Friday 15 November 2013

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI ZIARANI RUVUMA

 9

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM ABDULRAHAMAN KINANA ameanza ziara yake ya siku 23 katika Mikoa ya RUVUMA na MBEYA kwa kuanzia wilayani TUNDURU Mkoani RUVUMA ambako amekutana na kero ya wananchi juu ya matatizo ya zao la Korosho na kuwahakikishia kuwa Serikali ya CCM imeanza kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na matatizo hayo.


KINANA ambaye ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr ASHA-ROSE MIGIRO amesema Wizara husika na tatizo la Korosho tayari zimeagizwa kuchukua hatua za haraka kutatua matatizo ya Korosho na pia kunyang’anya viwanda vyote vya korosho ambavyo tangu vibinafsishwe havibangui Korosho

Karibu kwa katibu Mkuu wa CCM Komredi ABDULAHAMAN  KINANA hapa RUVUMA ilikua ni katika kijiji cha NAKAPANYA wilayani TUNDURU ambako yeye pamoja na katibu wa NEC Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr ASHA-ROSE MIGIRO wamekaribishwa kwa kilio juu ya zao la Korosho.

Kilio hiki kimetolewa mara baada ya KINANA kuvalishwa vai la Jadi la na kutunukiwa cheo cha Heshima kwa kabila la wayao cha SULTANI LINYAMA, na mvalishaji akatumia fursa hiyo kutanabaisha kuwa wananchi wapo taabani kutokana zao wanalolitegemea kuwaangusha


Majibu ya KINANA kwa Kilio hiki yakawa tayari Kamati Kuu ya CCM imeziagiza wizara husika kutafuta majibu haraka iwezekanavyo na kupeleka ripoti katika kikao kijacho cha Kamati kuu ya CCM lakini akabainisha kuwa Mchezo unaofanywa na wanunuzi wa Korosho hauipendezi CCM wala Serikali yake

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO