Friday 28 June 2013

WATUMISHI 12 WA HALMASHAURI YA WILAYA ZA MKOA WA RUVUMA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MAKOSA YA JINAI NA UHUJUMU UCHUMI

Kamanda wa Taasis ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoa wa Ruvuma     DAUDI MASIKO
      Kamanda TAKUKURU akisisitiza jambo
              Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda wa Takukuru Ruvuma
-----------------------------------


                                                     
Taasisi ya kuzuia na kupambanana Rushwa TAKUKURU mkoani Ruvuma imewafikisha mahakamani watumishi 12 wahalmashauri za wilaya  katika mkoawa Ruvuma kujibu mashtaka mbalimbali ya rushwa .

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini  kwake kamanda wataasis yakuzuia na kupambana na rushwawa mkoa wa Ruvuma DAUDI MASIKO amesema watumish ihao 12 

wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya rushwa chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007, sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 16 mwaka 2002 na sheriayauhujumu uchumi kifungu namba 200 yamwaka 2002.

Watumishi waliofikishwa mahakamaniwatano wanatoka halmashauri ya wilaya ya Songea, watano wanatoka halmashauri ya wilaya ya mbinga na wengine wa wili wanatoka katika halmashauri ya wilayayaTunduru.

    
Pamoja na maelezo hayo waandishi wa habari walitaka kujua kwanini mashtaka hayo yamewakwepa wakurugenzi wakati wao ndio wanawasimamia watumishi kufanya shughuli za kiutendaji na majibu ya kamanda watakukuru Ruvuma ni haya .

Watumishi hao wanatuhumiwa kushtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, makosa ya jinai .


 

Thursday 27 June 2013

MMETOKELEZEA DADA PAMELA NA MPAMBE WAKE

HII NIMEIPENDA

HII HAIJAWAHI KUTOKEA AFRICA ULINZI WA UHAKIKA

Ulinzi katika ziara ya Obama ni wa hali ya juu kuliko ulinzi wa aliyewahi kupewa Rais yeyote wa Marekani kwa safari yake ya Afrika mwaka huu.
 
Tayari jeshi la nchi hiyo limewasili nchini, kuweka mambo sawa na kukagua maeneo yote ya karibu na sehemu atakazotembelea na kupita wakati wa ziara hiyo. Maaskari na majasusi zaidi ya 500 wapo Dar es Salaam kuhakikisha usalama huo na kuweka vifaa mbalimbali vya mawasiliano Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.
 
Licha ya hilo, ziara yake kutakuwa na askari 1,687 wakataokuja kwa meli maalumu kubwa ya kivita iliyosheheni silaha mbalimbali, ikiwamo ndege sita za kivita aina ya AV-8B Harrier na helikopta za kivita 23, ambazo zinatarajiwa kupasua anga la Tanzania kuimarisha ulinzi.
 
Meli hiyo ya kisasa aina ya Wasp Class (Uk 1), pia itakuwa imebeba meli nyingine zaidi ya tano maalumu kwa kubeba vifaru, magari ya deraya, askari na vifaa vingine itatia nanga Bahari ya Hindi kuongeza nguvu iwapo lolote litatokea.
 
Taarifa inaonyesha italazimika kuwapo kwa meli tatu za aina hiyo wakati wa ziara yake nchini Senegal, Tanzania na Afrika Kusini kwani mwendo wake siyo kasi hivyo kulazimika kutumia zote hizo kwa ajili hiyo.
 
Meli hiyo kubwa imeundwa kuwezesha askari wa Marekani kuingia kwa urahisi eneo la vita kwa brigedi nzima, kwani wanaweza kutumia aina zote za vita majini, angani na ardhini. Ni meli aina hiyo zilizotumika vita vya Marekani na Iraq. Licha ya mitambo ya kivita, ina hospitali kubwa yenye uwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa ya 600.
HATIMA YA SUGU IPO MIKONONO MWA DPP

ImageHatma ya kufikishwa mahakamani kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘’Sugu”( Chadema), iko mikononi mwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali.
 
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema jana kuwa jeshi lake limekamilisha upelelezi kuhusu tuhuma zinazomuhusu Sugu na kwamba wanasubiri maelekezo ya kumfikisha mahakamani. 
 
Mbilinyi alikamatwa juzi mchana akiwa mjini Dodoma anakohudhuria vikao vya bunge na habari zilisema anatuhumiwa kutoa maneno ya kashfa na uchochezi dhidi ya Waziri, Mkuu Mizengo Pinda.  
 
 Inadaiwa kuwa mbunge huyo amefanya hivyo kupitia mtandao wa kijamii. Kamanda huyo alisema jana Mbilinyi aliripoti katika Kituo cha Polisi Kati kama alivyotakiwa na jeshi hilo na kuongezewa dhamana hadi leo anapotakiwa kurudi tena kusikiliza hatma yake.
 
 Misime alisema “jeshi hilo liliamua kumkamata mbunge huyo baada ya kugundulika kuandika maneno ya kumtukana Waziri Mkuu kuhusu utendaji wake na kumdhalilisha katika siku ambayo hakuitaja.” 
 
Taarifa zisizo rasmi zinaonyesha kuwa, mbunge huyo anatuhumiwa kuandika maneno hayo ya kashfa kufuatia kauli ya Pinda hivi karibuni kuhusu kuwataka polisi kuwapiga raia wasiotii sheria. 
     
 
  Alikuwa akijibu swali la papo kwa papo ndani ya Bunge wiki iliyopita ambapo alisema Serikali imechoshwa na vitendo vya watu kutotii sheria na kutoa mfano wa matukio ya Mtwara na Arusha. 
Huko Mtwara polisi walitumia nguvu zaidi kuwadhibiti wananchi waliokuwa wakikataa gesi isisafirishwe kwa njia ya bomba kwenda Dar es Salaam, wakati huko Arusha, walifanya hivyo katika kuwatawanya wafuasi wa Chadema, waliokuwa wakishiriki katika tukio la kuaga maiti. 
 
Baadhi ya watu wakiwamo wanaharakati walisema kauli hiyo inaweza kuleta chuki kati ya polisi na wananchi.

BAADHI YA MAGAZETI YA LEO

Monday 24 June 2013

POLISI RUVUMA WAKAMATA MENO 18 YA TEMBO

WATU WANNA WANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI MKOANI RUVUMA BAADA YA KUTELEKEZA MENO YA TEMBO KUMI NA NANE KATIKA KIJIJI CHA MAJALA KATIKA WILAYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA .

AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA RUVUMA DEUSDEDITI NSIMEKI AMESEMA TAREHE 19.6.2013 MAJIRA YA SAA NNE USIKU ASKARI POLISI WA WILAYA YA TUNDURU WAKIONGOZWA NA MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA TUNDURU NA WAKISHIRIKIANA NA MAAFISA WANYAMAPORI  WALIFANYA DORIA NA KWA PAMOJA KWA AJILI YA KUWAFUATILIA WATU WANAOSAFIRISHA NYARA HIZO KUTOKA KIJIJI CHA LIGUNGA KWENDA KIJIJI CHA MAJALA .

MNAMO TAREHE 20.6.MWAKA HUU MAJIRA YA SAA 3.00 USIKU NJE KIDOGO YA KIJIJI CHA MAJALA KATA YA NANDEMBO WILAYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA  ASKARI WALIWEZA KUONA WATU WANNE WANASUKUMA BAISKELI KUELEKEA KIJIJICHA MAJALA, WATU HAO BAADA YA KUONA MWANGA WA TAA ZA GARI LILIKUWA NA ASKARI POLISI NDIPO WALIPOLISHTUKIA NA KUTUPA BAISKELI ZAO NA KUKIMBIA.

BAISKELI HIZO ZILIKUWA ZIMEFUNGWA VIFURUSHI NA ASKARI WALIPOFIKA ENEO HILO WALIGUNDUA KUWA NI MENO YA TEMBO HIVYO WALIFANIKIWA KUKAMATA MENO YA TEMBO 18 YENYE UZITO WA KILOGRAM 84 NA THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 200 .

AIDHA KAMNDA WA POLISI WA MKOA WA RUVUMA AMETOA ONYO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI HILO ILI KUFANIKISHA KUKAMATWA KWA WATU HAO.

PICHA ZA MENO YA TEMBO YALIYOKAMATWA KATIKA WILAYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA

                                    Askari na waandishi wa habari

                                                                       MENO YA TEMBO
kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deudedit Nsimenki akiwa ameshika JINO LA TEMBO yenye uzito wa kilo kumi




  24.6.2013   SONGEA

Watuwannewakaziwakijiji cha Majala kata 
ya NandembowilayayaTunduru mkoani Ruvuma  wanatafutwa na jeshi la polisi kwatuhuma za kuyatelekeza meno kumi  na nane ya tembo wakati wakiyasafirisha kutoka kijiji cha ligunga kuelekea kijiji cha Majala.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wapolisi wa mkoa wa Ruvuma bwana DEUSDEDITI NSIMEKI amesema watuhumiwa haowalikimbia nakutelekeza baiskeli zao walipoona mwanga wataa  za gari likiwa na askari polisi.



Kamanda Nsimeki amesema watu hao walikuwa wamebeba pembe za tembo kumi na nane zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia mbili. Na mpaka sasa hakuna aliyekamatwa lakini polisi bado wanaendelea na msako mkali.

1.

Aidha kamanda Nsimeki ametumia nafasi hii kuwaomba wananchi Waendelee kuwaunga mkono polisi kwakuwapa ushirikiano wakutoa taarifa sahihi kama hii ambayo imewawezesha kukamata meno mengi ya tembo.


Akiwageukia waalifu ametoa onyo kali kwa kuwataka waache mara moja kuhu jumuu chumi wa nchi kwa kuwa vita ya kupambambana na wawindaji na wafanyabiashara wa meno ya tembo au raslimali nyingine za taifa haina suruhu kwa kuwa polisi namaliasili wamejipanga kuhakikisha tatizo hili linakwisha kabisa.


Hili ni tukio la tano kutokea la kukamata meno ya tembo katika mkoa wa Ruvuma ambapo uchunguzi wa awali haujaonyesha kama tembo wanaouwawa wanatokea katikaMbuga za selou au nchi jiraniyaMsumbiji.

Sunday 23 June 2013

MWENYEKITI UVCCM TAIFA: SIAFIKI SERIKALI MFUMO WA SERIKALI TATU


Sunday, June 23, 2013

MWENYEKITI UVCCM TAIFA
 
ARUSHA, Tanzania

MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu kama inavyopendekezwa katika rasimu ya katiba.

Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.


Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge (CCM) zanzibar, amesema uwepo mfumo wa serikali tatu ni mzigo mkubwa kwani kutokana na uduni wa uchumi wan chi yetu itakuwa vigumu kuendesha serikali tatu kwa maana ya serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara na ule wa muungano.

“Jamani tusidanganyane, kuendesha serikali tatu ni mzigo, kwa uduni wa uchumi wetu sidhani kama itakuwa rahisi kuendesha serikali tatu, kama kutakuwa na serikali tatu kuna hatari ya kuvunjika kwa muungano wetu huu maana uwezo kuchangia hatuna, tutajiingiza kwenye matatizo makubwa, vijana tuwe makini na tutumie taaluma zetu kuhimiza umuhimu wa kuwepo kwa muungano huu wa sasa,"

Aidha Sadifa amewahimiza vijana kuwa mfano mzuri kwa jamii huku akiwahimiza kuwa waadilifu, wazalendo, kujiamini na kuwa na nidhamu hali ambayo itasaidia kuwepo kwa amani na usalama wa nchi.


Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo hayawezi kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wa zanzibar na Tanganyika  kama njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.

“Vijana tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea muungano wetu wa sasa, taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani na usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai nchi haitatawalika,” amesema



Hata hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na vyama vinavyoeneza chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku akifafanua kuwa kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na yassingilie haki za wengine.

“Chama pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama vingine vimeanzishwa ambavyo mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi ukajikopesha fedha kienyejienyeji kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini na saccos hizi ambazo ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa


Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.
Amesema kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto wa wakulima’ wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo hiyo jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa wanafunzi hao.

“Mikopo ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa wakati kwani lazima tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa mikopo kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni tatizo,” amesema Mtulya (habari na TAIFA LETU.com).

HAFLA YA WASTAFU WA TAMISEMI NA KIKAO CHA MUUNGANO- DODOMA


IMG_0281Makatibu Tawala wa Mikoa Wastaafu, Bernard Nzungu  (kushoto) na Getrude Mpaka wakisakata Rhumba katika sherehe ya kuwaaga viongozi na watumishi waliohama na wastaafu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka ya serikali za mitaa iliyofanyika kwenye viwanja vyaBuge Mjini Dodoma Juni 22, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0165 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi runinga ya nchi 32 Katibu Twala wa mkoa wa Pwani Mstaafu, Bernard Nzungu katika sherehe ya kuwaaga viongozi na watumishi waliohama na wastaafu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka ya serikali za mitaa iliyofanyika kwenye viwanja vyaBuge Mjini Dodoma Juni 22, 2013. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Hawa Ghasia. (Picha naOfisi ya Waziri Mkuu)
 

MAWE HATO YAPO KATIKA ZIWA NYASA KATA YA LIULI MKOANI RUVUMA YANAVUTIA KWA UTALII WA NDANI NA WA NJE


Mwonekano wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.
 Viongozi wandamizi wa Shirika lisilo la Kiserikali la RUNECISO wakielekea Katika Jiwe la Pomonda kuona hali ya Pango lilipo katika Jiwe hilo ambalo lilihifadhi watu waliojificha wakati wa Vita vya 1 na vya 2 vya Dunia
 Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.

Saturday 22 June 2013

YALIOJILI KWENYE KILI TOUR DODOMA

 LINEX kwa stage
  Roma Mkatoliki
 Dula na Zebwela kwenye stage walisimamia show
Wapenzi wa burudani Dodoma wakiingia katika uwanja wa Jamhuri Dodoma kwa wingi sana.
 
 

DIAMOND AKIWA COMORO

Picha kutoka kushoto
ni Dumi Utamu,Diamond Platnumz,Rama Tonser
&Emma Platnumz

OMMY DIMPOZ APIGWA CHUPA NA MASHABIKI AKIWA JUKWAANI HUKO DODOMA

Kuna tetesi kuwa Ommy dimpoz amepigwa mawe jukwaaani dodoma na kushindwa kufanya show ya kilimanjaro music award dodoma. 
Wadau toka  Dodoma wasema  msanii yoyote atakaye mdiss msanii wa dodoma hawatamruhusu kufanya show Dodoma  na watamshusha jukwaani kama walivyo fanya leo  kwa  Ommy

BARAZA LA MADIWANI MBINGA LAGAWANYIKA NA KUZAA NYASA


 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu akizungumza katika kikao cha uvunjaji wa baraza la madiwani wa wilaya ya Mbinga leo hii katika ukumbi wa Maendeleo
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu akionyesha hati za utambulisho wa Halmashauri mbili za nyasa na mbinga kabla yta kukabidhi hati hizo
 Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyasa Shaib Mnunduma akipokea hati ya utambulisho wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa
Toka toka kushoto kwako aliyekaa ni mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga na aliyesimama ni  Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga Hussen Ngaga akizungumza jambo wakati wa Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kabla ya kuvunjwa.
 Mkuu wa wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi akizungumza baada ya kutangazwa na mkuu wa Mkoa wa Ruvuma  Said Thabiti Mwangu  kuvunjwa  Baraza la madiwani  wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga

LUCY TOMEKA ANYAKUA TAJI LA REDDS MISS KINONDONI 2013


 
Mshindi wa Redds Miss Kinondoni 2013, Lucy Tomeka akivalishwa taji lake na mrembo aliyekuwa akilishikilia taji hilo Redds Miss Tanzania 2012/2013, Bright Alfred. Lucy Tomeka aliweza kuchukua taji hilo kwa kuweza kuwagalagaza wenzake wapatao 12 katika kinyang'anyiro hicho kilifanyika jana ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip jijini Dar.    

 Warembo waliofanikiwa kuingia katika tano bora wakifurahia kwa pamoja, katikati ni Redds Miss Kinondoni 2013 Lucy Tomeka, (shoto kwake) ni Prisca Clement, (kulia kwake) ni Phillios Lemi. Wengone ni Sarah Paul (kwanza kulia) na Linda Joseph (kwanza kushoto).

  Tatu bora ni katikati ni Redds Miss Kinondoni 2013 Lucy Tomeka, (shoto kwake) ni Prisca Clement, (kulia kwake) ni Phillios Lemi. Habari na G .sengo

WATOTO WALILIA HAKI ZAO ZA KUISHI, KULINDWA NA KUHESHIMIWA

                         Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng, Stella Martin Manyanya ambaye pia ni Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma akizungumza na Watoto wa Wilaya ya Nyasa alipotembelea wilayani humo hivi karibuni


Na Gideon Mwakanosya ,Namtumbo

WATOTO wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kukomesha vitendo vya ubakaji vinavyofanywa kwa watoto wadogo wilayani humo kwani tatizo hilo limeonesha kuwa kubwa ambapo katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu jumla ya watoto 14 walibakwa na kesi zao kuripotiwa katika kituo kikubwa cha Polisi cha Wilaya hiyo.

Wakisoma Risala ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu jana iliyofanyika Kiwilaya katika kijiji cha Hanga wilayani Namtumbo walisema kuwa pamoja na jitihada za Serikali na wadau mbalimbali za kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwa watoto wadogo bado tatizo hilo ni kubwa kwa Wilaya ya Namtumbo.

Walieleza kuwa katika takwimu za miaka miwili iliyopita zinaonesha kuwa mwaka 2012 wanafunzi 16 waliacha shule kutokana na mimba na wanafunzi 151 kati ya hao wavulana 88 na wasichana 63 waliacha shule kwa utoro na mwaka 2013 wanafunzi 12 wa kike walipata ujauzito na kuacha shule huku wanafunzi 34 walikuwa watoro mwaka 2012 na mwaka 2013 wanafunzi 18 ambao waliripotiwa kuwa watoro.

Walisema kuwa tatizo la watoto kutumikishwa kazi za majumbani kama vile kazi za ndani na mashambani,kutumiwa na watu wazima kufanya biashara ndogo ndogo hata kama wanatakiwa kuwepo mashuleni bado limekuwa ni tatizo hivyo ni vyema kila mzazi akatambua kuwa kila mtoto ni wake na anahitaji malezi bora hasa kuwapatia elimu iliyo bora na itasaidia kupunguza tatizo la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Kwa Upande wake mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu alisema kuwa kila wananchi wakiwemo wazazi na walezi wanawajibu wa kuhakikisha kuwa watoto wao hawatumikishwi kazi za hatari na kazi zinazowazidi umri ili kupunguza tatizo la watoto kukimbilia mitaani na kujiingiza katika mambo mabaya ikiwemo madawa ya kulevya.

Alisema kuwa kutowajibika kwa wazazi na walezi katika kulea familia kunasababisha mambo mengi yasiyofaa ndani ya jamii ikiwemo utoro,mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hivyo ni wajibu wa kila mzazi katika kuwafichua waharifu wanaowapa mimba wanafunzi ili vitendo hivyo vikomeshwe kabisa ndani ya Mkoa huo.

Aidha alisema kuwa wazazi na walezi watambue kuwa watoto wanahaki ya kulindwa, kukua,kuendelea kuishi na kushiriki kutoa mawazo ndani ya jamii lakini kuna baadhi ya wazazi a walezi watoto wanapohitaji huduma hupewa karipio kali na wakati mwingine kipigo pasipo sababu.

MWISHO.

Sunday 16 June 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU MLIPUKO WA BOMU ARUSHA HII HAPA ISOME


Inspekta Jenerali wa Polisi nchini, ametoa taarifa kwa vyombo vya habari, kisha amejibu maswali kadhaa, vitu vya msingi kwa sasa ni kuwa Taarifa Muhimu zitatolewa na Jeshi kwa wakati muafaka tena kwa usahihi, ila kwa leo amesema hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa na jeshi kutokana na tuhuma za tukio hilo ingawa Ushirikiano umepatikana wa kutosha kutambua wajihi wa anayesadikiwa ndiye mtuhumiwa, lakini pili, Jeshi la Polisi litaifanyia kazi kauli ya Kiongozi mmoja wa Chama cha siasa aliyesema watu wasipochagua chama chao watakufa, watakufa kabisa

TGNP NA MPANGO WA UTAFITI SHIRKISHI WA URAGHABISHI

Miongoni mwa Wanawake walipo Pembezoni wakipepeta pumba za Mchele ili waweze kupata punje za mchele ambazo zinawasaidia kwenda kutengeneza chakula chao au vitumbua ambavyo wanaviuza na kujikimu na maisha, hapo ni Songea
Bibi mkazi wa Bombambili Songea ambaye anakadiliwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 70, akitengeneza udongo ambao unapendwa sana na kina mama(Picha zote na Stephano Mango, Songea)

Na, Privatus Karugendo

KATIKA jitihada zake za kupambana na mfumo dume, uliberali mamboleo na mifumo yote kandamizi na kupambana ili rasilmali ziwanufaishe wanawake walioko pembezoni, TGNP imeanzisha mpango wa utafiti shirikishi wa uraghabishi.

TGNP, imeamua kuukumbatia mpango huu kwa vile unatoa nafasi pana ya ushirikishwaji hadi ngazi ya vijijini na kuchochea kuibua kero na changamoto nyingi ambazo zinahitaji majibu ya jamii nzima.

Mpango huu unatumika kama mbinu muhimu ya kujifunza, kutafakari, kuchambua na kutekeleza mikakati mbalimbali ya ujenzi wa Tapo la ukombozi wa wanawake kimapinduzi lililokita katika ngazi za msingi ya kijamii na lenye uwezo kwa kudai uwajibikaji katika kutoa huduma bora, kusimamia rasilimali za taifa ili ziwanufaishe makundi yaliyoko pembezoni hususan wanawake.

Lengo kuu na mpango huu wa utafiti shirikishi wa uraghabishi ni kuwezesha ushiriki wa wanawake, wanaume, makundi na mitandao katika ngazi ya jamii kufanya uchambuzi wa hali halisi kwa mrengo wa ukombozi wa wanawake kimapinduzi; kuibua kero na changamoto zinazokabili makundi husika na za pamoja.

Mpango huu pia unalenga katika kukuza uwezo na uelewa wa uchambuzi wa kero zinazoikabili jamii.

Tamko la TGNP kwa vyombo vya habari lilitolewa tarehe 9. 6. 2013, ni la mpango huu ulioendeshwa kwenye wilaya tatu za Mbeya Vijijini, Kata ya Mshewe, Morogoro Vijijini Kisaki na Kishapu – Shinyanga. Katika makala hii tutajadili mrejesho wa utafiti huu ambao ni wa aina yake.

Changamoto za uwekezaji na mgawanyo mbaya wa ardhi kwa wananchi, ilijitokeza katika utafiti huu na mfano mzuri ni Kata ya Mshewe, Mbeya Vijijini. Katika kata hii utafiti ulibaini mgawanyo mbaya wa ardhi kwa wawekezaji; ardhi nzuri na yenye rutuba imetolewa kwa wawekezaji kiasi kwamba wenyeji hawana mashamba na wanalazimika kuwa vibarua kwenye mashamba ya wawekezaji.

Mbaya zaidi ni kwamba wawekezaji wenyewe wanawalipa kidogo. Mfano wanawake wanalipwa kati ya shilingi 2,500 hadi 3,000 kwa siku.

Pamoja na kulipwa kidogo, wanakumbana na rushwa ya ngono na manyanyaso mengine hali inayosababisha ongezeko la magonjwa ambukizi yakiwamo VVU na ukimwi.

Changamoto hii ya mgawanyo mbaya wa ardhi imejitokeza pia katika Kata ya Kisaki, Morogoro mjini, ambapo wakulima wadogo wadogo wanapambana na wafugaji.

Kwa vile wafugaji hawana maeneo ya kutosha kwa mifugo yao, wanaingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kuleta vita mbaya. Kwa upande mwingine wafugaji wanatumia fedha kuwahonga viongozi ili wasisumbuliwe wanapoingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima.

Matumizi ya fedha ni kupokonya wanyonge haki zao, ni tatizo sugu kwa wananchi waishio pembezoni.

Suala jingine muhimu lililojitokeza kwenye utafiti huu wa TGNP kwenye wilaya tatu, ni upatikanaji wa maji safi na salama.

Pamoja na sera ya taifa kwamba maji yawe umbali wa mita 400 kutoka kwa makazi ya watu, bado maeneo mengi hapa Tanzania yana tatizo kubwa la kupata maji safi na salama. Watu wa Kishapu na Mshewe, ni miongoni mwa wananchi wa Tanzania ambao bado wana tatizo hili kubwa. Kijiji cha Ilota- Mshewe, wananchi wanalazimika kuchangia maji machafu na mifugo.

Tatizo hili la maji safi na salama ni kubwa sana katika vijiji vya Isoso na Lubaga katika Kata ya Kishapu, wanawake wanatembea mwendo mrefu na katika mazingira hatarishi kutafuta maji; mazingira haya yanasababisha mimba za utotoni, ubakaji na vipigo kwa wanawake wakichelewa kutoka kuchota maji.

Na nyongeza ni kwamba muda mwingi na rasilmali vinatumika kusaka maji kitu kinachoongeza hali ya umaskini katika jamii ya watu hawa wa Kishapu.

Ukosefu wa huduma bora za afya ni suala jingine lililoibuliwa na mpango wa utafiti shirikishi wa uraghabishi. Mfano kati ya wanawake 20 walihojiwa katika Kijiji cha Ilota, Mbeya Vijijini ni mwanamke mmoja tu ndiye aliyetaja kujifungulia hospitali.

Umbali wa hospitali na vituo vya afya unawalazimisha wanawake wengi kuzalia nyumbani kwa wakunga wa jadi.

Hii ni hatari kwa mama na mtoto na kuna ukweli wa wanawake wengi kupoteza maisha wakati wa kujifungua na watoto kutopata huduma muhimu za chanjo wakiwa na umri chini ya miaka mitano.

Kata ya Kisaki, Morogoro Vijijini, tatizo si hospitali wala kituo cha afya, tatizo ni dawa na wahudumu wa afya katika vijijini vya Gomero, Stesheni na Nyarutanga. Vijiji hivi vina majengo mazuri, lakini hakuna dawa na wahudumu.

Mbali na tatizo hilo, pia inapobidi wananchi wanachangia gari la wagonjwa shilingi 70,000, ili kumpeleka mama mja mzito kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Hali hii ni hatari, maana wanawake wengi wanaweza kupoteza maisha yao kwa kushindwa kulipia hizo shilingi 70,000.

Ukiachia masuala hayo yaliyotajwa hapo juu, utafiti huu wa TGNP, ulibaini kwamba lipo tatizo la msingi ni uongozi mbovu na rushwa. Hili lilitajwa kila sehemu iliyofanyiwa utafiti.

Kwamba uongozi mbovu na rushwa vinasababisha ukosefu wa huduma za msingi kwa wanawake na wanaume walioko pembezoni.

Na kwamba kuna usiri wa taarifa za mapato na matumizi, viongozi kutowashirikisha wananchi katika masuala ya maendeleo, viongozi ngazi za vijiji kuruhusu video za ngono na viongozi kutotekeleza ahadi zao kwa wananchi.

Ni mengi yaliyojitokeza kwenye utafiti huu, ila yametajwa machache ili kufikisha ujumbe kwa wahusika, ili wajaribu kutafuta majibu ya kuondoa unyanyasaji wa wanawake na wasichana katika wilaya hizi zilizotembelewa na watafiti wa TGNP pamoja na maeneo mengine ndani ya taifa letu.

Mfano tatizo la maji linasababisha vipigo kwa wanawake, ubakaji, elimu duni kwa wasichana, mimba za utotoni na ukosefu wa kipato.

Serikali kuu na serikali za mitaa zinaweza kuyatumia matokeo ya utafiti huu kurekebisha matatizo yaliyoorodheshwa hapo juu: Mfano serikali kuirejesha ardhi ya Kata ya Mshewe inayomilikiwa na wawekezaji wa nje na ndani ya nchi, kwa manufaa ya wananchi sasa na vizazi vijavyo.

Pia serikali itenge maeneo ya wafugaji katika Kata ya Kisaki, ili kuepusha mapigano kati ya wakulima na wafugaji.

Huduma ya kupatikana maji safi na salama ishughulikiwe katika vijiji vilivyotajwa na ambavyo havikutajwa.

Utafiti huu umeonesha wazi kwamba maji safi na salama ni muhimu kwa Watanzania wote. Huduma ya hospitali pia iboreshwe. Pia ni muhimu kuwapo na mfumo wa kuwawajibisha viongozi wote wanaokiuka maadili ya kazi zao ili kuondokana na aina zote za rushwa na ukatili wa kijinsia hasa ukatili kwa wanawake na wasichana.

Lakini pia viongozi wawakilishi hususan madiwani na wabunge wanaweza kutumia matokeo ya utafiti kudai uwajibikaji wa serikali kwa wananchi katika ngazi zote kupita bajeti, ripoti ya mkaguzi wa serikali, kudai sera ya haki ya uhuru wa wananchi na mikakati mbali mbali ya maendeleo.

Vyombo vya habari, taasisi za utafiti na makundi ya kiraia yanaweza pia kuutumia mpango huu wa utafiti shirikishi wa uraghabishi kuibua masuala ya wanajamii na kujenga uwezo wa wanajamii kuhoji na kudai uwajibikaji.

Hapana shaka kwamba mpango huu wa utafiti shirikishi na uraghabishi ndio unafaa kabisa kubainisha chanzo cha vurugu za Mtwara. Mpango huu unamruhusu kila mshiriki kuzungumza bila kuogopa na kwa njia hii ya uraghabishi, watu wanajifunua na kujiweka wazi.



TUPE MAONI YAKO