, huku akitabasamu, akiwa anasindikizwa na askari Magereza.
Lulu akijificha uso, asipigwe picha na waandishi wa habari 'Paparazi' wakati akitoka nje ya Mahakama Kuu, akiwa mamepatiwa dhamana katika ombi lake alililoliwasilisha mahakamani hapo.
Lulu akiingia mahakamani kwenda kukamilisha masharti yake ya dhamana, Dar es Salaam leo.
Lulu akiangua kilio baada ya kushindwa kuongea na waandishi wa habari waliokusanyika mahakamani hapo.
Lulu akitoka katika lango Kuu la Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kupata dhamana.
Lulu akilia wakati akitoka Mahakamani huku nyumba akifuatiwa na mama yake mzazi.
Wasanii nao wallijitokeza mahakamani hapo kumfariji Lulu, kulia ni msanii wa filamu, Muhsin Awadh 'Dk. Cheni'
Lulu akiondoka mahakama hapo.
Wakili anayemtetea Lulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mteja wake kupata dhamana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo. Lulu amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali waliosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja, kusalimisha hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam  bila ruhusa ya mahakama na kuripoti kwa msajili kila mwezi.  Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Bunge launda Kamati Maalumu kwenda Mtwara

Spika wa Bunge bi Anne Makinda amesema Bunge limeunda Kamati Maalumu kwenda mkoani Mtwara kutafuta suluhu kuhusu suala la nishati ya gesi, iliyopatikana mkoani humo.

Spika Makinda ameyasema hayo wakati akiahirisha kikao cha Bunge kilichoanza leo Mkoani Dodoma.

Spika amesema matokeo ya Kamati hiyo Maalumu yatawasilishwa kujadiliwa Bungeni.

Iddi Maalim wa TBC anaripoti katika taarifa iliyosomwa saa saba mchana ifuatavyo:
Bunge sasa linaunda Kamati ambayo itakwenda Mtwara, kuwasikiliza Wananchi halafu ndani ya kikao hiki –mkutano huu unaofanyika– Kamati ya Bunge itakuwa imekwenda Mtwara, itawasikiliza Wananchi, italeta masuala ambayo yanazungumzwa kule Mtwara kisha yatajadiliwa.

Hili alikuwa analizungumza baada ya kusema kuwa amepokea vikaratasi na maombi mengi kwamba Bunge lijadili suala la Mtwara, gesi kama suala ambalo ni la dharura.

Lakini akasema kwamba, ile hoja si ya dharura na akaeleza pia ukweli kwamba Wabunge ambao wanasema lijadiliwe kama suala la dharura wengi wao hawalifahamu kwa undani, kwa hiyo badala ya kujadili jambo ambalo hawalifahamu kwa undani, ni afadhali ataunda kamati ambayo itakwenda Mtwara ikirudi itakuja na majibu, na mapendekezo ya Wananchi na ndipo Bunge litajadili ndani ya Mkutano huu wa kumi.

Zaidi ya vituo vya afya elfu moja nchini havina dawa za malaria

Asilimia 26 ya vituo 5,080 vya matibabu vya Serikali vilivyo katika mikoa 22 Tanzania Bara, havina dawa za aina yoyote za ngazi ya kwanza za kutibu malaria na kwinini ambayo hutumika kwa watu wenye malaria sugu.

Ngazi ya kwanza ya tiba ya malaria ni dawa mseto (ALu) na kwa wastani matumizi ya dawa za ALu nchini ni dozi milioni 1.3 kwa mwezi, ikimaananisha kuwa na dozi takribani 15,600,000 kwa mwaka.

Hata hivyo, taarifa zilizo katika ripoti ya Global Fund (kupitia ripoti za AMFm) Januari 1,2012 mpaka Januari 17, 2013 Tanzania iliagiza na kupokea dozi 4,917,780 kwa sekta ya umma kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa awamu nne kwa mwaka.

Dawa za kukabiliana na malaria hutolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia mradi wa msonge unaoratibiwa na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) ukifadhiliwa na wafadhili mbalimbali, hususan Global Fund, Mfuko wa Ufadhili wa Rais wa Marekani (PMI-USAID), Benki ya Dunia na wahisani wengine.

Kwa mujibu wa taarifa zilizo kwenye mtandao unaopokea taarifa za kila siku za uwepo wa dawa za malaria katika vituo vya serikali (SMS for Life) vingi ya vituo hivyo havijapokea dawa kwa siku hata 369.

Taarifa zilizotolewa na shirika lisilo la serikali linalofanya kazi ya kuboresha utawala bora, uwazi na uwajibikaji katika Sekta ya Afya na Ukimwi nchini (SIKIKA)katika mkutano na wahariri uliofanyika Dar es Salaam jana, zilisema uhaba huo wa dawa umekuwa ukitofautiana baina ya mikoa na wilaya.

Mkurugenzi wa Sikika, Irenei Kiria alisema uhaba uliopo na asilimia kwenye mabano ni Mwanza (57%), Ruvuma (53%), Mara (46%), Kigoma (43%), Shinyanga (42%) na Tabora (41%). Aliitaja yenye asilimia ndogo kuwa ni Dodoma asilimia 3, Singida 4%, Manyara 6% na Kilimanjaro asilimia 10.

Takwimu za Utafiti wa Virusi vya Ukimwi na Malaria nchini kwa mwaka 2007/8 maambukizi ya malaria mikoani, Mwanza inaonekana kuwa na maambukizi kwa asilimia 31 ukifuatiwa na Ruvuma 24%, Mara 30%, Kigoma 20% na Shinyanga 30% na ndio mikoa inayoongoza kwa uhaba mkubwa wa dawa hizo.

Aidha, alisema hali ni mbaya katika wilaya kwenye mikoa yenye uhaba mkubwa. "Katika mkoa wa Mwanza, wilaya ya Ukerewe imeripotiwa kuwa na uhaba wa ALu kwa asilimia 88 katika vituo vyake vya huduma, ikifuatiwa na Sengerema 80%, Geita 70% na Misungwi 65%," alisema Kiria.

Kiria alisema uhaba wa dawa umejitokeza sana kwa kipindi kirefu sasa ingawa kumekuwa na mipango na miongozo thabiti ya kupambana na malaria.

"Katika nchi ambayo kila mwaka watu kati ya  60,000 na 80,000 hufariki dunia kwa malaria, upungufu huu ni hatari kubwa," alisema Kiria na kuongeza kwamba taarifa za sasa za upungufu ni za Januari 28.

Wahariri wakichangia mada hiyo waliungana na Sikika kuitaka Serikali ikomeshe uhaba sugu na kuishiwa dawa mara kwa mara, kufanya ununuzi wa mwaka mzima ili kuwa na dozi milioni 15.6 na kuhakikisha kuwa na dawa za ziada za kutosha angalau kila baada ya miezi sita.

Walisema hilo linawezekana kwa kuwa fedha zinazofadhili mradi huo zinatoka nje na wakati huo huo serikali lazima itafute rasilimali pesa za kutosha  ili kununua dawa za ALu.
Sikika imekuwa ikifuatilia uwepo wa ALu kupitia mfumo wa Serikali kwa miaka miwili sasa na kugundua upungufu huo ambao unaonekana hakuna mtu anayeufanyia haraka kuuondoa.

WAZIRI MKUU AFANIKIWA KUTULIZA JAZBA ZA WAKAZI WA MTWARA....

  Waziri mkuu Mizengo Pinda amefanikiwa kutuliza jazba za wakazi wa Mkoa wa Mtwara kwa kuwaeleza kuwa kiwanda cha kusindika gesi ghafi kitajengwa kijijini Madimba mkoani humo ili mabaki yatokanayo na gesi hiyo yatumike kuvutia uwekezaji wa viwanda, hii ikiwa ni kauli tofauti na ya madai ya wakazi hao ambao hasira zao zilichangiwa na taarifa kwamba kiwanda hicho kingejengwa Dar es salaam.

Kwenye mkutano wa majumuisho uliofanyika january 29 2013 Waziri mkuu baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao kwa siku mbili mfululizo, amesema hakuna tone la gesi ghafi itakayosafirishwa kwa njia ya bomba.

 
Namkariri akisema “Imani yangu ni kwamba maelezo yametosheleza, mtakua na kiwanda chenu cha kusindika, mtakua na kiwanda cha kusafisha, mtakua na hayo matawi kadhaa kwa ajili ya uzalishaji wa umeme kwa ajili ya usindikaji wa viwanda”

Mwanzoni madai ya wakazi wa Mtwara yalikua ni kupinga usafirishaji wa gesi ghafi mpaka Dar es salaam wakieleza kwamba huo mpango utafukuza wawekezaji wa viwanda Mtwara ambao ungechochewa na upatikanaji wa malighafi baada ya kusafishwa kwa gesi.


Pia wananchi walipinga ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kinyerezi Dar es salaam na badala yake wakataka hiyo mitambo ijengwe hukohuko Mtwara.
 
Mbali na hayo, Waziri Mkuu aliwataka wananchi kumsamehe mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia kwa kauli alizotoa december 21 2012 katika kikao cha kamati ya ushauri pale alipoombwa kuyapokea maandamano ya wakazi wa mkoa huo december 27 ambapo aliwaita wapuuzi na wahaini.

Waziri mkuu katika majumuisho yake aliambatana na Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya kazi profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe, Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi Dr. Shukuru Kawambwa na Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi.

Katika hizo siku mbili pia Waziri mkuu alikutana na vyama vya siasa vya upinzani, chama cha Mapinduzi CCM, viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo, Wafanyabiashara, Madiwani na wenyeviti wa mitaa pamoja na Wanaharakati.

ZAO LA KOROSHO BADO NI GUMZO WILAYANI TUNDURU

WAKATI kukiwa na Sinto fahamu juu ya upatikanaji wa Soko la Uhakika la
kuuzia Korosho Wakulima wa zao hilo  wilaya Tunduru mkoani
Ruvuma,wameiomba serikali itoe kibali cha kuruhusu korosho zao kuuzwa
kwa wafanyabiashara binafsi ili kuwaepusha na hasara wanayoendelea
kuipata wakati  huu ambapo wanasubiri malipo yao ya mwaka uliopita.

Kilio hicho kumepazwa katika nyakati tofauti na wakulima hao na
kuungwa Mkono na Viongozi walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Dhalula
wa Chama kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Tunduru (TAMCU) kilicho keti
katika ukumbi wa Chama hicho

 

Wakifafanua taarifa hiyo wakulima hao walisema kuwa hali hiyo
inatokana na  muda wa uvumilivu kupita na hata kuvuka kikomo hivyo
wameamua kuchukua maauzi hayo ya kuitaka serikali ichukue hatua haraka
ili wasiendelee kupata hasara kama ilivyotokea katika msimu wa mwaka
2010/2011.

Walisema katika msimu huu zaidi ya tani 500 ya zao ilo hazikununuliwa
hali mabayo iliwasababishia hasara na matatizo mengi wakulima hao
ambao kwa sasa  wakulima hao hawataki kusikia tena neno la ushirika
kwani unawasababishia umasikini na kukubali kuuza mazao yao ikiwemo la
korosho kwa walanguzi wanaonunua kwa bei ndogo kuliko kusubiri bei ya
serikali ambayo haina uhakika.

 
Akizungumzia hali ya Mkanganyiko huo Meneja wa Chama Kikuu cha
Ushirika cha wakulima wa Tunduru (TAMCU) Bw. Imani kalembo alidai kuwa
hali hiyo inatokana na Chama hicho kukosa sifa za Kukopesheka baada ya
kushindwa kurejesha Deni la zaidi ya shilingi Bilioni.2.8 kati ya
fedha zilizokopwa msimu uliopita.

Alisemsa deni hilo lilishindwa kulipika kufutia ubabaishaji wa
wanunuzi wakubwa ambao alitelemsha bei kwa kiasi kikubwa na kukifanya
chama chao kuuza Korosho zao kwa Bei ya Tsh.850 kwa kilo moja kutoka
Tsh. 1200 walizonunulia kutoka kwa wakulima na kusabishiwa hasara hiyo

Tuesday 22 January 2013

Mkapa ajitosa sakata la gesi

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa 
Kwa ufupi
Mkapa alisema mwenendo wa mazungumzo, maandamano na mikutano ya hadhara inayoendelea mkoani Mtwara, inaelekea kuashiria kuvunjika kwa amani hali aliyosema kuwa inajenga kutokuelewana kati ya viongozi wa vyama vya siasa na Serikali, wananchi na vyama vya siasa na wananchi na viongozi wa Serikali.
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameelezea kufedheheshwa kwake na mgogoro wa gesi, huku akiwataka wananchi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Mtwara kusitisha harakati za maandamano na mihadhara.

Mkapa alitaka wakazi hao kuacha kulumbana na Serikali kuhusu suala hilo, badala yake wajiandae kukaa meza moja nayo kutafuta mwafaka kwa njia ya amani.
Katika tamko lake alilolitoa Dar es Salaam jana, Mkapa alisema: “Fujo, vitisho, kupimana nguvu na malumbano siyo masharti ya maendeleo.
“Nikiwa kama mwana - Mtwara na raia mwema, mpenda nchi, nimefedheheshwa sana na matukio haya ya siku za karibuni Mtwara. Kwa sababu hiyo natoa wito kwa wadau wote wa maendeleo ya Mtwara, kusitisha harakati hizi na maandamano na mihadhara.
“Badala yake wajipange kukaa pamoja katika meza moja,  kupitia historia, kutathmini mipango, kuchambua kwa kina mikakati ya utekelezaji wake, hatimaye kufikia mwafaka wa ujia wa maendeleo. Liwezekanalo leo lisingoje kesho.”
Mkapa alisema mwenendo wa mazungumzo, maandamano na mikutano ya hadhara inayoendelea mkoani Mtwara, inaelekea kuashiria kuvunjika kwa amani hali aliyosema kuwa inajenga kutokuelewana kati ya viongozi wa vyama vya siasa na Serikali, wananchi na vyama vya siasa na wananchi na viongozi wa Serikali.
“Mtafaruku huu haufai kuachwa na kutishia usalama, mipango ya maendeleo siyo siri, mikakati na mbinu za utekelezaji wake siyo siri,” alisema Mkapa na kuongeza:
“Maelezo yake mazuri yanaweza kutolewa yakadhihirisha namna na kasi ambayo rasilimali zinawanufaisha wananchi wa eneo zilimo na taifa zima.”
Mkapa alisema hali hiyo ni tishio kwa wawekezaji wa ndani na nje, kwani mara zote hawapendi vurugu, fujo na vitisho.
Kauli hiyo ya Mkapa imekuja siku kadhaa tangu kuwapo kwa maandamano na vurugu zinazofanywa na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara wanaopinga gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.
Tayari viongozi kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete wametoa tamko juu ya suala hilo wakionya kuwa halikubaliki kwa kuwa rasilimali hiyo si kwa ajili ya wana Mtwara pekee.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyalaani maandamano hayo akisema walioyaandaa wamelenga kuigawa nchi vipandevipande, Chadema kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kumbana waziri huyo ili aondoe udhaifu uliopo katika sekta ya nishati.
Desemba mwaka huu, maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara waliandamana wakipinga uamuzi wa Serikali kusafirisha gesi kwa njia ya bomba kutoka hapa kwenda Dar es Salaam.
Maandamano hayo yaliyoratibiwa na vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, Sau, Tanzania Labour Party (TLP), APPT- Maendeleo, ADC, UDP na DP yakishirikisha wananchi wa wilaya za mkoa huo, zikiwamo Tandahimba na Newala  yalianzia katika Kijiji cha Mtawanya hadi Mtwara Mjini kupitia barabara ya kwenda Msimbati eneo ambako gesi asilia inapatikana.




maafa stendi ya ubungo

ubungo1 6ac3f
ubungo2 cc0a5
SEHEMU ya ukuta wa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo alfajiri umeanguka na kuyaharibu vibaya magari zaidi ya ishirini yaliyokuwa yameegeshwa nje ya eneo hilo. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa idadi ya magari yaliyopatwa na ajali hiyo yanakadiriwa kufikia 24 ambapo watu watatu wanasemekana wamejeruhiwa.
ubungo3 3104f
ubungo4 27999
ubungo5 bb613
ubungo c5ed1

Saturday 19 January 2013

MKUU WA WILAYA YA TUNDURU AAGIZA VITANDA VIPELEKWE ARAKA KATIKA ZAHANATI YA KITANDA.


Akiwa ndani ya zahanati hiyo
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bwana Chande Nalicho hii leo alipokuwa katiaka ziara yake ya kutembelea baadhi ya maeneo ambayo serikali ilitoa ahadi ya ujenzi wa miradi mbalimbali.

Mkuu huyo wa Wilaya ametembelea katiaka zahanati iliyopo katika kijiji cha Kitanda kata ya Mlingoti Mashariki wilayani Tunduru nakumuagiza Muuguzi mkuu wa wilaya ya Tunduru Bwana Norbet Haule kupeleka vitanda haraka iwezekanavyo katika Zahanati hiyo.

Agizo hilo amelitoa baada ya kukuta Zahanati haina kitanda hata kimoja.
Hivyo imepelekea kwa mama wajawazito ambao wanafika katika Zahanati hiyo kujifungua kwa shida na kuwaladhimu kulala chini .

Akiendelea kuzungumza Bw. Chande Nalicho amedai hakupendezwa na uongozi huo wa Zahanati kwa kuwalaza wagonjwa chini pale wanapokuja kupata tiba.

Katika taharifa fupi iliyosomwa na Muuguzi Mkuu wa wilaya ambapo amesema Ujenzi wa Zahanati hiyo umeghalim jumla ya 330,009,00/=(milioni mia tatu therathini na mia tisa) imejegwa  na TASAFU na katika ujenzi huo Serikali imechangia milioni sita/(6,000000/=) na Zahanati hiyo Bado inakabiliwa na tatizo kubwa la wauguzi(watumishi)ambapo mpaka sasa inajumla ya wauguzi(watumishi)wawili,tu na mmoja kati ya hao ni Elizabeth Mbepela.

Thursday 17 January 2013

MTOTO HUYU ANAHITAJI MSAADA WA MATIBABU

 
Mtoto Simoni Mlope
 Kulia ni mama wa mtoto Simoni Mlope ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa tundu kwenye moyo na kulazimika kukatisha masomo yake ya shule ya msingi. Hapo yupo nyambani kwake maeneo ya mahenge alipotembelewa na waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma.
*************


Mtoto simon Mlope mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa eneo la mahenge katika manispaa ya songea mkoani Ruvuma amelazimika kukatisha masomo yake ya shule ya msingi akiwa darasa kwanza  kutokana na mototo huyo kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo .



Mtoto simon Mlope alikubwa na ugonjwa moyo  tangu mwaka 2001 mara baada ya kuzaliwa na kugundulika kuwa  moyo wake una tundu hali ambayo inasababisha  kuvuta pumzi kwa shida.



Mama wa mototo  simon mlope anayeitwa AMINA ALLY  anawaomba watanzania kumsaidia mtoto  wake fedha za matibabu Baada ya kuambiwa na madaktari kuwa simon anatakiwa kwenda nchini  india kutibiwa,baada ya kupata rufaa kutoka muhimbili mwaka 2006  huku familia yake ikiwa haina uwezo kabisa.



Majirani wa familia ya simon nao wanasema kuwa mototo simon anahitaji msaada wa haraka kwa kuwa hali yake sio nzuri na kuwaomba watanzania wamsaidie.



Kinachosikitisha zaidi baba wa mtoto huyo  anayejulikana kwa jina la SIMON MLOPE  ameondoka nyumbani hapo tangu mwaka 2011 na hajulikani aliko kwa sasa, ingawa mwanzoni alisema yuko nchini Msumbiji.

Kwa anayeguswa na tatizo hili na anataka kumsaidia  SIMONI MLOPE  atumie simu namba  0752732290

 

JIMBO KUU KATOLIKI LA SONGEA LAFUNGA MCHAKATO WA KUMTANGAZA SISTA BERNADETA MBAWALA KUWA MWENYEHERI

 Hili ni sanduku lililowekwa masalia ya Mtumishi wa Mungu  Sista Bernadeta Mbawala katika kanisa la jimbo kuu katoliki la Songea Mkoani Ruvuma ambaye 14.1.2013 jimbo lilifunga mchakato wa kumtangaza mwenyeheri kwa kuadhimisha misa takatifu na kusafirsha taarifa zake zilizokusanywa na mahakama ya mchakato.
 Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki Mhashamu Norbert Mtega akitoa wito kwa watanzania kuchangia mchakto wa kumtangaza sista Bernadeta kuwa Mwenyeheri. na baadaye mtakatifu.


 Maandamano yakielekea ndani ya kanisa kwa ajili ya kuadhimisha misa ya mchakato huo.

Masista wakiwa wameshika picha ya sista Bernadeta Mbawala 
 Masista wakiimba katika misa takatifu ya mchakato huo.
 Hao ni mapadre wa kanisa katoliki la Songea wakiwa ndani ya kanisa 

 Hili ni sanduku lililowekwa masalia ya Mtumishi wa Mungu sista Bernadeta Mbawala.

Jimbo kuu katoliki  la Songea leo limeadhimisha misa takatifu ya kufunga mchakato wa kumtangaza  sista BERNADETA MBAWALA OSB  kuwa mwenye heri na baadaye mtakatifu katika ngazi ya jimbo.
****************************
Akizungumza na waumini wa jimbo katoliki la Songea  Askofu mkuu wa jimbo la Songea  Mhashamu NORBERT MTEGA alisema jimbo kwa upande wake tayari limeshafanya utafiti na kukusanya   taarifa mabalimbali alizoziandika sista Bernadelta Mbawala, ambapo wamepata barua alizoandika enzi za uhai wake zaidi ya mia moja, na machapisho mbalimbali ya magazeti.

Pia walipata sala alizotunga mwenyewe na kuzitumia kusali lakini kazi kubwa ilikuwa ni kuhoji watu kadiri ya sheria za kanisa ambapo tayari wamehoji watu 83, wakiwemo mapadre na watawa kutoka Songea na njombe.

Askofu Mtega aliongeza kuwa kanisa sasa limechukua hatua ya  kuanza  kutafiti na kuzungumza hadharani  ili sista Bernadeta OSB aweze kupata heshima ya kutangazwa mtakatifu.

Askofu huyo wajimbo kuu katoliki la Songea Mhashamu Norbert Mtega katika Mahubiri yake hayo alisema kama sista BERNADETA OSB atafanikiwa kutangazwa kuwa mtakatifu atakuwa ni mtanzania wa kwanza kufikia hatua hiyo, na kuwaomba waumini waendelee kuomba ili mchakato huo ufanikiwe.

Alisema baada ya kumaliza mchakato huo wa ngazi ya jimbo kinachosubiliwa sasa ni kutokea kwa miujiza miwili  na miujiza hiyo itokee popote duniani, ukitokea muujiza kwanza basi sista Bernaderta  atatangazwa kuwa mwenye heri na ukitokea muujiza wa pili atatangazwa kuwa mtakatifu.

Askofu alitumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania kuchangia kwa hali na mali zoezi hili la mchakato kwa kuwa kunahitajika zaidi ya dola 20,000/= ili uweze kukamilika.

Aidha Askofu Mtega alimuelezea Sista Bernadeta OSB  Kuwa alizaliwa mnamo mwaka 27/10/1911  katika kijiji cha likuyufisi wakati huo kwa sasa ni manispaa ya Songea, wazazi wake ni Stefan Msikazonge na Agata Mayanda, alibatizwa 5/11/1911 peramiho, kipaimara alipata tarehe 8.12.1921 peramiho, na alijiunga na utawa 7.08.1929 peramiho, Nadhiri za kwanza alipata 11.11.1934  wakati huo hakukuwa na nadhiri za daima na alikufa ta29.11.1950.

Sista Bernadeta Mbawala OSB  kutoka nyumba ya mtakatifu Agnes ya chipole  maisha yake na wazazi wake yalikuwa ni ya sala na kuabudu sana na alikuwa anatokewa na moyo mtakatifu wa yesu n aalikuwa anazungumza sana na bikira maria na mtakatifu Agnes,

Aliugua sana lakini aliunganisha mateso yake nay a yesu kristu na hakuwahi kutamka kutafuta dawa za mitishamba, alitolea mateso yake kwa kuwaombea wakosefu na hivyo amewafundisha wakristu kuyapokea mateso kwa imani kwa kuwa mateso ni moja ya sala na sadaka.

Baada ya kufa kwake miaka 61 baadaye  kanisa limeshuhudia watu wakienda kusali katika kaburi lake na kufanikiwa mambo yao huku hakuna kiongozii wa dini aliyeagiza watu wafanye hivyo huo ni ushuhuda kuwa sista BERNADETA anafaa kuwa mtakatifu.

Kazi kubwa imefanywa na mahakama ya mchakato huo ya kuandaa taarifa za sista Bernadeta ambazo taarifa hizo zimekamilika na Askofu mtega ametia saini na kugonga muhuri tayari kwa kusafirishwa kwenda ROMA  kwa mchakato zaidi.

Naye padre CAMILIUS HAULE  naibu wa askofu aliyemwakilisha  askofu katika kufanya kazi kwenye Mahakama ya mchakato  huo  akiwa ni mtetezi wa haki  ametoa tamko .nanukuu  hakuna kitu chochote cha kutiliwa shaka kati ya yale yote yaliyokusanywa na mahakama ya mchakato na ndio yatamkwe hivyo.

Kwa upande wake waziri wan chi ofisi ya makamu wa Rais mazingira  dokta terezya huvisa ametoa ushuhuda mbele ya waumini kuwa amekuwa akiomba katika kaburi la sista Bernadeta na kupata mafanikio ikiwa pamoja na uongozi na ametoa mchango wa shilingi milioni mbili kwa ajili ya mchakto na ujenzi wa kanisa la lizaboni katika manispaa ya songea.

Taarifa za sista bernadeta ndio zinazosafirishwa kwenda ROMA kwa ajili ya kuendelea na mchakato zaidi lakini Masalia ya mwili wake yamebaki katika sanduku la mbao katika kanisa la jimbo kuu katoliki  la songea kwa wale wote wanaohitaji kusali katika masalia hayo wanaalikwa.

TUPE MAONI YAKO