Saturday 14 September 2013

KINANA SHINYANGA KUNUFAIKA NA VIWANDA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi katika uzinduzi wa mradi wa vibanda vya biashara katika uwanja wa Kambarage huku akishuhudiwa na Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqinq.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwa baiskeli kutoka Uwanja wa Kambarage kuelekea uwanja wa Shycom kwenye mkutano wa hadhara.
Balozi wa China nchini Dk.Lu Youqinq akiwapungia wananchi wakati akielekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Shycom,Shinyanga mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Balozi wa China nchini wakiwasubiri wenzao tayari kuelekea kwenye uwanja wa Shycom ambapo mkutano mkubwa ulifanyika.
Kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Balozi wa China nchini na Mbunge wa Shinyanga mjini Steven Masele wakiendesha baiskeli kuelekea kwenye uwanja wa Shycom ambapo mkutano mkubwa na wa kihistoria ulifanyika leo tarehe 13 Septemba 2013.
 
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiingia kwenye uwanja wa Shycom na baiskeli tayari kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara.
 
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto),Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqinq na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye , Balozi wa China alipata fursa ya kuelezea kwa wananchi wa Shinyanga namna uwekezaji utaweza kuunufaisha mkoa huo ambapo viwanda vya nguo, kusindika mafuta, asali na bidhaa zitokanazo na mifugo vinategemewa kujengwa katika mkuo huo na kutoa nafasi kwa ajira ,kuinua uchumi ,elimu na kuondoa kabisa umasikini.
 
BY JOHN BUKUKU

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO