Tuesday 12 February 2013

Wazee wamtoa machozi Mbunge Majimarefu


Na Yusuph Mussa, Korogwe

MBUNGE wa Korogwe Vijijini, mkoani Tanga Bw. Stephen Ngonyani maarufu 'Majimarefu', amemwaga machozi baada ya baadhi ya wazee wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mombo, kumweleza ukweli juu ya vita aliyonayo ndani ya CCM.


Walidai pamoja na juhudi kubwa anazofanya ili kutatua kero mbalimbali za wananchi, bado ana changamoto kubwa ya
kupingwa na baadhi ya wanachama wenzake.

Wazee hao waliyasema hayo juzi katika mkutano wao na Bw. Ngonyani uliofanyika katika Mji wa Mombo ambapo pamoja
na mambo mengine, walidai baadhi ya wana CCM wenzake wanamhujumu kwa kushindwa kuitangaza miradi
aliyoitekeleza kupitia ilani ya chama hicho.

Bw. Nyongani alilazimika kutoa machozi baada ya Bi. Mwanaisha John, kusema tangu Tanzania Bara ipate uhuru wake, hajawahi kuona mbunge aliyekaribu zaidi na wananchi jimboni humo kama ilivyo kwa Majimarefu lakini bado anapigwa vita na wana CCM.

Naye Bw. Hussein Kijemkuu, alisema wakulima wamekuwa watumwa katika nchi yao kutokana na wafugaji kutumia fedha
ili kuwadhalilisha na kuharibu mazao yao kwenye bonde la Kwamkumbo, lakini hakuna hatua wanazochukuliwa.


“Wafugaji wanatunyanyasa na kudai hatuwezi kuwafanya lolote
na kusisitiza katika makundi ya ng'ombe wao, wapo wa diwani
(jina linahifadhiwa) na Ofisa Tarafa,” alisema Bw. Kijemkuu.

Akipokea kilio hicho cha wananchi, Bw. Ngonyani alisema yeye ataendelea kuipenda, kuitumikia CCM mbali ya kupigwa vita na baadhi ya viongozi wa chama hicho ngazi mbalimbali kwani
yeye yupo kwa ajili ya kuitetea ilani ya chama tawala.

Katika hali isiyo ya kawaida, chama hicho Wilaya ya Korogwe Vijijini kimemeguka vipande viwili, kundi la moja likimuunga
mkoano Bw. Nyonyani na kujiita CCM A, wakati kundi jingine
linamuunga mkono Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Korogwe Vijijini, Dkt. Edmund Mndolwa ambalo ni CCM B.

Akizungumza na Majira, Katibu wa CCM wilayani humo, Bi. Elly Minja, alikana chama hicho kumeguka vipande viwili lakini alidai kuwa, awali kulikuwa na mgogoro kati ya Bw. Ngonyani na Dkt. Mndolwa ambao hivi sasa wamepatanishwa.

Chanzo Majira

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO