Tuesday 12 November 2013




          Katibu wa vijana ccm mkoa  Mwajuma   akiwa na kiongozi wa chipukizi

 Na Steven Augustino, Tunduru
 

VIONGOZI waliopewa dhamana ya kuwaongoza Wananchi kupitia tiketi ya
Chama cha mapinduzi Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wametakiwa kutimiza
wajibu wao kwa kutekekleza sera za chama hicho na kuwaletea maendeleo
wananchi katika maeneo yao.
 

Wilto huo umetolewa na katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
Bw.Abiniel Nzagule wakati akiongea na baadhi ya viongozi wa chama
hicho wakati wa mapokezi wa Makamanda 6 wa kikosi cha Girini gadi wa
 

Chama hicho yaliyofanyika katika Ofisi za kata ya majengo mjini hapa.
Aidha katika hotuba hiyo Bw. Nzagule aliwatahadhalisha Viongozi hao
kuwa endapo watashindwa kutimiza wajibu wao kwa wananchi Chama hicho
hakita jihuisha na Uchakachuaji wa kumbeba kiongozi yeyote na
kumuingiza katika kinyang’anyilo cha uchaguzi wa serikali za mitaa
unaotarajiwa kufanyika 2014 na Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na
Maduiwani.
 “

 wito wangu kwa viongozi waaliopo madarakani kupitia tiketi ya chama
chetu kuhakikisha wanawajibika ipasavyo wakati huu na kuwafanya
wananchi kurudisha imani kwao vinginevyo hali itakauwa mbaya sana kwao
katika chaguzi zijazo “ alisema Bw. Nzagule kuongeza kuwa bila wao
kujituma chama hakitakuwa na mbebeo ya kuwachukulia viongozi hao
katika chaguzi hizo.
 

Bw. Naagule aliendelea kufafanua kuwa katika mafunzo UVCCM Wilaya ya
Tunduru ilipeleka Makamanda 74 kati yao vijana 6 wakitoka katika kata
hiyo na kufanya idadi ya  Makamanda walioshiriki katika mafunzo hayo
kuwa na kikosi cha makamanda 400 walioshiriki katika mafunzo hayo
kimkoa.
 

Awali akitoa taarifa ya mapokezi hayo Diwanai wa kata hiyo bw.
Athumani Nkinde alimweleza Kiongozi huyo kata yake ilichukua uamuzi wa
kuwapeleka vijana hao 6 katika mafunzo hayo yaliyofanyika Kimukoa
Wilayani Namtumbo ikiwa ni tofauti na maelekezo ya Chama kutaka kila
kata kupeleka Vijana 2 na kuwaaghalamia wao wenyewe zikiwa ni juhudi
za kata hiyo kujiimarisha na kujiandaa na chaguzi zijazo.
 

Mwenyekiti wa umaoja wa Wanawake wa UWT Kata ya majengo Bi. Somoye
Nagi pamoja na kuwataja vijana hao kuwa ni Bw. Mohamed Omari, Juma
said, Asha Issa, Issa Athumani, Zainabu Njaidi na Bibie mapunda pamoja
na mambo mengine aliwahakikishia viongozi na Wanachama hao kuwa
mafunzo waliyopatiwa makamanda hao yamewasaidia kukitambua kukielewa
chama chao ipasavyo.
 

Akifunga mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi kata ya majengo
Bw. Jiramu saidi alitoa wito kwa watu wenye malengo ya kugombea
nyadhifa mbali mbali kuanza maandali ya kugombea nafasi hizo kuanzai
Uchaguzi wa serikali za mitaa kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo
watatimiza haki zao za kuchagua na kuchaguliwa na akawatoa hufu kuwa
hakuna kiongozi ambaye amepewa hati miliki ya uongozi ndaani ya chama
chao.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO