Thursday 30 October 2014

SAKAMIMBA TUNDURU MARUFUKU

SERIKALI Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma imepiga marufuku ngoma za Usiku ambazo zimekuwa zikichezwa na watoto wa Kike maarufu kwa jina la SAKAMIMBA.

Sambamba na marufuku ya ngoma hizo pia jamii imeaswa kuachana na utaratibu wa mila potofu za kuwacheza jando na unyago watoto wenye umri mdogo ili kuendelea kulinda maadili ya destuli za mwafrika. 
Aidha taarfa hiyo pia imewataka watendaji wa vijiji,kata na maafisa tarafa kuratibu, kusimamia na kuzuwia shughuli za Sherehe ambazo zitakuwa hazizingatii maadali katika maeneo yao.

Hayao yalisemwa na Mkuu wa Wilayab ya Tunduru Bw. Chande Nalicho wakati akiongea na wananchi wa Kijiji cha songambele kilichopo katika tarafa ya Nakapanya wilayani himo na akawataka wananchi kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinaratibiwa na kutekelezwa kwa Watoto wenye umri mkubwa ikiwa ni tofauti na sasa ambapo wazazi na walezi hao wamekuwa wakiwacheza wakiwa na umri mdogo.

Akifafanua taarifa hiyo dc, Nalicho alisema kuwa mtindo wa wanafamilia hao kuwapeleka na kuwacheza unyago kwa watoto wa kike na jando kwa watoto wa kiume wakiwa na umri mdogo umekuwa ukidhalilisha utamaduni wetu.
Alisema kwani baada ya watoto hao wenye umri mdogo baada ya kumaliza mafunzo hayo huenda kutoa siri za mafunzo hayo kwa wenzao na kufanya majaribio kwa vitendo mambo yote waliyojifunza.

“mafunzo hayo ni hatari na nijanga kubwa hasa kwa watoto wa kike ambao baada ya kumaliza mafunzo hayo huenda kufanya majaribio kwa vitendo mambo yote waliyojifunza” alisema Dc, Nalicho.
Alisema kufuati jamii kuendelea kupuuza taratibu za kutekeleza wajibu wao katika malezi ya Watoto wao hasa wakike vitendo hivyo ndivyo ambavyo vimekuwa vikipelekea watoto wa kike kupata mimba wakiwa katika umri mdogo.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO