Monday 2 September 2013

 Na Steven Augustino, Dodoma
Serikali Imekiri kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani unakabiliwa  na
changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa usimamizi,uadilifu wa watendaji,
viongozi wa vyama msingi vya ushirika hali ambayo imesababisha
wakulima kuendelea kunyonywa na kudhurumiwa.

Hayo yamebainishwa jana Naibu waziri wizara ya Kilimo, chakula na
ushirika Adam Malima wakati alipokuwa anajibu  hoja za wajumbe wa
mkutano  wa siku mbili wa wadau wa tasnia ya korosho uliofanyika
mjini Dodoma.

Aidha Waziri Malima alisema kutokana  na changamoto hizo zote  wizara
imechukua jukumu la  kufanyiwa kazi, kwa kupeleka muswada wa kisheria
na wizara ya viwanda na Biashara, utagusia zaidi juu ya mfumo ili
kuboresha  kwa lengo la kuwaondolea adha wakulima wa zao hilo.

Akichangia mada hiyo katika mkutano huo Mkuu wa wilaya ya Liwale
Ephraim Mbaga alisema mfumo huu wa staabadhi ghalani umekosa mwelekeo
kutokana na  wakulima  kutolipwa fedha zao za malipo ya pili hali
iliyosababishwa  vurugu kwa baadhi ya  maeneo  hali iliyopelekea mali
za madiwani, mbunge kuchomewa moto katika wilayani Liwale.

Mmbaga alisema chanzo kikuu ni kutokana kutolipwa malipo yao ya pili
ya sh 600  kama ilivyotangazwa na bodi ya korosho katika msimu
uliyopita kwa visingizio kuyumba kwa soko la dunia.

Mwingine aliyepata nafasi ya kuwatetea Wakulima wa zao hilo alikuwa
Naibu waziri wa nchi  Tamisemi katika ofisi ya waziri mkuu Kassimu
Majaliwa na kusema kuwa umefika wakati wa idara husika kuridhia maombi
ya wakulima wa wilaya za Liwale, Nachingwea na Ruangwa ambazo
zimeazimia kujiondoa kutoka chama kikuu cha ushirika mkoa wa Lindi
Ilulu  waanzishe chama kwao.

Alisema ili mfumo huo wa stakabadhi mazao ghalani uweze  kuondoa
changamoto zilizokuwapo wakulima hao wameamua kuanzisha chama  kwa
lengo la kuboresha utekelezaji.

Naye Mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila alikiambia kikao hicho
kuwa mkulima anaanza kuibiwa kuanzia vyamavya ushirika alitoamfano
alikusanyiwa kilo kumi akilipwa fedha za kg Nane, kwa kama kuna
wakulima wapatao zaidi ya 100 wanachukuliwa zaidi ya kg 50 kwa hiyo
mtendaji wa ghala anakuwa na uwezo wa korosho zaidi ya tani 200 bila
ya kulima.

Mwananzila alisema vyama vya msingi havikuna wataalamu wa mahesabu
hali yo inasababisha kuingia mikataba na taasisi za fedha mwisho wa
siku wanakuwa na madeni ambayo yanakuwa  mali  ya wakulima ambayo
ulipa bila kushirikishwa

Mwishoooo

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO